Kimsingi, ili wananchi waendelee kuchangia ni lazima pawepo na taarifa za mapato na matumizi yote ya fedha. Wengi wamezoea kuburuza wananchi na kuwalazimisha kulipa kodi. Kama hao madiwani wana ubavu basi walazimishe wananchi kuchangia kama wanavyotaka kulazimisha Mbunge wa wananchi akajieleze kwao. Ni aibu wawakilishi wa watu kushirikiana na chombo (serikali) kukandamiza wananchi badala ya kupanga mipango ya maendeleo pamoja. Ni wajibu wa halmashauri kuweka wazi taarifa zote kwa uwazi ndipo wananchi wachange. Vitisho kwa mbunge halali wa wananchi sio suluhisho la matatizo ya wananchi bali uwajibikaji na utiii wa sheria zilizopo.