Tunamshukuru Waziri wa Ulinzi, Innocent Bashungwa kwa kuongelea ‘malengo’ ya ubinafsishaji wa bandari za Tanzania

Tumia akili, Bashugwa ni waziri ulitegemea aseme kinyume na maamuzi ya baraza la mawaziri ambayo mwekiti wake ni Rais? Tutumie akili sazingine.
Yaani badala ya kutekeleza majukumu yako ya ualimu huko Manyara,unahorojoka JF asubuhi asubuhi.
Kwa walimu kama wewe,elimu yetu kuwa hivi na kuwa na wajinga wengi waliopoteza muda kwenye vyumba viitwavyo madarasa ni halali.
 
Bandari, Licha ya kushughulika na upakiaji na upakuaji mizigo, bandari ni mpaka na lango kuu la nchi, hivyo bandari haipaswi kubinafsishwa kwa wageni.
Mapungufu ya utendaji pale bandarini ni matokeo ya ufisadi unaofanywa na kikundi cha watu wachache wanaofikiri wana akili zaidi ya wengine wanaofuata sheria. Bandari inaweza kuboreshwa kwa kufanya ubinafsishaji wa ndani kupitia soko letu la hisa.
Ifanyike tathmini ya mali za bandari, ina mashine ngapi za kupakulia mizigo? Mahitaji ya mashine yabainishwe na kama kuna mapungufu mashine zinunuliwe...Sio lazima tuikumbatie DPW hasa tukiwa taifa huru kwa miaka 60.
Nashauri, TPA ihamishiwe wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, iundwe kampuni ya Suma-TPA iorodheshwe kwenye soko letu la DSE ili mtaji utoke ndani ya nchi, kama itatulazimu kutafuta mwekezaji iwe ni baadhi ya gati, moja au mbili. Suma-TPA kama kampuni tanzu ya Jeshi iwezeshwe kununua winchi za kutosha. Kama tunanunua vifaru hatuwezi kushindwa kununua mitambo ya bandarini.
 
Bashungwa hana mawazo binafsi, yeye anafafanua maamuzi ya serikali inyaoongozwa na rais labda km una interest binafsi na Bashungwa

Tunachofanya hapa ni kazi ya "kuwaongoza viongozi" kwa njia ya hoja sanifu.

Ukweli kwamba Bashungwa yumo katika Baraza la Mawairi ni fursa muhimu kwa ajili ya kufanikisha lengo hili

Hatuna shida na siri za Baraza la Mawaziri
 
Bandari, Licha ya kushughulika na upakiaji na upakuaji mizigo, bandari ni mpaka na lango kuu la nchi, hivyo bandari haipaswi kubinafsishwa kwa wageni.
Mapungufu ya utendaji pale bandarini ni matokeo ya ufisadi unaofanywa na kikundi cha watu wachache wanaofikiri wana akili zaidi ya wengine wanaofuata sheria. Bandari inaweza kuboreshwa kwa kufanya ubinafsishaji wa ndani kupitia soko letu la hisa.
Ifanyike tathmini ya mali za bandari, ina mashine ngapi za kupakulia mizigo? Mahitaji ya mashine yabainishwe na kama kuna mapungufu mashine zinunuliwe...Sio lazima tuikumbatie DPW hasa tukiwa taifa huru kwa miaka 60.
Nashauri, TPA ihamishiwe wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa, indwe kampuni ya Suma-TPA iorodheshwe kwenye soko letu la DSE ili mtaji utoke ndani ya nchi, kama itatulazimu kutafuta mwekezaji iwe ni baadhi ya gati, moja au mbili. Suma-TPA kama kampuni tanzu ya Jeshi iwezeshwe kununua winchi za kutosha. Kama tunanunua vifaru hatuwezi kushindwa kununua mitambo ya bandarini.

Sheria yetu ya ubinafsishaji inataja "Airports, Aviation, Shipping, Navigation" kama eneo mojawapo la ubinafsishaji.
 
Sheria yetu ya ubinafsishaji inataja "aviation" (bandari) kama eneo mojawapo la ubinafsishaji.
Sheria zinaweza kubadilishwa Kama zinahatarisha usalama nchi. Anga, bandari, mawasiliano, nishati, usafirishaji ni maeneo yanayopaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa. Ni maeneo tunayopaswa kuyahudumia wenyewe.
 
Bashungwa mdomo wake umeoimda, uko tenge hasa akiwa anaongea propaganda

Nashauri tujitofautishe na kina Mary Chatanda wasioheshimu tofauti kati ya valid and sound reasoning dhidi ya fallacious reasoning.

Tujadili hoja bila kumkwarua mleta hoja, tupokee ujumbe hata kama tunamkataa mjumbe
 
Unasoma vichwa vya habari tu



Halafu unabweka Kama mbwa mwenye kichaa. Stupid
Ndicho nilichokiona! Niliposoma kichwa Cha habari kidogo ni-gnore content lakini baada ya kusoma content Mama Amon ana hoja nzito inayohitaji majibu mazito! Nani wa kuyajibu? Wakati kwenye mfumo wamejaa vilaza wanaongalia matumbo yao Leo na sio future ya kizazi Cha Leo na kesho?
 
Nakuelewaga sana mama Amon.

JE umeupitia MKATABA WA DP world na SELIKALI ya Tanzania????

Unaweza ukaweka madhaifu yake pia.

NB. HAKUNA MTU ANAYEKATAA UWEKEZAJI/UBINAFSISHAJI, SHIDA NI HUO MKATABA.
Ukisoma bandiko la mama Amon ameainisha maeneo kama matatu yenye ukakasi. Tujitahidi kusoma kabla ya kujibu. Nadhani hata viongozi waliyosaini hiyo IGA hawakasoma na kutafakuri Kwa kina tena Kwa kutumia experts
 


Tumefurahi kumsikia Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa, akiongelea uzuri wa malengo ya uwekezaji katika Bandari za Tanzania.

Lakini Mhe. Bashungwa anapinga mtazamo kwamba mkataba wa Tanzania na Dubai unaongelea ubianafsishaji wa bandari.

Mara ya kwanza tulimsikia Spika Tulia Ackson akimkataza Profesa Kitila Mkumbo kutumia neno "ubinafsishaji" wakati wa mjadala wa Bunge tarehe 10 Juni 2023 kwa ajili ya kurasimisha mkataba huu.

Wakati huo tulikaa kimya juu ya katazo hili kwa kuwa Spika sio mchumi. Lakini Waziri Bashungwa ni mchumi mwenye shahada ya uzamili, na amefanya kazi Benki ya Dunia abaye ni kiranja mkuu wa ubinafsishahaji duniani. Kwa hiyo sasa ni wakati mwafaka kurekebisha dosari husika.

Tunachojua kuhusu maana na mipaka ya ubinafsishaji;

Kwa mujibu wa Savas (1987), "ubinafsishaji ni mchakato wa kuhamisha asilimia yote au asilimia kidogo ya umiliki wa rasilimali au taasisi zinazomilikiwa na serikali na kuziweka mikononi mwa wajasiriamali walioko kwenye sekta binafsi kwa ajili ya kuongeza kasi ya utendaji, tija na kuipunguzia serikali mzigo wa gharama za uendeshaji."

Kwa ufafanuzi zaidi tunaweza kurejea kazi ya E.S. Savas (1987), "Privatisation: The Key to Better Government (Chatham: Chatham House Publishing Inc)."

Kitabu hiki kinaonyesha kuwa mchakato huu unaweza kuhamisha asilimia yote au asilimia kidogo ya ummiliki wa haki zinazohusu matumizi (use ownership rights), au umiliki wa haki zinazohusu faida (fruits ownership rights), au umiliki wa haki zinazohusu uwezo wa kuuza kitu kinachoilikiwa (substantive ownership rights), au baadhi ya haya matatu, au yote matatu kwa pamoja.

Maoni yetu ni kuwa, kwa kuzingatia fasili hiyo hapo juu, na kutazama malengo ya mkataba wa awali kati ya Tanzania na Dubai, kinachoendelea kupitia mkataba wa awali kati ya Tanzania na Dubai ni mcchakato wa ubinafsishaji.

Kwa hakika, ibara ya 2(1) ya mkataba huu inathibitisha haya kwa kusema yafuatayo:

1689605005061.png


Tunakubaliana na Waziri wa Ulinzi, Mhe. Bashungwa, kwamba malengo ya ubinafsishaji wa bandari yanawafaa, sio CCM pekee, bali umma wote wa Tanania.

Tunaelewa kwamba nchini Tanzania ubinafsishaji unaratibiwa chini ya sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ya mwaka 2010.

Yaani, "The Public-Private Partnership Act No.10/2010, Chapter 103," ambapo ibara ya 6(3) inataja maeneo 26 ya ushirikiano wa kiuhumi kati ya serikali na wawekezaji binafsi, yaanii:
  1. "Crop farming,
  2. Livestock,
  3. Poultry,
  4. Fisheries,
  5. Irrigation,
  6. roads,
  7. Bridges,
  8. Railways,
  9. Airports,
  10. Aviation,
  11. Shipping,
  12. Navigation,
  13. Energy,
  14. Buildings,
  15. Industry,
  16. Exploration,
  17. Mining,
  18. Education,
  19. Health,
  20. Environmental Conservation,
  21. Waste Management,
  22. Information Technology,
  23. Communication Technology,
  24. Trade,
  25. Sports, and
  26. Recreation."
Kwa mujibu wa sheria zetu ubinafsishaji ni sera ya Taifa. Na katika sekta yoyote kati ya sekta hizi 26 ubinafsisiahji unaweza kufanyika kwa asilimia kidogo au asilimia zote mia moja.

Kwa hiyo, sio dhambi serikali ya Tanzania, ikiwemo serikali ya CCM, kubinafsisha bandari kwa kutumia mbinu yoyote halali.

Tatizo; Mbinu haramu haziwezi kuzaa matokeo halali

Tatizo ni kwaba katika mchakato wa sasa ni kwamba serikali na baadhi ya iongoi wa CCM katika CC na NEC wanatumia mbinu haramu ili kufanikisha malengo mazuri, jambo ambalo haliweekani. Tutaeleza.

Kwanza, kuna utata kwenye ibara ya 2(1), kuhusu aina na wigo wa mkataba wa Tanzania na Dubai juu ya ubinafsishaji unaokusudiwa. Maneno niliyoyapigilia msitari hapa chini yanahusika.

1689596226187.png


Maneno yenye utata na yanayoleta hofu kwa wananchi wakazi wa maeneo yaliyo jirani na maeneo yanayoguswa na mkataba ni haya;

"...areas of cooperation for the development, improvement, management and operation of SEA AND LAKE PORTS, SPECIAL ECONOMIC ZONES, LOGISTIC PARKS, TRADE CORRIDORS and other related strategic port infrastructure in Tanzania."

Maneno haya yakisomwa pamoja na maudhui ya awau ya pili ya utekelezaji wa mkataba kama yanavyoonekana kwenye Kiambatanisho Na. 01 yanazua utata na hofu kubwa. Sehemu ya Kiambatanisho hicho yenye kuongeza hofu ni hii hapa:

View attachment 2691778

Majukumu ya bandari na miundombinu yake hutumia ardhi ambayo imefungamana na maisha ya kila siku ya wakazi walio jirani na uwekezaji wa aina hiyo.

Kuhusu ardhi hiyo, sheria tajwa ya ubia inasema yafuatayo katika ibara namba 13:

"13. Where, the project requires acquisition of land for its implementation, the acquisition shall be carried on in accordance with the Land Act, Village Land Act, the Land User Planning Act, Land Acquisition Act and any other relevant laws."

Hivyo, wananchi walioko katika mwambao wa Bahari ya Hindi na miambao ya maziwa kama vile Ziwa Nyasa, Ziwa Viktoria na Ziwa Tanganyika wanataka kusikia serikali inasema nini kuhusu ardhi zao, kwa kuzingatia matakwa haya ya kisheria.

Pili, kuna tatizo la kufanya mambo kana kwamba sheria na kanuni za nchi zinazoongoza ubinafsishaji hazipo. Aina ya ubinafsishaji unaokusudiwa na serikali haiko bayana.

Kanuni namba 02, katika, Toleo Na. 37/2020, inasema kwamba ubinafsishaji unaweza kutekelezwa kwa kutumia modeli za ushirikiano ("partnership models") zifuatazo:

"(a) service and management contracts;
(b) design, build, operate and transfer;
(c) design, build, operate and maintain;
(d) build, operate and transfer;
(e) design, build and operate;
(f) design, build, finance, operate and maintain;
(g) build, own, operate and transfer;
(h) build, lease and transfer;
(i) build, transfer and operate;
(j) operation and maintenance;
(k) operation, maintenance and management; and
(l) lease, develop and operate."


Katika kitabu chake , "Privatization and Public–Private Partnerships (New Jersey: Chatham House)," Savas (2000:246) amechanganua aina hizi za ubinafsishaji kama ifuatavyo:
View attachment 2691724

Katika muktadha huu, watu wanauliza: ndoa ya Tanzania na Dubai itasimama kwa kutumia miguu gani? Swali hili halijapatiwa jawabu kamilifu.

Kwa kuwa IGA inaweka misingi ya ushirikiano, kulihitajika ibara nzima kwa ajili ya kufafanua jabo hili ndani yake. Tunaona kwamba haipo. Kama ipo imetumia misamiati mbadala ambayo imetupiga chenga.

Tatizo la tatu ni kwamba, hatua za kikanuni za ubinafsishaji zinazotajwa kwenye Kanuni za ubinafsishaji, Toleo Na. 37/2020, ibara ya 34-61, hazionekani kuzingatiwa na serikali.

Tayari Waziri Mbarawa aetufahamisha tangu tarehe 15 Julai 2023 kwamba mchakato wa kubinafsisha bandari zetu unahusu "solicited proposals/projects." Kuhusu aina hii ya ubinafsishaji hatua husika ni hizi hapa;

34. Procurement principles.
35. Methods of procurement of unsolicited projects.
36. Market sounding
37. Procurement of solicited project.
38. Bidding criteria of a private party.
39. Issuance of Pre-qualification documents.
40. Pre-qualification proceedings.
41. Participation of consortia.
42. Clarification of applications for pre-qualification.
43. Appointment of evaluation team.
44. Receipt, evaluation of applications for pre-qualification.
45. Approval of shortlist.
46. Contents of request for proposals.
47. Approval and issuance of request for proposals.
48. Further demonstration of fulfilment of qualification criteria.
49. Bid securities for solicited proposal.
50. Clarification and modification of bid documents.
51. Submission of bids.
52. Extension of time for submission of bids.
53. Evaluation of submitted proposal.
54. General evaluation criteria.
55. Financial evaluation criteria.
56. Evaluation of proposals based on criteria in bidding document.
57. Conduct of due diligence.
58. Preferred and reserve bidders.
59. Value for money report.
60. Approval of award of contract by Steering Committee.

61. Notice of intention to award contract.

Kanuni hizi ni sehemu ya sheria za nchi zinazoongoza ubinafsishaji, hata bila kujali sera za CCM zinasema nini.

Zimekiukwa kwa asiliia 100 na watu wote serikalini wamekaa kimya kwa sababu ya kubembeleza urafiki wa Kaizari.

"Ukipinga au kukosoa mkataba wa Tanzania na Dubai unapinga jambo la Mama," ndio kaulimbiu inayotumika kama nyenzo ya vitisho.

Hilo linakubalika kwenye dola ya Kisultani kama vile Dubai lakini Sio katika Tanzania ya Nyerere ambayo ni Jamhuri!

Na tatizo la nne ni kwamba, mkataba wa Tanania na Dubai unapendekeza ubinafsishaji utakaopitia mchakato wenye hatua kuu nne. Yaani,
  1. Mkataba wa awali wa kiserikali,
  2. Mikataba ya nyongeza ya kibiashara,
  3. Mkataba wa kukodishana uendeshaji wa bandari, na
  4. Mikataba ya kukodishana ardhi.
Yaani,
  1. Inter-governmental agreements (IGA),
  2. Host government agreements (HGA),
  3. Concessional agreements and
  4. Lease agreements."
Mchakato huu hautokani na sheria wala kanuni za ubinafsishaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Badala yake, tunatumia sheria na kanuni za serikali ya Dubai kuendesha serikali ya Tanzania. Jabo hili sio salama kwa nchi yetu. Ni kuuza uhuru na utaifa wetu.

Hitimisho na mapendekezo

Kwa ujumla, sheria ya ubinafsishaji na kanuni zake vinaanzisha mfumo murua wa kisheria unaosimamia ubia wa watu au kampuni binafsi katika miradi ya Serikali kupitia mikataba maalum
.

Ubia huo una lengo la kutekeleza marekebisho ya kiuchumi na kijamii nchini kwa lengo la kusaidia kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Watanzania wanataka kusikia viongozi wa chama na serikali wakiongea maneno yanayoakisi sheria na kanuni hizi. Bado kazi hii haijafanyika.

Mhe. Bashungwa na wenzake ambao ni wataalam wa uchumi na sheria wanaweza kuziba pengo hili kwa kiasi kikubwa. Tunawaomba wajitahidi kufikiri nje ya sanduki la kivyama maana Tanzania ni kubwa kuliko vyama.


Kwa ujumla, tunahimiza serikali kuheshimu sheria na kanuni za ubinafsishaji zilizopo kwa kuzingatia vifungu vyote vya kanuni zetu kuhusu jabo hili.

Mawazo yetu ni hayo tu kwa sasa. Tunamtakia Mhe. Bashungwa uchapa kazi bora na ufanisi katika siasa za kitaifa.

Ubinafsishaji makini hoye!,
Ubinafsishaji holela mwiko!

Mama Amon Desk,
"Sumbawanga Town"
Sumbawanga.
17 Julai 2023.

Hata hii ilikuwa na malengo mazuri, hivyo hatutakiwi kuangalia upande huo Tu, Bali WA kisheria na matokeo yake.

Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260​

1 of 4Next Last
Jump to newWatch
•••

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member​

Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 (zaidi ya bilioni 260 za Tanzania) kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi wa mwaka 2018 kufuta Leseni yao ya Kuhifadhi madini ya Nikeli.

Kampuni hizo zilifanikiwa kuishitaki Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa kwa kunyang'anya leseni hiyo.

Tanzania pia imetakiwa kulipa dola milioni 3.859 za gharama za kisheria kwa wadai, pamoja na ada na gharama za mahakama ya ICSID.

Kampuni ya Indiana Resources Ltd iliyoorodheshwa kutoka Australia, ambayo ndiyo wanahisa wengi wa mradi wa nikeli wa Ntaka, iliwahi kutishia kukamata ndege zinazoendeshwa na Kampuni ya Air Tanzania (ATCL). Indiana inasema sasa itachukua hatua haraka kutekeleza tuzo ya mahakama

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Uswidi mwaka jana zilishinda uamuzi wa $165m dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa serikali ya Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Sweden na Tanzania (BIT)

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.
 
Kwa kuwa miradi yote ya bandari inatekelezwa ndani ya mipaka ya Tanzania hakuna sababu ya IGA.
Huo ndiyo ukweli ambao wanapaswa kuujua. Matatizo ya ufanisi wa bandari ya DSM hayaihusu serikali ya kifalme ya Dubai. They are not problems of mutual interest between the two governments as per definition of IGA.

Sababu inayotolewa na Hamza Johari, aliyekuwa mwenyekiti wa Negotiation Committee, ya kwamba DP World wamejenga bandari kavu huko Rwanda na DRC haina mashiko yo yote. Hizo bandari kavu alizojenga huko si mali yake, ni mali ya serikali za Rwanda na DRC. Yeye alikuwa ni mjenzi tu. Wenye kuamua watumie bandari ipi kupitisha mizigo yao ni serikali za Rwanda na DR Congo. Hivyo kama ni kuingia mkataba wa IGA, tunapaswa kuingia IGAs na nchi za Rwanda na DRC kwani ndizo nchi tulizo na mutual interest ya matatizo ya bandari ya DSM. Pia nchi ya Uganda. Huyu DP World sana sana tungeliweza kumpa kazi ya ujenzi wa bandari kavu la kisasa huko Mwanza kwa mizigo ya Uganda. Tungeweza kuwashawishi Uganda wampe kazi ya kujenga bandari kavu ya aina hiyo pale Port Bell ili mizigo yao ikishafika Dar Port iweze kusafirishwa haraka kwa SGR na meli yetu ya HKT (Hapa Kazi Tu) hadi Port Bell ndani ya saa kumi!
 
NImemsifia kwa kuongelea alengo mema ya ubinafsishaji wa bandari

NImekosoa mbinu haramu zinazotumika kwenye ubinafsishaji wa bandari kwa kuonyesha kuwa kinahoendelea pale ni ubinafsisiahji bila kufuata sheria ya PPP na kanuni zake

Kosa liko wapi?

Nasubiri jibu lako
Kumradhi nilighadhibika nisamehe mwanangu. Nilikuwa na mambo mengi. Hivyo, sikujipa muda wa kusoma na kutafakari kila kitu.
 
Back
Top Bottom