Tundu Lissu ana deni kubwa jimboni, achukue tahadhari!

kwani serikali inaanzisha miradi kwa kutegemea michango ya wananchi? Wananchi wanalipa kodi,kodi zao zinaenda wapi? Serikali isipate kisingizio cha kutafuna hela za walipa kodi kwa mgongo wa lisu.ni upumbavu kuanzisha miradi kwa kutegemea michango ya wananchi.kwani pesa ambazo zinanakuwa alocated kwa ajili ya maendeleo ya jimbo yanaenda wapi? Kazi ya mp ni kuipush Gv deliver maendeleo kwa wananchi.hayo ya michango ni mbinu mbadala wa kuwanyonya wananchi in the name of maendeleo.
 
Real,LISSU ni jembe but ameshindwa kutimiza ahadi jimboni. Siyo visima tu hata roads, mi ni mbunge wangu, ccm wameanza kukosoa hayo, aangalie...
 
ana udhuru, kesi hizi nazo zinapoteza muda kwahiyo hawawezi kumlaumu kwa lolote.

huu ni ushabiki wa kijinga, Lisu yuko bungeni kwa kura za wana sgd mashariki, je wakimtosa mtaaenda nyie wana jf na bibi zenu mkampigie kura? Hakika lisu ukiendelea kulishwa huu ***** na wana jf itakua aibu kwako na chama pendwa CDM. Mtoa mada kasema iliyo kweli na hali ilivyo jimbo, mijitu mnakuja na hoja za kishabik na za kipumbavu, Lisu, its high tym to make sort of mobilization internally n externally kuleta maendeleo.
 
Nakubaliana na mtoa mada kuwa Lissu anapaswa kutimiza ahadi zake lakini pia sina uhakika wa asilimia nyingi kuhusu mtazamo wa Wananchi kama upo kama alivyoelezwa mtoa mada na huyo anayemuita msomi kwamba kutochimba visima inaweza ikawa sababu ya kummwaga Lissu hapo 2015. Kama ni hivyo, je mtu kama Bi.Kidude ambaye yupo bungeni tokea akiwa binti hadi ss hv kachimba visima vingapi huko jimboni kwake Njombe?

Wananchi wa Singida ni waelewa na sitarajii kuwa watachukulia visima kuwa ni kigezo kikuu cha kumnyima kura Lissu, bado wengi sana tuna imani na Lissu. Tuangalie pia vikwazo alivyo kuwa navyo ktk kutimiza malengo yake jimboni ndipo tutakapoona umuhimu wa kuendelea kuwa nae na kumtia moyo ktk kuendelea kututumikia.

NI MTAZAMO TU!!!
 
Tundu Lissu anafanya kazi ya kuziba mianya ambayo imefanya asipate hivyo visima hivyo si sawa kusema hajatimiza ahadi zake alizotoa huko Jimboni. Ili kumhukumu vilivyo apewe muda na pesa zirudi ndipo tuone kushindwa kwake.
 
too low men,
kama aliahidi atimize kwani hakujua kunafitina,kwanini kila kitu tunatumia ccm as reference?
 
Kwamba Lissu aliahidi kujenga visima ina maana gani? achukue jembe achimbe au achukue fedha zake zigharimie uchimbaji visima? Au una maana ya kuisimamia serikali ili ijenge visima?Wachangiaji wamekumbusha wajibu wa mbunge, huu wa kujenga visima ukoje? Tukubali kwamba aliahidi na akashindwa kujenga, hivi kama angekuwa hajaahidi hamna lolote ambalo mnaona yeye kama mbunge ana deni kwenu?

Hata kama ameshindwa hilo kama ilivyosemwa lakini mbona kwa upande mwingine amefanya mengi hasa suala la kuiwajibisha serikali kwa kutumia vikao vya bunge?
Mkuu nlichosema ni kua mbunge tulishamwambia na kasema atatekeleza ahadi na hajashindwa....sasa we unachopinga ni nini? Na im sure he mean that atatekeleza.
 
samirnasri

Unakosea sana kuanza kumlaumu m2 mwenye miaka miwili tu ktk ubunge na chama kilichokaa madarakani kwa miaka hamsini wakati pia unaelewa pia kuwa chama tawala kinafanya ghiliba kuzuia migao ya fedha kwenda ktk majimbo yanayoshikiliwa na upinzani kama ulivyosikia wiki iliyopita.

