Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,553
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amewasili nchini leo Julai 26, 2023 kutoka Ulaya.
Akihojiwa juu ya kuitikia wito wa DCI Kingai unaomtaka afike ofisini kwa mahojiano, Lissu ametoa kauli inayoashiria kuwa hatakwenda.
“Kwenda (kwa DCI) kufanya nini? Unapoitwa na Polisi mahali popote lazima polisi akuambie anakuitia kosa gani. Ile barua imesema kuna kosa? ……”
Baada ya kutoa kauli hii Lissu aliondoka. Kauli hii inatoa tafsiri kuwa Mwanasheria huyo nguli hatokwenda ofisi ya DCI iliyompa wito wa kufanya naye mahojiano kufuatia matamshi aliyotoa kama alivyonukuliwa akisema kauli za Rais ni matope.
Pia soma: Tundu Lissu: DCI Kingai kaniandikia barua ya wito wa kuripoti ofisini kwake. Nipo nje ya nchi, wiki ijayo narudi kumkabili