Tunatafuta mawakala wa kusambaza crank box toka pande zote za nchi

futikamba

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
243
13
Habari JF,

Napenda kuwajulisha kwamba tunatafuta mawakala kutoka pande zote za nchi kwa ajili ya kusambaza crank box.




Crank Box ni jenereta ndogo ya mkono isiyotumia betri, mafuta ya taa/dizeli/petroli wala umeme wa jua/tanesco. Inatumia nishati yako (human power) kutengeneza umeme unaoweza kuwasha taa aina ya LED 3 kwa kuzungusha kwa muda wa dk 1 tu kisha kupata mwanga kwa:-
  • Saa 1 kama taa 3 zimeunganishwa
  • Saa 1.5 kama taa 2 zimeunganishwa &
  • Saa 2 kama taa 1 imeunganishwa.
Faida zake ni:-
  1. Haina kabisa gharama za matumizi
  2. Ni ndogo & inabebeka
  3. Ni rafiki mzuri wa mazingira
  4. Waranti ya mwaka mmoja
  5. Tegemeo la maisha ni zaidi ya miaka 10
Matumizi yake:-
  1. Shuleni kwa kujisomea
  2. Nyumbani kwa shunguhli ndogo ndogo
  3. Kambini
  4. Zahanati zisizokuwa na umeme.
Kwa sasa tuna promosheni itakayoisha tar 30-Nov-2010. Bei ya promosheni ni TZS 15,000/= wakati bei ya halali ni TZS 35,000/=. Je si punguzo kubwa hilo!
Tunawakaribisha wote wenye nia ya biashara na sisi.

Tupo Mbezi Beach - Samaki karibia na hoteli ya Gates of Paradise.
Unaweza kuwasiliana nasi pia kupitia 0715 997688/ 0785 997688.



keyholders.JPG
CRANK BOX KWA MWANGA BORA NA WA KUDUMU...
 
hizo taa tatu zinaweza kuwekwa kwenye vyumba tofauti tofauti? yani kila taa na chumba chake?? je mwanga wake unatosha kuweka kama taa ya nje?? halafu baada ya hiyo dakika moja naweza kuchaji tena ikaendelea kupiga mzigo??
 
hizo taa tatu zinaweza kuwekwa kwenye vyumba tofauti tofauti? yani kila taa na chumba chake?? je mwanga wake unatosha kuweka kama taa ya nje?? halafu baada ya hiyo dakika moja naweza kuchaji tena ikaendelea kupiga mzigo??

Hi Ashangedere,
Hizo taa zinafaa kutumika kwa kila chumba, lakini kwa nyumba kubwa za mijini taa hizi ni ndogo sana. Zimetengenezwa kukidhi mahitaji ya taa za watu wa vijijini au rather wale wanaotumia koroboi, kandili na mishumaa. uwezo wake ni wa kumulika chumba cha futi 10X10, haziwezi kutumika kama security lamps.
Baada ya dk 1 ya kuchaji unaweza kupata mwanga kwa either masaa 2, 1.5 au 1. rejea maelezo yangu hapo juu.

Nashukuru kwa ushirikiano wako..
 
Sio za kichina hizo mkuuu... ni product ya The Nedherlands!
 
halafu baada ya hiyo saa moja ua mbili naweza kuchaji tena ikaendelea kupiga mzigo??![/QUOTE said:
Mbona swali hili Mkuu anaonekana kulikwepa?..ni mara ya 2 sasa hajibu!

PK & Ashangedere,
Kwa kujibu swali lenu, NDIO inawezekana wakuu. Kama charge itaisha baada ya hayo masaa 2, unaweza tena kuchaji kwa kuzungusha dk 1 tu na kupata tena mwanga kwa kadri unavotaka.
 
unaweka namba za simu ukipigiwa hupokei, we vipi?

Samahani sana mkuu but somtimes nakuwa kwenye sehemu zenye matatizo ya network au pia kikaoni. Please usichoke kujaribu kwani nikiwa kwenye position ya kuongea vizuri, napokea simu.
 
jamani wanajamvini akuna alojaribu hii kitu nafikiri kwa matatizo ya umeme wa tanzania vinatufaa kuwa nacho om kuepusha ajali za mishumaa na chemli jamani lakini ni kama wanavyoongea mana tatizo la wafanya biashara wa tz na wanapenda kuongea maelezo tofauti na kifaa wanakiongezea uwezo wa maneno ambayo mtengenezaji akuyaweka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom