Tunaukaribisha uchunguzi kwa Zitto Kabwe

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
TAARIFA KWA UMMA

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeshtushwa na tuhuma, kashfa, porojo na matusi mbalimbali yaliyotolewa jana na msemaji wa chama cha Mapinduzi(CCM), Ndugu Christopher Ole Sendeka dhidi ya Kiongozi wa chama chetu, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto.

Kutokana na hayo chama kina masuala yafuatayo ya kusema kwa wanachama wetu na umma wa Watanzania kwa ujumla:

• Chama chetu kinakaribisha uchunguzi juu ya mali na madeni ya Kiongozi wetu, ndugu Zitto. Tutafurahi uchunguzi huo ukihusisha akaunti zake za benki pamoja na mfumo wa maisha yake binafsi (Life Style).

Tunavitaka vyombo vya uchunguzi vianze kazi hiyo mara moja kwani tunaamini kuwa Kama kuna Kiongozi ambaye Mali, Madeni, Maslahi na Akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto.

Ikumbukwe kuwa Katiba na Kanuni za chama chetu huwataka Viongozi wote wa chama kuweka hadharani tamko la mali zao na madeni, ndugu Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria, na mali pamoja na madeni yake yako hadharani na mtandaoni. Tunatambua chama tawala kinaweweseka na tunataka kiondokane na ugonjwa huo wa kuweweseka,badala yake wachukue hatua za uchunguzi dhidi ya ndugu Zitto.

• ACT Wazalendo tunayo taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG. Kupitia taarifa husika CAG ametoa Hati safi Kwa Shirika la NSSF Kwa hesabu za mwaka 2014/15. Hajaona ufisadi wowote ule.

Sijui msemaji wa CCM anatumia taarifa ipi ya CAG kusema kuwa NSSF ilinunua Ardhi Kwa bei ya Shilingi Milioni 800 aliyomhusisha nayo Kiongozi wetu.

Kwa mujibu wa barua ya CAG Kwa Uongozi wa NSSF (Management letter), Shirika hilo halijanunua ardhi yoyote Kigamboni, bali Shirika limeingia ubia wa Ardhi Kwa Hisa (Land for Equity).

Hivyo ni vizuri mbwatukaji huyo wa Chama tawala akaeleza kwa undani Ufisadi anaousema juu ya manunuzi ya ardhi kwa kunukuu ripoti ya CAG kaitoa ukurasa namba ngapi katika ripoti husika.
Labda chama chake kina taarifa nyengine ya CAG tofauti na iliyowasilishwa kwenye Kamati ya PAC.

Rais Magufuli, ambaye ni Mwenyekiti wa chama tawala, amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kuwa Balozi. Kauli za Msemaji wa chama tawala alizozitoa jana zikiaminiwa zina maana kuwa Rais na Mwenyekiti wa chama chake anateua mafisadi kuwa mabalozi. Ni vizuri nyie wanahabari muulize juu ya hili jambo.

• Ni wajibu wa Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo kuupinga ujinga popote pale ulipo, Kiongozi wa Chama chetu, ndugu Zitto, anatekeleza wajibu huo kwa Uzalendo mkubwa kwa Taifa lake.

Chama chetu kiko pamoja naye katika kupinga Ufisadi mkubwa wa ESCROW ambao chama tawala kimeukalia kimya, ufisadi wa Mabilioni ya HATI FUNGANI na hata sasa anapowapigania Waandishi wa Habari nchini katika Kampeni yake ya kupinga MSWADA MBAYA wa Habari.

Tunajua kuwa kampeni hii ya kupinga Mswada mbaya wa Habari ndiyo ambayo imezua ubwatukaji huu wa msemaji wa chama tawala.
Ni muhimu Serikali na chama tawala wajue kuwa chama chetu kitaupinga mswada huo ambao utakwenda kuua tasnia ya habari nchini mpaka pale utakaporekebishwa. Porojo, kashfa na matusi havitaturudisha nyuma, tutaisimamia hoja hii mpaka mwisho.

• Tunamtaka msemaji wa chama tawala aache porojo, kashfa, vijembe na matusi. Ni muhimu ajikite katika kukishauri chama chake kutekeleza ahadi zake kwa wananchi. Sasa ni mwaka mmoja tangu wachaguliwe, lakini hakuna madawa hospitalini, hakuna mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, hakuna ajira mpya, hakuna kupanda mishahara kwa watumishi wa umma, hakuna hata jiwe la msingi la Kiwanda kipya lililowekwa tokea Serikali ya awamu ya tano iapishwe, mzigo imepungua bandarini, magari makubwa ya mizigo yameamuriwa yapaki tu kwa kuwa sekta ya Usafirishaji imeuliwa, na maisha ya Watanzania yamezidi kuwa magumu.

