Tundu Lissu: Tutazichapa bungeni kuzuia mswada haramu wa vyombo vya habari

Mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni Tundu Antipass Lissu ameionya vikali serikali ya CCM dhidi ya mpango wa kuleta mswada haramu wa kudhibiti vyombo binafsi vya habari nchini.

Lissu amesema wabunge wa Ukawa watatumia njia yoyote hata ikibidi kupigana ndani ya bunge hilo ili kuzuia upokwaji wa haki ya Watanzania.

Lissu amesema lengo la mswada huo ni ili kuhakikisha ni habari tu za CCM zinatangazwa hasa katika kipindi cha uchaguzi kwani itakuwa ni marufuku TV binafsi kutangaza Taarifa ya habari badala yake TBC pekee inayomilikiwa na CCM ndiyo itakuwa na haki hiyo.

Lissu ameapa kwamba kamwe hawataruhusu mswada huo kusomwa bungeni.

Source: ITV

Wanatumiwa na Mengi anajua sheria ikipita itamlazimisha piakuwalipia Bima Waandishi wake wote!
 
Inaweza kuwa ni sera lakini siyo siasa. Siasa ni kinyume cha kupigana.

Kinacho angaliwa hapa ni kipi kitakacho kufanya upate ukombozi au kitakacho kufanya upate ukombozi kwa haraka zaidi.

Sasa kama umepiga siasa wee,umeona hazisaidii kukufikisha kwenye malengo na yule unayempigia siasa ana ona ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,hapo kuna sababu ya kutokuzichapa?wakati dalili zote zinaonyesha kuwa ili upate haki ni lazima mchapane.
 
Kinacho angaliwa hapo ni kipi kitakacho kufanya ufikie ukombozi aufikie ukombozi kwa haraka zaidi.

Sasa kama umepiga siasa wee,umeona hazisaidii kukufikisha kwenye malengo na yule unayempigia siasa ana ona ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,hapo kuna sababu ya kutokuzichapa?wakati dalili zote zinaonyesha kuwa ili upate haki ni lazima mchapane.

Huyo anatumika tu na atakua kaahidiwa na Mwenyekiti wa MOAT kupatiwanmuda kwenye Tv yake na atapigana kweli maana alipokua akisomea sheria kule wanakopigania IS aliambiwa akiwa mahakamani kama wakili anaruhusiwa kupigana
Ili ashinde kesi yake!:boxing::boxing:
 
Tukundane inaelekea wewe ni mkimbizi hilo jina umelipata wapi?ndo maana huna uchungu na manyanyaso wanayopata waandishi wa habari dhidi ya MOAT.

Huruma kama hizi mngezionyesha siku Ile ambayo mtu wenu Pinda alipo sema kuwa wapinzani wapigwe tu,mngeonekana ni watu wamaana.

Leo kibao kimewageukia kuwa ninyi ndio mnaotakiwa mpigwe,mmeanza kuweweseka,mnaweweseka nini tulieni zipigwe,wapinzani walioagizwa kupigwa na Pinda nao ni watanzania kama ninyi.

Halafu inakuwaje ujiite jina la mpiganaji Kinjekitile halafu unaogopa kuzichapa,wewe ni Kinjekitile feki nini.
 
Huyo anatumika tu na atakua kaahidiwa na Mwenyekiti wa MOAT kupatiwanmuda kwenye Tv yake na atapigana kweli maana alipokua akisomea sheria kule wanakopigania IS aliambiwa akiwa mahakamani kama wakili anaruhusiwa kupigana
Ili ashinde kesi yake!:boxing::boxing:

Ha ha ha sawa Kinjekitile junior mpiganaji muoga kama kunguru,Kinjekitile angekuwa muoga kama hivyo sidhani kama kwenye orodha ya mashujaa angekuwemo.
 
Ha ha ha sawa Kinjekitile junior mpiganaji muoga kama kunguru,Kinjekitile angekuwa muoga kama hivyo sidhani kama kwenye orodha ya mashujaa angekuwemo.

Huna tofauti na kale kazee kalikokuwa Arusha wiki iliyopita....Ukoo wa Panya
 
Back
Top Bottom