Kwa mpenda maendeleo yeyote anaweza kuelewa kuwa tumetawaliwa na CCM tokea uhuru lakini maji na barabara achilia mbali hospitali na shule bado tuko nyuma zaidi ya nchi ambazo bado zipo vitani kwa muda mrefu saana.

Hivyo wananchi wa Singida nikiwasikia wanamlaumu huku wanayafahamu haya yote nitawashangaa sana tu!! Watakuwa ni sawa kama wanapiga hatua moja mbele mbili nyuma. Hata hivyo sikupingi kwani unaonekana una nia njema na mabadiliko ya nchi hii.
 
Last edited by a moderator:
Kat ya wabunge wa cdm ambae kurudi kwake 2015 ni kwa mashaka ni huyu mh.lisu..hadi sasa hakuna kitu cha maana alichowafanyia wananchi wa jimbo lake..kila ukipita vijijini mitaa ni kelele huyu mbunge hakuna kitu kazi kutaka sifa tu na kubaki zaidi na kazi za chama chake ni maneno ya vijana kwa wazee... Lisu tekeleza ahadi kutaja majaji sijui nini hakuwasaidia wananchi
 
Mpigakura unayelalamika kuwa mbunge hajatekeleza ahadi lakini unashindwa japo kutaja ahadi moja ambayo Lissu hajatekeleza
 
Kat ya wabunge wa cdm ambae kurudi kwake 2015 ni kwa mashaka ni huyu mh.lisu..hadi sasa hakuna kitu cha maana alichowafanyia wananchi wa jimbo lake..kila ukipita vijijini mitaa ni kelele huyu mbunge hakuna kitu kazi kutaka sifa tu na kubaki zaidi na kazi za chama chake ni maneno ya vijana kwa wazee... Lisu tekeleza ahadi kutaja majaji sijui nini hakuwasaidia wananchi

Mnapenapasiana kama mpira wa miguu.

Alikuwa nape na kadi kwa Dr slaa

Akaibuka tena nape kwa JJ Mnyika

Sasa wewe unakuja na Mh Tundu lisu.

Hao wapigakura katika jimbo la Lisu ulikutana nao katika kikao gani cha lini na maazimio ya kikao hicho yalikuwa nini chini ya

mwekiti gani?
 
Juzi nilikutana na rafiki yangu mmoja ambaye ni msomi wa shahada ya uzamili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam na ni mzaliwa wa Singida Mashariki, jimbo linaloongozwa na Lissu. Tukiwa safarini tulianza kusimuliana mambo mbalimbali yaliyokuwa yamejiri bungeni jana yeke. Nilimsimulia rafiki yangu juu ya muongozo uliokuwa umeombwa na Lissu kwa spika baada ya spika kubatilisha hoja ya zitto kabla hoja hiyo haijafika mezani kwake. Nilimsifu Lissu nikasema yule jamaa ni JEMBE kweli.

Jamaa yangu aliniambia kweli Lissu ni jembe lakini haoneshi u-jembe wake jimboni kwake. Nilishtuka na kumwambia aache utani akaniambia habari ndo hiyo kwamba Lissu amekuwa moto bungeni lakini jimboni kwake ameshindwa kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni. Nilimuomba anithibitishie maneno hayo kwani sikuamini kama Lissu angewasaliti wapiga kura wake. Jamaa akaniambia wakati wa kampeni Lissu aliahidi visima 12 endapo angechaguliwa kuwa mbunge na kwamba chama chake cha CHADEMA kiliahidi kumuonezea nguvu ya kujenga visima hivyo, lakini takribani miaka miwili sasa Lissu hajachimba kisima hata kimoja na kwamba wananchi wengi wamekata tamaa na wameahidi kumuhukumu katika uchaguzi mkuu ujao kama hatatimiza ahadi zake.

Zaidi ya hapo niliambiwa kitu ambacho Lissu amefanya ni kuwakingia kifua wananchi wake wasichangishwe michango mbalimbali kitu ambacho kimechangia halmashauri pia kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake kwa madai kwamba wananchi wake hawachangii kuwezesha kukamilika kwa miradi hiyo. Kilichowaumiza na kuwasikitisha zaidi wananchi wa singida mashariki ni pale Joshua Nassari alipoanza kuchimba visima siku moja tu baada ya kutangazwa mshindi wa jimbo la arumeru mashariki.

Nilisikitika sana baada ya kusikia habari hizo kwa kuwa mimi binafsi namuamini sana Lissu na uwepo wake bungeni una mchango mkubwa sana kwa ustawi wa upinzani na kwa kuiweka serikali katika msitari mnyoofu. Nililazimika kuziamini habari hizo kwa kuwa mtoa habari ni mfuasi wa mageuzi na kwa kuwa na mimi napenda harakati za CDM katika kulikomboa taifa nimeona ni vyema niliweke suala hili jamvini ili wahusika walione na wachukuwe hatua stahiki jimbo lisije likarudi kwa chama cha magamba mwaka 2015.

Najua bado Lissu ana zaidi ya miaka miwili mbele ya kuweza kusimamia ahadi zake kwani ahadi ni deni. Wananchi wanahoji kama chadema walimwambia watamsaidia ajenge visima mbona mpaka leo hawajatimiza ahadi kama walivyofanya Arumeru mashariki? au kwa kuwa singida ni ngome ya CCM? Naomba chadema kama chama wachukuwe hatua kuhakikisha baadhi ya ahadi hizo zinatimizwa ili kulinda hadhi ya chama kuelekea mwaka 2015.

Chadema wakumbuke kwamba singida na kanda ha kati kwa ujumla imekuwa ngome ya CCM kwa miaka mingi hivyo hawapaswi kuchezea bahati waliyoipata huko singida mashariki bali wanatakiwa watumie jimbo hilo kama chachu ya kupata mjimbo mengi zaidi mwaka 2015. Singida mashariki iwe mfano kwa majimbo mengine ya ukanda huo ili wananchi washawishike kuchagua chadema katika uchaguzi ujao. Daima mtu anayekupenda atakwambia ukweli.

Nategemea michango yenye kujenga na sio kejeli wale kubeza, najua wengi tuna mapenzi binafsi na Lissu lakini kwenye ukweli lazima tuuseme kwa manufaa ya upinzani ambao naamini wengi tunaupenda.


Lissu alichaguliwa na wananchi wa singida mashariki lakini ni mbunge wa watanganyika wote, the voice of the voiceless, tunalipa kodi ya nini kama unataka nchi iendeshwe kwa michango, futa kodi halafu tuendeshe nchi kwa michango kama harusi, tunalipa kodi mnaiba halafu mnarudi mnatuambia tuchangie maendeleo ni akili taahira ndo inaweza kununua wazo hili.
 
Huyu chiz anayesema Tindu ajiangalie ,mbona hawaambii magamba waangalie wasije wakahukumiwa kwa kukaa madarakani miaka 50 hata malengo ya Milenia yanaelekea kufeli chini ya uongozi wa sisiem? Na imebaki miaka 3 kufikia 2015!
Usitumike kama wanakutumia mwanaharakati na wakikulazimisha? Waambie noma aiseee!
 
"KUPANGA NI KUCHAGUA" Lissu alipanga na kuahidi uchimbaji wa visima ila amechagua kutotrkeleza ahadi hzo, haya 2015 siyo mbali Wanasingida Mashariki watamhukum kwenye sanduku la kura. UMOJA NI USHINDI
 
Sasa na wananchi wa Singida mashariki wamesema wanampa mh,Lissu miaka 45 ili waone kama atashindwa kujenga visima 12,upo.?by the way,asante kwa kuwakumbusha wapiganaji.
 
Sasa na wananchi wa Singida mashariki wamesema wanampa mh,Lissu miaka 45 ili waone kama atashindwa kujenga visima 12,upo.?by the way,asante kwa kuwakumbusha wapiganaji.
 
Fanya utafiti achana na maneno ya kuambiwa. Tundu Lissu bado anakubalika sana jimboni kwake although bado ana kazi ya kutekeleza ahadi zake.
 
Mnapenapasiana kama mpira wa miguu.

Alikuwa nape na kadi kwa Dr slaa

Akaibuka tena nape kwa JJ Mnyika

Sasa wewe unakuja na Mh Tundu lisu.

Hao wapigakura katika jimbo la Lisu ulikutana nao katika kikao gani cha lini na maazimio ya kikao hicho yalikuwa nini chini ya

mwekiti gani?

anayemlalamikia na kukomalia ahadi awakomalie wizara ya maji wamehaidi nini hawajatekeleza miaka 51 ya uhuru
Lissu visima 12 mishipa inawatoka za ccm zikomalieni ndo wanakusanya kodi kwa serikali yao ye ni kuwashinikiza wangalie sekta za maji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom