Tundu Lissu: Tutazichapa bungeni kuzuia mswada haramu wa vyombo vya habari

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni Tundu Antipass Lissu ameionya vikali serikali ya CCM dhidi ya mpango wa kuleta mswada haramu wa kudhibiti vyombo binafsi vya habari nchini.

Lissu amesema wabunge wa Ukawa watatumia njia yoyote hata ikibidi kupigana ndani ya bunge hilo ili kuzuia upokwaji wa haki ya Watanzania.

Lissu amesema lengo la mswada huo ni ili kuhakikisha ni habari tu za CCM zinatangazwa hasa katika kipindi cha uchaguzi kwani itakuwa ni marufuku TV binafsi kutangaza Taarifa ya habari badala yake TBC pekee inayomilikiwa na CCM ndiyo itakuwa na haki hiyo.

Lissu ameapa kwamba kamwe hawataruhusu mswada huo kusomwa bungeni.

Source: ITV
Chama cha Demokrasia na mandeleo Chadema kimesema kita hakikisha kina pinga vikali mswaada wa sheria wa vyombo vya habari unao tarajiwa kupitishwa bungeni usipitishwe, kwasababu una lenga kukandamiza vyombo vya habari vya watu binafsi.

Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa Singida mashariki Mhesimiwa Tundu Lissu amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara wilayani Ikungi, na kusema kuwa lengo la serekali ni kuwarudisha watanzania miaka ya nyuma, ili kuweza kuficha maovu yanayo tendeka ndani ya serekali kwa kutumia chombo kimoja cha taifa cha habari.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Tundu Lissu amewataka wananchi wa jimbo la Singida mashariki kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa wingi, kwa kufanya hivyo watakuwa na nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi mkuu kama jinsi walivyo fanikiwa kushinda katika uchaguzi wa serekali za mitaa kwa kupata ushindi wa zaidi viti arobaini huku CCM ikiambulia viti tatu.

Akiongea na maelfu ya wakazi wa jimbo la Singida mashariki waziri kivuli wa maliasili na utalii na mbunge wa Iringa mjini Mheshimiwa mchungaji Peter Simioni Msigwa, amesema baadhi ya viongozi wa CCM wame hujumu nchi kwa kutorosha maliasili nyingi hapa nchini, na kumekuwa na rushwa karibu katika sekta zote hata kusababisha huduma muhimu kama hospitali kukosa madawa, kutokana na hali hiyo Chadema imeamua kusimama imara na kutembea nchi nzima kuwaeleza wananchi na ili waweze kujua wachague chama gani katika uchagu mkuu unao kuja.

Katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na mamia ya wakazi wa jimbo la Singida mashariki wakiwemo wachungaji wa makanisa mbalimbali mashehe na wananchi wa jimbo hilo wameonyesha niayao ya kumrudisha mbunge wao kwasabau ya kuwatetea wananchi kuacha kuchangia michango maendeleo ambayo inatakiwa kutolewa na serekali.
 
Kuzichapa siyo issue bungeni siyo uwanja wa masumbwi ni hoja tu maana wabunge wengi hata wa ccm wanapinga musuada huu
 
Katika hili naunga mkono 1000%.ukawa msiruhusu mswada huo ukaingia bungeni. ukiingia tu simameni na pigeni kelele mpaka huo mswada uondolewe kwenye ratiba. ccm imeamua kuwaziba mdomo na masikio watanzania. wabunge wetu wazalendo igeni kenya hakuna kuchekea ujinga.
 
Molemo

Kwa watawala wetu wa CCM kupeleka muswada huo kandamizi wa kuminya uhuru wa kupata habari, ni dhahiri kuwa hao magamba maji yapo shingoni.
 
Last edited by a moderator:
Hapa bila ngumi mswada utapitishwa maana magamba magumu wamejaa bungeni! Natamani na mm niende nikawaunge mkono! Tena na usongo na wale wabunge vichwa ukoko!
 
Ataishia kutolewa nje na kura ya ndiyo itapigwa, atumie akili sio sarakasi wala karate,Bungeni sio uwanja wa masumbwi
 
Akili ya mgomvi inawaza ngumi badala ya hoja, Mhe.Lisu tumia akili utaishia kukabwa na askari na kutupwa nje afu uisome namba!
 
Naunga mkono Hoja!! huu upuuzi waotaka kuleta wa kulazimisha watu kuangalia TBCCM haukubaliki hata kidogo

Wengine TBCCM hatuangalii hata kwa bunduki
 
Tukisema hiyo sheria ni kandamizi na hatuitaki,kama hawasikii tutawachapa tu,na wananchi tunasema wapigwe tu.
 
Naunga mkono Hoja!! huu upuuzi waotaka kuleta wa kulazimisha watu kuangalia TBCCM haukubaliki hata kidogo

Wengine TBCCM hatuangalii hata kwa bunduki

Lisu ni mwanansheria aje hapa atupe component nzima ya huo muswaada vipengele vyote na sio kimstari kimoja cha tbc tu muswaada sio tbc
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom