Suluhisho za changamoto zilizopo kwenye muungano Tanzania

greater than

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,281
2,191
Awali ya yote natumaini wananchi wenzangu wote mpo salama.

Ndani ya kipindi hiki cha miezi miwili kumeibuka mjadala mkali ukihusu changamoto za muungano kutoka pande zote mbili za muungano. Mda mwingi umetumika kujadili changamoto kuliko kuweka mawazo ambayo yatatatua changamoto hizo.

Uzi huu ni maalum kwa ajili ya kupendekeza suluhu ya changamoto zilizopo.

Nami ntaanza kwa kupendekeza mambo kadhaa yenye kuleta suluhu.

1.UTAMBUZI WA TANGANYIKA
  • Nchi ya Tanganyika itambulike na kutamkwa kwenye katiba, na uwepo wake uishie kwenye masuala yasiyo ya muungano
2.UONGOZI WA TANGANYIKA
  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiyo atakayesimamia masuala ya Tanganyika
  • Cheo cha makam wa Rais wa Jamhuri kitashikwa na Mtanganyika tu.
  • Nafasi zote za mawaziri katika wizara za mambo yasiyo ya muungano zishikwe na Watanganyika tu.
3. BUNGE
  • Bunge la Jamhuri ndiyo litakuwa bunge linaloamua mambo ya Tanganyika
  • Idadi ya Bunge ya Zanzibar ibaki hivyo hivyo
  • Kwenye mijadala ya mambo yasiyo ya muungano ,wabunge wa Zanzibar wataruhusiwa kuchangia tu.
  • Wabunge kutoka Zanzibar hawataruhusiwa kupiga kura kwenye mambo ambayo si ya muungano.
3.UMIRIKI WA ARDHI
  • Kutakuwa na ardhi ya Jamhuri na Ardhi ya Tanganyika na Zanzibar
  • Ardhi yote ambayo kuna Majengo ya Serikali ya Jamhuri, itakuwa ni ardhi ya Jamhuri
  • Ardhi yote yenye miundombinu ya mambo ya muungano,itakuwa ardhi ya Jamhuri....mf.Kambi za kesho,vyuo vikuu,vituo vya polisi,Mbuga za Taifa
  • Kila nchi itatenga 25% ya eneo la ardhi yake kwa ajili ya Jamhuri,utumizi wa wananchi wa pande zote mbili.
  • Nje ya 25 % kwa Bara,Mzanzibar hatoruhusiwa kumiliki eneo
  • Nje ya 25% kwa Zanzibar,Mtanganyika hatoruhusiwa kumiliki eneo.
4.URAIA
  • Uraia wa kwanza wenye nguvu ni wa utanzania
  • Uraia wa Zanzibar na Tanganyika utasaidia kwenye masuala yasiyo ya muungano tu.
  • Mtu hatohitaji kitambulisho cha aina yoyote kwenda kokote nchini, iwe Zanzibar au Tanganyika.
 
Mimi siyo muumin wa serikali tatu, ila naamini ndani ya serikali ya Jamhuri, kunaweza wekwa taratibu maalum ya kushughulukia masuala ya bara.
 
Namba 3: Bunge la Tanganyika haliwezi kuepukika kama tutatambua uwepo wa Tanganyika na kuirejeshea mamlaka yake. Bunge la Tanganyika litakuwa Dodoma, wakati Bunge la muungano napendekeza liwe Dar es salaam.

Ingependeza zaidi kama muungano huu tata tungeuvunja rasmi na kuzirudishia Tanganyika na Zanzibar mamlaka yake, kisha tuingie kwenye Fédération ya East Africa kila nchi kivyake.
 
Back
Top Bottom