Tundu Lissu Live ndani ya HOTMIX EATV

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Baada ya ccm kuingia kiwewe na kufanya hujuma watu wasipate elimu juu ya katiba pendekezi na kumdhalilisha mzee wetu jaji warioba leo wanaingia kwenye mtihani wa pili pale ambapo Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu atakuwa ndani ya kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV leo tarehe 4-11-2015 kuanzia saa 12:00 jion lissu atakuwa akifunguka kuhusu Katiba pendekezi.

Sasa kwa wale wasiotaka watu wajadili na kupata elimu kuhusu katiba pendekezi na leo wasimame na Mabango yenye jumbe tofauti mbele ya Tv zao Lazima watawala wafike mahala na kukubali ni vigumu kuzuia maji kupita kwenye mkondo wake.

Watz wote kaeni mkao wa kula kuanzia saa 12 jioni Lissu atatoa elimu hiyo bure na Live!
Karibuni!!!
 
Mkuu.
Tutamsikiliza nguli wa sheria na mwanasiasa mahiri Mh. T. Lissu.

Ninaomba uchambuzi wao wauandae vema kisha waweke you tube ili kuweza kufanya rejea.
 
poa kamanda asante! ila wanaweza wakate umeme

Ingia kwenye maombi mkuu umeme wa TZ kwa sasa kama unajambo la muhimu unataka kuangalia laZima uzame kwenye maombi la sivyo utabaki kusimuliwa tu!!!
 
Tindu lisu katiba pendekezwa kila ukinyaka tu unapigwa na haki, haki ya wakulima haki ya wafugaji, haki ya wazee, ya vijana, ya wazee, ya wasanii na nyingine nyingi , lkn hadhipelekeki mahakamani, sasa kama uhuwezi kwenda mahakani hiyo ni haki?
 
Hana jipya. Yupo kama mtu aliyechanganyikiwa. Ni wa kumpuuza.
 
Asubuhi alitema nondo channel ten, jioni EATV na kesho asubuhi tunataka TBCCM akaue ..!
 
Shukrani kwa kutupatia taarifa mapema. Nilikuwa na appointment saa 12 lakini imebidi ni-cancel
 
Nipo macho lakini ngoja niset na alarm kwenye simu yangu ili nisijekupoteza hata nukta kumsikiliza Lissu.
 
Na asubuhi alikuwa channel 10 kumbe wajumbe wa Zanzibar hawakufika125 ila Sitta kadanganya ni 148
 
TBCCM hawatampa nafasi...vinginevyo wakifanya hivyo ajira ya mkurugenzi wao itakuwa matatani.

Hivi tbc bado inarushaga matangazo mkuu?miaka kadhaa sasa sijaiangalia.
 
Back
Top Bottom