Tundu Lissu ana deni kubwa jimboni, achukue tahadhari!

wanachadema wenzangu taarifa kama hizi si za kupuuza hasa katika hiki kipindi kigumu,hivyo ni muhimu kwa watu walio karibu na tundu lissu kumueleza haya na kama ni kweli ni kuyafanyia kazi! 2015 hatutakiwi kuacha jimbo jamani!

I second on you, Binafsi napenda nione mabadiliko chanya katika nchi yangu na sii kushabikia kila kitu kinacho enda kinyume na wana-chadema.. Kama kweli Wild fauna ni mwana-jimbo huko singinda ni vyema mawazo yake yachukuliwe kwa busara na si kupinga tu.

Binafsi naona chadema kwa sasa waelekeze Nguvu zao huko vijijini na si kila leo kuitisha mikutano mijini..

Naongea hivi kwa lengo la kukijenga chama ki-ushauri napenda nione chadema wakifanya kile kinachotarajiwa na wengi..
 
Last edited by a moderator:
Hao wananchi wa huko kwa Lissu mbona vilaza sana, walimchagua kama Mbunge au Mfadhili?? Kama mbunge tumesikia akitoa hoja kibao bungeni kutimiza wajibu wake lakini kama walimchagua awe mfadhili wamebugi wangemchagua Manji awe mbunge/mfadhili wao. Jukumu la kuchimba visima ni la serikali, mbunge anasimamia utekelezaji kupitia mfuko wa jimbo au halmashauri. Cha kushangaza wanamlaumu Lissu halafu wanasifia Mwigulu Nchemba...

Samahani,naomba niwe tofauti kidogo nawe.
Naanza kukubaliana nawe kuwa Lissu hajachaguliwa na wana Singida Mashariki kuwa mfadhili,lakini ubunge wake kaupata kutoka kwa hao watu, tena kutokana na ahadi alizozitoa kipindi cha kampeni, na uwezo wake wa kushawishi wana Singida kumchagua yeye (Lissu).
Hizo hoja anazozitoa bungeni (ambazo nyingi ni za maeneo mengine na siyo jimboni kwake) angezitoaje kama asingepata fursa ya kuchaguliwa na watu wa Jimboni kwake...? Au labda angepata zali kama lile la Mbatia....?
Mimi japo napenda kuona TL akirejea bungeni na pia kuwapo kwa ongezeko la wabunge wengi zaidi wa upinzani, ningeona ni vizuri hawa wabunge wetu wabalance mambo, wajadili mambo ya kitaifa ili kuwasemea hata wale wabunge mabubu, lakini wakumbuke kuwakilisha mahitaji ya majimbo yao, vinginevyo wengine wanapiga jalamba tu kwani ndo wanaamini wananchi wao hawasikii matatizo yao yakiwasilishwa bungeni.
 
nyie mbulula mmejipanga kuanzisha thread alafu mjijibu harakaharaka hii haita wasaidia nyie ni k. tu na ndo mana nimewajibu kwa ujumla wenu najua mnajijua.....ahadi za jk. hamziongelei mmebaki na lissu mnyika na lema wa arusha nashauri mjipange upya wa tz wa sasa sio wale mliowazoea ur all silly.
 
Jamani CCM njooni huku kwa Tundu Lissu jimbo limemshinda kabisa, halitukataza kuchangia shughuli za maendeleo akadai yeye atapigania maendeleo sasa huku hakuna jipya alilofanya zaidi ya kumsikia kwenye vyombo vya habari, madiwani wake wa CDM wamejiudhuru sasa atafanya kazi na akina nani? amekuwa bingwa wa lawama badala ya kutekeleza majukumu yake. kiongozi asiyepigania maendeleo hatufai. tunasikia atakimbilia jimbo la Singida mjini uchaguzi wa 2015 jamani huyu jamaa ni kimeo hafai huku tumemchoka. CHAMA CHA MAPINDUZI KARIBUNI SANA MUENDELEE KUWAJIBIKA.
 
We umetokea wapi, Lumumba vipi ?
Tueleze ni ahadi gani aliitoa Tundu Lissu ambayo hajaitekeleza ?

Bwana mdogo acha mbwembwe za kwenye key board; Tundu Lissu ni machine nyingine; kama huamini mshauri muishiwa dhaifu na serikali yake akagombee ubunge kwenye jimbo la Lissu uone kitakacho mkuta.
 
Ngoja labda tumuite mulugo aje arekebishe elimu huko kwenu labda mtaamka usingizini.
 
Mkuu ulikua wapi umeniwahi hii thread mkuu, nilikutana na baadhi ya wanajimbo wake, wanamlalamikia sana huyu mjamaa, wanadai kawasahau, kabisa, hakuna mambo ya maendeleo aliyoyafanya huko kwao, na kama asipojirekebisha ataukosa ubunge tena 2015...kazi anayo
 
Kwani kabla ya Tundu Lissu miaka yotehilo jimbo lilikuwa chini ya nani hadi likakosa maendeleo?
 
Kwa hiyo unawaita CCM waje huko kutokea wapi? Kwani Singida hakuna Uongozi wa CCM? au unataka CCM Makao Makuu ndio waje?

Suala la madiwani kujiuzulu linazuia vipi Mbunge kutetea wananchi na kuisimamia Serikali? Na hizo ahadi ambazo ametoa Lissu na hajatekeleza kwani JK alipokuja hapo alitoa ahadi gani na ipi ametekeleza? Inshort kama hakuna chochote kilichofanyika hapo basi JK hakutimiza ahadi zake.
 
Jamani CCM njooni huku kwa Tundu Lissu jimbo limemshinda kabisa, halitukataza kuchangia shughuli za maendeleo akadai yeye atapigania maendeleo sasa huku hakuna jipya alilofanya zaidi ya kumsikia kwenye vyombo vya habari, madiwani wake wa CDM wamejiudhuru sasa atafanya kazi na akina nani? amekuwa bingwa wa lawama badala ya kutekeleza majukumu yake. kiongozi asiyepigania maendeleo hatufai. tunasikia atakimbilia jimbo la Singida mjini uchaguzi wa 2015 jamani huyu jamaa ni kimeo hafai huku tumemchoka. CHAMA CHA MAPINDUZI KARIBUNI SANA MUENDELEE KUWAJIBIKA.

Hao madiwani wameomba udhuru kwenda kujisaidia au?? Hebu funguka mkuu...

Bahati nzuri wenzio maCCM wanamfaham vizuri huyo, unachowaambia ni sawa na mtu kukwambia ''njoo fasta hapa Serengeti simba dume amelala njoo umshike sharubu''

Heri W.P. Slaa (PhD) awe rais kuliko Lissu ashinde ubunge,,,, by J.M. Kikwete
 
Sio kila mtu anaweza kuwa kiongozi.Yule ni mwanaharakati tu.na mwanasheria mzuri sana lakini sio kwenye siasa.
 
Acha ujinga wewe,Tundu hajatokezea ktk chombo chochote kueleza atagombea singida mjini,acha kueneza ujinga wako..wewe ni gamba zito lenye ukurutu unukao,eti maendeleo si ufanye wewe yani tundu aje hadi ktk familia yako?mpumbavu mkubwa wewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom