TAKUKURU: Kuitwa kwenye mafunzo ya Uchunguzi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO YA AWALI YA UCHUNGUZI

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) anapenda kuwatangazia watu wote walioomba nafasi 320 za ajira ndani ya TAKUKURU kwamba mchakato wa ajira umefikia hatua ya kwenda kwenye Mafunzo ya Awali ya Uchunguzi.

Vigezo vilivyotumika katika kuwapata watu wanaotakiwa kwenda kwenye mafunzo ni pamoja na vifuatavyo;-

• Kiwango cha ufaulu wa mshiriki kwenye usaili;
• Haiba ya mshiriki; na
• Upekuzi kuhusu mwenendo wa kila mshiriki.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia:

1. Kila mshiriki anapaswa kuhudhuria Mafunzo ya Awali ya Uchunguzi yatakayofanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania Moshi;

2. Kwa upande wa nafasi ya AFISA UCHUNGUZI kila mshiriki anapaswa kuripoti kwenye Ofisi za TAKUKURU Kilimanjaro tarehe 10 Mei, 2023 siku ya Jumatano

3. Kwa upande wa nafasi ya MCHUNGUZI MSAIDIZI kila mshiriki anapaswa kuripoti kwenye Shule ya Polisi Tanzania Moshi tarehe 10 Julai, 2023 siku ya Jumatatu;

4. Maelekezo kuhusu ushiriki wa mafunzo haya yameainishwa kwenye barua ya wito.

5. Barua ya wito wa kwenda kwenye mafunzo imetumwa kwenye anwani na email ya kila mhusika.

Mkurugenzi Mkuu anawapongeza wote waliofanikiwa kuchaguliwa kwenda kwenye mafunzo hayo.

Imetolewa na;

Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
Mtaa wa Jamhuri, S.L.P 1291,
41101 DODOMA.
 
Back
Top Bottom