Hayo ndiyo mambo ya msingi ya Watanzania, chama chetu kitaendelea kuisimamia serikali katika mambo hayo Bungeni kama anavyofanya mbunge na Kiongozi wetu wa Chama.
Mwisho kabisa, tunapenda kujua kama haya aliyoyasema Ole Sendeka ndiyo msimamo rasmi wa Chama chake au ni maneno yake mwenyewe,maana kama ni msimamo wa chama chake,tutakuwa na mengine ya kusema.

"Taifa Kwanza, Leo na Kesho"

Habibu Mchange
Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa
ACT Wazalendo

Oktoba 29, 2016
 
Aliyetuhumiwa ni Zito au chama cha ACT? Nafikiri hayo ni person issues
 
clip_image002.gif

Attachments

  • 20161029_113746.mp4
    3.4 MB · Views: 53
Dr. Ramadhani Kitwana Dau alikuwa ni zaidi ya Director General wa NSSF, haiwezekani Vyama vya Siasa hasa Chama Tawala kupambana na Vyama vya Upinzani kwa kutumia Jina la Daktari huyo, haijawahi kutokea na haitotokea, Siku Moja kabla ya Ijumaa kuu ya 2016 Vyombo vya habari vikiongozwa na IPP media vilishinda Mahakamni kumsubiri Dr.

Magazeti ya Udaku nayo kutwa kucha habari za Dr

Mitandao ya Kijamii kutwa kuchwa ni habari za Dr
Naweza kuthubutu kusema Dr Dau ni Maarufu kuliko hata baadhi ya Mawaziri na Wakuu wa Taasisi kadhaa za Umma na Binafsi na cha ajabu zaid ukikutana na Dr Dau Mwenyewe ni Mtu Simple sana ambae unaweza hata usimtambue Kama ni msomi wa hadhi ya Phd I.e hajikwezi kabisa japo pia huwa Hana kawaida ya kujipendekeza au kumuogopa Mtu yoyote na popote.
 
Aliyetuhumiwa ni Zito au chama cha ACT? Nafikiri hayo ni person issues
Haiwezi kuwa personal kwa sababu tuhuma dhidi yake zinatokana na nafasi yake kama Mwenyekiti wa PAC; kwamba alitumia nafasi hiyo kukingia kifua mafisadi! Kwahiyo ni tuhuma zinazotokana na nafasi yake kisiasa kwahiyo haiwezi kuwa personal!!!
 
Rais Magufuli kamteua Kuwa Balozi huyo mnaemtuhumu Zitto alimkingia Kifua!
 
Mlimuandikia barua na kupost, kumpelekea pia au ni mmekuja hapa kutafuta kiki tu?
 
ni vizuri sendeka amejibiwa mapema. swali la msingi kwa ACT. je zitto ni act na act ni zitto? kwa mtazamo wangu mchange katumia vibaya mamlaka yake kama msemaji wa chama..
 
Mbona Lowasa kamsema Magufuli, Lowasa kajibiwa na Ole Sendeka badala ya Magufuli Mwenyewe?
 
Dr. Ramadhani Kitwana Dau alikuwa ni zaidi ya Director General wa NSSF, haiwezekani Vyama vya Siasa hasa Chama Tawala kupambana na Vyama vya Upinzani kwa kutumia Jina la Daktari huyo, haijawahi kutokea na haitotokea, Siku Moja kabla ya Ijumaa kuu ya 2016 Vyombo vya habari vikiongozwa na IPP media vilishinda Mahakamni kumsubiri Dr.

Magazeti ya Udaku nayo kutwa kucha habari za Dr

Mitandao ya Kijamii kutwa kuchwa ni habari za Dr
Naweza kuthubutu kusema Dr Dau ni Maarufu kuliko hata baadhi ya Mawaziri na Wakuu wa Taasisi kadhaa za Umma na Binafsi na cha ajabu zaid ukikutana na Dr Dau Mwenyewe ni Mtu Simple sana ambae unaweza hata usimtambue Kama ni msomi wa hadhi ya Phd I.e hajikwezi kabisa japo pia huwa Hana kawaida ya kujipendekeza au kumuogopa Mtu yoyote na popote.
hahahaha tatizo sio dau tatizo dini yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom