Tundu Lissu ana deni kubwa jimboni, achukue tahadhari!

Salamu jf,

Nasikitika kwa mbunge wangu tundu lisu kuamua kulitelekeza jimbo. Mheshimiwa tundu lisu umekua ni mbunge wa kitaifa,umesahau ulipotoka. Tangu uchaguliwe umekuwa hufiki jimboni kuskiliza kero za sisi wananchi wako wa singida mashariki,kwanza unaishi dar na umekua bize sana na kazi zako za uwakili pamoja na kazi za chama.

I declare the interest that mimi ni mwanachadema mkereketwa na wananchi wanalalama sana huku,tafadhali mbunge wangu kumbuka wapiga kura wako. Uzinduzi wa MC4 wa jimbo la kati utakapopita tafadhali apologize kwa wananchi wako. Najua huwa unapita huku sana kwa hiyo ni vyema ukawasikiliza wapiga kura wako.

Naomba kuwasilisha
 
Watu kwa kujivika ukuu!
Yaani mawazo yako unayafanya ndio mawazo ya wana Singida Mashariki wote.

Kama wewe ni mwanachadema, taja namba yako ya uanachama.
 
Ninamheshimu sana mkuu Wild fauna hapa Jamvini na ninaamini hajaleta habari ya kimbeya.

Mkuu Tundu Lissu kazungumze na watu wako watakuelewa tu kutokana na majukumu mengi uliyo nayo ya kitaifa na ya chama chako.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu molemo nia yangu sio kumzodoa mweshimiwa lisu ila nikutaka kumkumbusha asisahau jimbo kiasi hicho. Kwa mie sishangai lisu amavyokuwa bize kwani naelewa jinsi alivyo nguzo imara katika ujenzi wa chama,tatizo ni hawa wananchi ambao wanauelewa mdogo kuhusu utendaji wa mbunge. Above all lisu is my role model katika siasa zetu hapa nchini.
 
Salamu jf,

Nasikitika kwa mbunge wangu tundu lisu kuamua kulitelekeza jimbo. Mheshimiwa tundu lisu umekua ni mbunge wa kitaifa,umesahau ulipotoka. Tangu uchaguliwe umekuwa hufiki jimboni kuskiliza kero za sisi wananchi wako wa singida mashariki,kwanza unaishi dar na umekua bize sana na kazi zako za uwakili pamoja na kazi za chama.

I declare the interest that mimi ni mwanachadema mkereketwa na wananchi wanalalama sana huku,tafadhali mbunge wangu kumbuka wapiga kura wako. Uzinduzi wa MC4 wa jimbo la kati utakapopita tafadhali apologize kwa wananchi wako. Najua huwa unapita huku sana kwa hiyo ni vyema ukawasikiliza wapiga kura wako.

Naomba kuwasilisha
NAONA HAPA UMEAMUA KULETA UMBEYA TU KWANI HATA KIPOFU HATA KAMA HAONI ILA HUWA ANASIKIA MAMBO AMBAYO RISU ANAYAFANYA JIMBONI KWAKE. rudi kwa aliyekutuma.
 
Namfahamu Lissu, najua kazi aliyofanya kwa ajili ya watu wa Jimbo lake. Najua tangu achaguliwe amejitahidi kufanya mikutano zaidi ya Mitatu kila Kijiji tangu awe mbunge, Lissu anafika Jimboni kwake kwa wananchi kwa kiasi Kikubwa kuliko wabunge wote wa Mkoa wa Singida, anafanya mikutano sio Jimboni kwake tu hata Majimbo mengine. Kuhusu Kukaa Dar es Salaam, ni sawa lakini sio kwa starehe, Yeye ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani, muda mwingi anahitajika kwa shughuli za Kambi ya Upinzani, kwa shughuli za Waziri Kivuli wa Sheria kuandaa hoja nzito zilizosaidia Watanzania. Mleta hoja ulipaswa kuulizwa kama kweli unatetea watu wa Singida, anzisha hoja ya kuuliza Mbunge wa Singida Mjini amechangia mara ngapi bungeni, kuna mijadala ya Katiba ametoa wapi mchango wake, Lissu alishiriki hata kutoa maoni ya katiba Jimboni, na Bungeni kafanya. Mwishoni mwa mwaka jana alikamatwa na polisi na kuzuiliwa kufanya mikutano Jimboni, je ilikuwa wapi hiyo? Anajitahidi kufika Singida hata kusaidia watu wake wanaoshtakiwa kwa kesi, amebaki kuwa ni mbunge pekee ambaye watu wa Singida tunajivunia, tena sio Singida tu hata Kanda ya Kati nzima. Lissu alizuia michango ya sekondari kwa wananchi wake, serikali ikasema itaacha kujenga shule katika Jimbo lake, lakini imeendelea kuzijenga, Nimeheshimu Katiba kwa kuwa ni Uhuru wa maoni, basi umejitahidi, angalau unajua kusoma na kuandika ila waalimu hawakutosha Shuleni.
 
Lissu nenda Singida watumikie wananchi waliokupigia kura.
 
Mkuu Lissu kazi anayofanya ni kubwa sana we mwenyewe unaona alivyokuwa bungeni,usijali hawezi akawasahau ila na nye jitumeni
Kazi yake ni kutumikia walio mchagua awawakilishe,sasa kama anakazi zingine kwanini alikimbilia ubunge?
 
wanachadema wenzangu taarifa kama hizi si za kupuuza hasa katika hiki kipindi kigumu,hivyo ni muhimu kwa watu walio karibu na tundu lissu kumueleza haya na kama ni kweli ni kuyafanyia kazi! 2015 hatutakiwi kuacha jimbo jamani!
 
halafu nyie watu wengine mmpagawa mbona jamaa anafanya kazi sana hayo ni mawazo ya kilofa ya kumuambia kuwa jimbo kaliweka rehani! ndio ni mbunge wenu lkn na sisi kama taifa tunahitaji mchango wake. mwacheni afanye kazi. akipata wasaa atakuja tu. namuamini sana lisu.
 
Mkuu Lissu kazi anayofanya ni kubwa sana we mwenyewe unaona alivyokuwa bungeni,usijali hawezi akawasahau ila na nye jitumeni
Hawawezi kujitume. Wanajituma vipi wkt mwenyewe Lissu amewakataza kuchangia na kushiriki shughuli za maendeleo! Ndio maana wamebweteka wanamsubiri ili awapelekee ugali na ikibidi awafagilie nyumba na viwanja vyao, Pamoja na kuwatandikia vitanda vyao.
 
kwa hiyo wajibu wa hao wananchi ni nini?je kama we ndo mojawapo unataka upelekewe ugali,ufagiliwe nyuma pamoja na uwanja na kutandikiwa kitanda?
 
kwa hiyo wajibu wa hao wananchi ni nini?je kama we ndo mojawapo unataka upelekewe ugali,ufagiliwe nyuma pamoja na uwanja na kutandikiwa kitanda?

Usikatae kaka, mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, ndio maana wanamshangaa kwa nini haendi. Kinyume chake wange-appritiate kazi kubwa anayofanya huku mjini!:violin:
 
Tundu Lissu achukue tahadhari kubwa na aanze kuzifanyia kazi ahadi zake kwa wananchi. Bahati mbaya kwa sasa wabunge wanageuzwa serikali/afisa miradi, na kama aliahidi basi ni vema afanye hivyo maana wabaya wake ni wengi mno na wanata kumtoa bungeni.

Umenena na lafaa kuzingatiwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom