~*~ Tunawaudhi ~*~

tic tac ! tic tac ! tupo pamoja mkuu ! enough said ! Mheshimiwa Rais bado anaendelea kuchapa kazi, wao wanataka walete propaganda zao hapa na kutaka JK asifanye kazi, lakini wapi !

ccm tutatawala hadi kiama. wapinzani wale nyembe kama wana hasira.
 
Ndiyo Tunawaudhi!!

Wanakaa chini na kujiuliza kwanini tunawafuata fuata! Wanakereka tunapoandika na kuwajadili na wanaona tunawaandama pasipo sababu ya msingi. Wanachukia na wangekuwa na uwezo wangesha tubamiza kama mtu anavyobamiza nzi ukutani!

Tumekuwa kwao kero isiyokoma, wasumbufu waliotumwa, na watu wenye wivu na maendeleo "yao". Wanakasirika na kununa, wanachukia na kuchukizwa! Tukipita wanatema mate pembeni, na tukiwasalimia hadharani wananyosha mkono kibahili! Wameudhika!!

Tumewaudhi kwa sababu suala la EPA lilitakiwa limalizwe kimya kimya, na sakata la Richmond lilikuwa limeshatolewa "maelezo". Tumewaudhi kwa sababu suala la Kiwira linamhusu "Rais Mstaafu" ambaye tuliambiewa tumuache "mzee wetu astaafu kwa amani". Wameudhika, na tena wamekereka.

Tumewaudhi kwa sababu tumeenndelea kuwahoji hata baada ya kuambiwa mtu kafa; Na tunaendelea kuwaudhi kwa sababu inaonekana tumekuwa watukutu tusiosikia, hatuelewi majibu yao na zaidi ya yote tumekuwa kama luba tumewang'ang'ania kwenye miguu yao ikimbiliayo maovu na ifanyayo haraka kuharibu!

Ndugu zangu, tumewaudhi na tunaendelea kuwakera; wakikaa ofisini kusaini mikataba mipya wanafikiria mara mbili sasa; wakitangaza tenda wanaulizana kama kuna maslahi binafsi yaliyofichwa; Wamebaki wenyewe kushukiana na kuhisiana ubaya na sasa wanazungukana kama watoto wanaocheza "kioo kioo"! Ajulikani nani hasa kakivunja! Wamebakia kuulizana huku wengine wamejificha "tiari bado"?!

Ndio wanakerwa na uwepo wetu, wanachukizwa na uthubutu wetu, wangelikuwa na uwezo kama wa paka kumrukia panya wangedaka mawazo yetu, kuyararua na kuyaweka kiporo ili wayachezee kesho yake! Wangekuwa na uwezo wangetukwapua kama kinyonga akwapuavyo vipepeo na kutubamiza kwenye ndimi zao za moto, na kufumba vinywa vyao kwa ghafla kama mamba wafanyavyo pembezoni mwa Rufiji!

Wanajiuliza kwanini tunawafuatafuata, kwanini hatuwaachi wafanye "kazi", kwanini tunafuatilia matendo na maneno yao wakati wao ndio "viongozi"? Wanashangaa kwanini wakisema mambo ya "vijisenti" kauli zao zinakuzwa kama kwa baragumu! Hawaelewi, wamebakia kuchukizwa na kukerwa!

Ndiposa, sisi sote tunaitwa kufanya uamuzi; aidha kusalimu amri na kuwaacha wapumue kidogo? au kukaza uzi ule ule. Tuna uamuzi wa kukubali maelezo yao ya juu juu au kuendelea kuwachimba kwa maswali ya ziada; tuna uamuzi wa aidha kuwaonea huruma kwa sababu familia zao na jamaa zao wamefadhaishwa na kufedheheshwa au kuendelea kwa sababu kwa maamuzi yao wametufadhaisha na kutufedhehesha sisi kama taifa! Tukubali majibu yao ya awali na turidhike?

Tunaitwa kufanya uamuzi; kujipanga mstari na kupiga makofi na kuwaimbia nyimbo za shangwe au kukaa kimya na kusubiri tuone wanachofanya nini ili tuamue sawasawa. Tunaitwa kufanya uamuzi wa kukubali kutawaliwa nao jinsi wapendavyo, au kuwalazimisha kutambua tunavyopenda kutawaliwa nao! Yes! Tunaoumauzi pia wa hata kuamua kama tunataka waendelee kututawala tena au hii ndiyo iwe ngwe ya mwisho kwao!

Kama wewe ni Mtanzania na mzalendo wa kweli, bila kujali hali yako ya maisha, elimu yako au nafasi yako ya kisiasa na kijamii, bila kujali kama wewe ni mfurukutwa au mkeretwa, bila kujali kama unafuata mrengo wa kulia au wa kushoto au kama itikadi yako ni ya kijamaa au ya kibepari; kama kweli una mapenzi na taifa lako, kama kweli unataka Tanzania ije kusimama kama Taifa la watu walio huru kweli na sawa; Taifa ambalo ndani yake kila mmoja ana nafasi sawa ya kufanikiwa; Taifa ambalo ndani yake wana na mabinti wake wanaona fahari kulitumikia na siyo kulitumia, kuliendeleza na sio kulitelekeza, kuliinua na siyo kulifumua! Taifa la kisasa, Taifa la Kiafrika, na Taifa ambalo kwa mafanikio na fahari litasimama katika jamii ya Mataifa ya ulimwengu!

Basi tunaitwa kufanya uamuzi, na uamuzi huo kwa hakika utakuwa ni wa kuwaudhi na kuwakera watu fulani fulani. Je uko tayari kuwaudhi mafisadi? Je uko tayari kuwakera waliokwiba fedha za Taifa letu? Je uko tayari kuwasumbua usiku kucha waliobaka raslimali za Taifa letu huku wanatuchekelea na kujilamba vinywa vyao huku wakipangusa ala zao?

Najua mimi niko tayari! sijui wewe.. lakini huko tunakokwenda, ni wale walio tayari kusimama peke yao na pweke ndio wataliinua Taifa letu na kulifanya liwe jinsi ile tulitamanivyo liwe! Stand up and be counted otherwise sit down and be forgotten!

Naona leo wameudhika hadi wamekuja kujaza forum hapa lakini huu watashindwa tu.
 
Kuudhika? njaa na wivu tu unawasumbua,

wewe ulidhani kuwa wana chadema ndio pekee mtajazana hapa na kuishambulia ccm kila siku? sasa tumejipanga na karibuni mtapotea kabisaa hapa na hamtaonekana.

Tuliwaachia mkaanza kupanda vichwa sasa.
 
Mkjj, Ahsante sana kwa article hii nzuri sana. Nakuomba uisambaze hii article katika magazeti yote ya Kiswahili ya Tanzania kama vile Tanzania Daima, Raia Mwema, Mwananchi, Mwanahalisi na mengine ambayo yatakuwa tayari kuiweka article hii katika magazeti yao ili Watanzania wengine nao wapate nafasi ya kuisoma.

Mimi niko tayari kupambana katika vita hii ili kuhakikisha tunawatokomeza mafisadi kwa maslahi yetu na yavizazi vyetu vijavyo. Tukifanikiwa kuwashinda mafisadi basi kutakuwa hakuna kipingamizi cha kuhakikisha utajiri wetu mkubwa tulionao unatumika kwa maslahi ya Watanzania wote ukilinganisha na sasa ambapo utajiri huo unawanufaisha mafisadi wachache ambao hawafikii hata 1,000 katika nchi ya watu 40 millioni

Kwa mara nyingine tena, ahsante sana.
 
wana chadema hadi mnatia huruma saaasa. speech ndefu na hakuna kitu. Ccm imekuja kufight back.
 
kwi kwi kwi,

huyu kweli ni bi saddam husein.
Mkuu umewakomesha hadi wametokomea kabisa?

tutammwagia maua, na kumuwekea kapeti jekundu si unajua ili bi. saddam afurahi maana saddam mwenyewe akikasrika, tumekwisha !
 
Kuudhika? njaa na wivu tu unawasumbua,

wewe ulidhani kuwa wana chadema ndio pekee mtajazana hapa na kuishambulia ccm kila siku? sasa tumejipanga na karibuni mtapotea kabisaa hapa na hamtaonekana.

Tuliwaachia mkaanza kupanda vichwa sasa.

sifa zilizidi propaganda ! now they get to taste some of what they were doing !
 
na mulicholeta ni kipi zaidi ya pumba tu na ufisadi?

maskini weee !! dreva wa saddam huyooooo.............kamlete basi na bi. saddam ! tutawamwagia maua, na kuwaimbia nyimbo nzuri ili saddam afurahi ! bila ya kusahau makofi !
 
Swali ni kuwa Tanzania hii tutaiinua kivipi ilihali mfumo uliopo umeoza. Na uoga umezigubika nyoyo za watu kiasi kwamba hata imani zao zimeathirika. Mzee Mwanakijiji aweza kuwa tayari je na wengine? Tupo ambao tunafurahi kutoa post zetu au thread lakini ule utayari ni mdogo hatuko kama wenzetu wakenya tumebaki kulaumiana na kunyoosheana vidole. ADA YA MJA HUNENA MUUNGWANA NI KITENDO
 
Mkuu Kada mchukia maendeleo

Hivi ni lazima kila thread uchangie? Hivi kwanini wakati mwingine usikae kimya?
 
Kada mpinzani ! unanikumbusha hadithi moja ya zamani sana kuwa kila mtu anatabia yake ya kuzaliwa/kurithi nk mathalani hata ukimchumkua mtoto wa haranu ukamficha katika chupa atajitahidi tu angalau atoe kidole juu ili tu aonekane kuwa yeye ni mwana haram!
 
Na bado wataudhika mpaka wajigundue kuwa wapo uchi ili wavae nguo
 
Wamenona sana hawa kama wale wapiganaji wa Sumo, hivyo kutembea msamba wazi na tumbo wazi ni Ruksa! hakuna nguo zitakazo watosha. Watadai zitengenezwe kwa nyuzi za dhahabu na almasi!

Hawajioni wako uchi, hawana haya au soni, wameshazoea wanataka nasi tuzoee...
 
Unanikumbusha story ya VAZI la MFALME....

Itabidi watafutwe washonaji kutoka ng'ambo ya mbali kuwa kuwaandalia mavazi yao ya ajabu...

Na akili zao nahisi hazijasetiriwa
 
Ningekuwa Mtawala ningependa upinzani wenye nguvu....nisingeponda upinzani.....
Sababu nia yangu ya kwanza isingekua ni kutawala tu, nia ya kwanza ingekua kuwapatia watz kilicho bora...na upinzani unavyozidi kuwa na nguvu ingenisaidia kuondoa uzembe, jeuri na dharau katika mfumo wangu wa utawala.....kisha watz wangepata wanachostahili....
Ningekuwa mtawala ningesaidia upinzani kupata nguvu zaidi.... Yes! Upinzani wenye nguvu ni faraja kwa watz!
 
sijakebehi, ila ninachosema ni kwamba, yooote aliyogusia HAMNA JIPYA, na kama unaandika kitu basi lazima uwe AIM ya kuandika, hadi hivi sasa sijaona chochote kipya, na kama solutions nadhani zilishatolewa before katika threads husika !

asante !

kama wewe ni muislam huwa unakwenda msikitini kufanya nini wakati Quran imeandikwa zaidi ya miaka 1500 iliyopita kuna jipya kwenye Quran? Na kama wewe ni Mkristo huwa unakwenda Kanisani kufanya nini wakati yesu alishapaa kwenda mbinguni zaidi ya miaka 2000 iliyopita, lipi jipya unalolifuata au kulitafuta kanisani? Tuache unafiki kila maslahi ya mafisadi yanapoguswa kwa kujifanya hakuna "jipya!
 
Swali ni kuwa Tanzania hii tutaiinua kivipi ilihali mfumo uliopo umeoza. Na uoga umezigubika nyoyo za watu kiasi kwamba hata imani zao zimeathirika. Mzee Mwanakijiji aweza kuwa tayari je na wengine? Tupo ambao tunafurahi kutoa post zetu au thread lakini ule utayari ni mdogo hatuko kama wenzetu wakenya tumebaki kulaumiana na kunyoosheana vidole. ADA YA MJA HUNENA MUUNGWANA NI KITENDO

unajua mkuu umeongea point tupu ! Lakini kwa kuwa wengi humu hawataki kuangalia au kukubali points zinazoongelewa, wanashindwa hata kukusupport na unachosema, lakini wengi wanachojua ni kada akipakwa basi wanakimbilia kutoa thanks na unafiki wao utadhani kama hiyo itasaidia kujenga tanzania !

anyway usikate jamaa ndio jf hiyo !
 
Back
Top Bottom