Tundu Lissu amjibu Zitto kuhusu tuhuma za LEAT

zitto hajawahi kushindwa kutetea na kulinda credibility yake
zitto huwa hakurupuki huwa anaongea kwa fact na anajiamini
zitto huwa haibui hoja ambayo anajua hajui mwisho wake nasubir ze return of super men zitto muyangwa kabwe huyu vuvuzela atazima zake
Kazurure tu wewe mzururaji... Naona lissu humjui ww
 
Wewe kazi unayoiweza kwa sasa ni kumpigia shoeshine Dr Mihogo that's it.

Stress zinakusumbuwa, sijui Dr Mihogo aliwaahidi nini masikini?

Mkuu..
Huyu idaya alivurugwa pale aliposkia Dr.Mihogo kalazwa nje na kimada..
Baada ya kua Archtect wa kumpokea Muheshimiwa Lowassa..
 
Sidhani usemacho kwa Zito.mlimchukia bule pale cdm walipomtoa kwa madai ya kusema anashilikiana na upande mwingine ila nachoona ni walimuogopa tu coz yule jamaa ni akili kubwa na ametoka Kigoma,wangekua nae mpaka leo kama angekua katokea Kilimanjaro
Elimu elimu elimu,,,viva lowasa,,ona izi pumba anazoandika huyu mtu mzima ambae anafamilia,,,is just bcoz of elimu elimu elimu,,,,,sasa tuambie tundu lisu ni mtu wa Kilimanjaro?? Profesa safari ni mtu wa Kilimanjaro?? Salum mwalimu,mchungaji msigwa, wote hao bado wapo cdm,,,kuna vtu unaweza kucoment hata Mtoto wako akiona anaweza asikuamkie kwa kukudharau,
 
Nikikumbuka 2014 Lisu alivyokuwa anakuja na mafaili yenye ushahidi kuwa Lowasa ni fisadi,

Alafu 2016 Lisu huyo huyo ni mbeba note book za Lowasa !!!

Tangia hapo mimi na watanzania wenye akili Kila kitokacho mdomoni mwa Lisu huwa hakiaminiki tena
Hujui siasà kaa kmya
 
Anaandika Lissu,

Fedha gani za Mzungu nilizopigia kampeni mwaka 2015?

Fedha zote nilizotumia kwenye uchaguzi wa mwaka jana zilitokana na malipo ya kiinua mgongo tulizolipwa wabunge wote.

Niliondoka LEAT mwezi February 2009, zaidi ya mwaka na nusu kabla sijawa mbunge.

Kazi ya ushauri wa kisheria niliyoifanya kati ya mwaka 2007 na '09 haikuhusu wananchi wa vijiji vitano vya Bagamoyo kunyang'anywa ardhi zao.

Ilihusu kampuni ya SEKAB Bio-Energy kupewa hekta 22,000 za Shamba la RAZABA (Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo) ambalo Serikali ya Mwalimu Nyerere iliipatia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika miaka ya '60 kwa ajili ya ufugaji ng'ombe.

SEKAB Bio-Energy walipewa shamba hilo kufuatia makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2007.

Barua ya Wazungu hao kupewa shamba hilo iliandikwa na Dkt. Jumanne Ngasongwa, wakati huo Waziri wa Uchumi, Mipango na Uwezeshaji.

Mimi nilipewa kazi ya ushauri wa kisheria juu ya taratibu za utathmini wa shamba hilo kwa ajili ya ulipaji fidia na masuala yanayohusiana nayo.

Kwa kuwa mimi sio wakili magumashi, nyaraka zote nilizoziandaa kwa ajili hiyo ninazo na nimezipitia tena baada ya maCCM wa humu ndani na/au mawakala wao kuleta uzushi huu.

Hakuna hata moja inayohusu mwanakijiji hata mmoja kunyang'anywa ardhi yake. And believe you me, I was paid handsomely for my legal advice.

Mimi ninajulikana kimataifa kwa kupigania haki za ardhi za wanavijiji katika nchi hii zilizoporwa kwa mabavu na maCCM na kukabidhiwa wawekezaji wa nje.

Whether ni Rufiji Delta au kwenye hifadhi za taifa za Umasaini au kwenye Goldfields za Kanda ya Ziwa, nimetetea wananchi dhidi ya makampuni ya kigeni na mawakala wao wa Serikali za maCCM.

Nimeifanya kazi hiyo tangu ujana wangu. I'm proud to say I've fought tirelessly and consistently for my people.
Eti unajulikana kimataifa kupigania haji za wanavijiji that's a joke
 
Zitto Vs Tundu Lissu,
Naamini Lissu ni zaidi.
of course tobo ni zaidi kwa hoja za kijinga kama vile ''Rais Magufuli'' wakati Zitto yupo bize kuhoji mambo yanayohusu mstakabali wa taifa kama vile IPTL, EsCROW, Ubuzwagi na mengine kama hayo.
 
Kumjibu zitto ni kupoteza muda,Zitto anafanya kazi ya watawala,kazi yake ni kuwatoa wapinzani kwenye reli hasa pale watawala wanapokuwa wamebanwa,ajue tu kuwa wapinzani wa leo hawapunguzwi kasi kijinga kiasi hicho,Lissu is our time hero.
UKUTA lini? au mmeufyata?
 
Kumjibu zitto ni kupoteza muda,Zitto anafanya kazi ya watawala,kazi yake ni kuwatoa wapinzani kwenye reli hasa pale watawala wanapokuwa wamebanwa,ajue tu kuwa wapinzani wa leo hawapunguzwi kasi kijinga kiasi hicho,Lissu is our time hero.
Umetoka povu!Kila mwenye ovu anatakiwa kuambiwa bila kujali chama anachotokea
 
Katika maelezo yake hajakanusha kama kweli wananchi hawakupoteza ardhi yao.
Mwanasheria wa mwendokasi.. zee la kubwabwanja halina hoja

..TL amekanusha.

..ngoja nikufafanulie kilichotokea.

..miaka ya 80 serikali ya Tanganyika iliipa ardhi serikali ya Zanzibar kwa ajili ya kuanzisha ranchi.

..Serikali ya Znz ilishindwa kutekeleza mradi huo hivyo ukafa.

..miaka ya 2000 ndiyo wamekuja wawekezaji toka Sweden na kununua ranchi hiyo.

..TL ndiye aliyekuwa mshauri wa kisheria wa mwekezaji ktk suala hilo la ardhi.

..kisheria ardhi ilikuwa inamilikiwa na serikali ya Zanzibar kwa hiyo hakukuwa na uwezekano wa wananchi wa kawaida "kuporwa" ardhi yao kama anavyodai Zitto Kabwe.
 
Back
Top Bottom