Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Mzeee Kyoma,

Pole mzee na vitisho, ila mimi ninakuomba nitumie kwenye pm uko nchi gani halafu unipe masaa kama sita nitakwambia huyo mtu ni nani,

wewe nitajie nchi tu inatosha, tunahitaji kupambana sambamba na huu ujinga hapa forum leo kwako kesho itakuwa kwa mwingine!
 
Kyomo

Umewagusa vibaka pale ambapo hawataki washikwe; Ipo siku wote watalipa tena hapa hapa duniani. Wanawatumia watu wao ili kupotosha ukweli lakini ukweli utasemwa tu, hii tamaa yote ya EAC Federation inatokea huko huko kwa hawa wezi waliokubuhu kwani waliona jinsi ambavyo hatua zilivyokuwa zinaendelea.
 
KNKU,
kwa kila kiongozi aliyekwenda kutibiwa nchi za nje miaka ya zamani, basi elewa alikuwepo Mtanzania mwingine mwenye kuihitaji zaidi nafasi hiyo. katika hili la matibabu nakuhakikishia kwamba hawana tofauti na hawa wa leo.

vilevile tulikuwa tukijiita wajamaa na kuzikandia nchi za magharibi kwa msingi huo kwenda nchi za mashariki was the prefered option.

hivi unafahamu kwamba kila kiongozi mkuu pale Tanzania anatibiwa na daktari bingwa wa Muhimbili? hata augue mafua anakwenda kumuona daktari bingwa!! wanaposafiri nje ya nchi wanaambatana na daktari bingwa. sasa hebu jiulize huyo daktari ameacha wagonjwa wake wangapi wakitaabika?

unapoambiwa Sokoine/Mwalimu amefariki akiwa na pea mbili la viatu unaweza kufikiri labda huyu Mzee alikuwa akisafiri na mkokoteni au rikwama. NOOO, alikuwa akisafiri na msafara wa Mabenzi, new model, kama Lowassa na Kikwete.

Hata wakati wakisomesha watoto wao shule za serikali bado walikuwa wakisoma shule unazoweza kuziita "first class" za wakati huo. Kwa hiyo tusijidanganye kwamba viongozi wa miaka hiyo walikuwa na roho nzuri, huruma, na ukarimu, kuliko hawa wa sasa.

Kyoma,
kwanza pole kwa maswahibu yaliyokukuta. Ninapenda mtu anayejenga hoja kwa ushahidi/data. Forum ilianza kupooza lakini naona umeichangamsga.

Hoja yako ni ndefu sana, jaribu kutoa "dose" ndogo ndogo next time. vilevile, jaribu kutenganisha kwa paragraph ili iwe rahisi kujibiwa kipengele kimoja-kimoja.

Sasa kama nilivyoeleza, hoja yako ni ndefu, pia umeitetea kwa data, hivyo ninahitaji kuvuta pumzi kabla sijaijibu.
 
Mzee Joka,

Taifa letu kama mataifa yote duniani yalivyo, tuna utaratibu wa kuwahudumia viongozi wetu wakuu wa taifa, kisheria, ni na madhumuni ni kuwapunguzia mzigo wa kuhangaika na maisha ili waweze kuutumia muda wao wote kwa kulitumikia taifa,

Sasa tusingetegemea rais wa jamhuri na waziri mkuu wake, kusafiri kwa kutumia "nguruwe" kama enzi zile 504 ilivyokuwa ikiitwa, tunawanunulia mabezni ya kisasa tukiwa na understanding kuwa in the process ya uongozi wao pia watahitaji kuwapokea viongozi wageni toka nje, na wao pia tunawapatia usafiri mathubuti ili waweze kuwafikia wananchi kwa uhakika na ontime,

Watoto wa Mwalimu na Marehemu, si kweli kwamba walisomeshwa shule za "First Class", katika wakati wao shule za namna hiyo zilikuwa tatu hapa Dar, nazo ni Bunge Primary, Dar International School, na Arusha International School, hakuna mtoto wa hao wazee aliyesoma hizo shule, kwa hiyo hiyo hoja ni weak, halafu hata watoto wao waliosoma nje walisoma kwenye Communists Countries, ambako ukweli hakukuwa na tofauti yoyote na bongo kwenye hizo nji, na mpaka leo hii sio rahisi kupata kazi as kazi, ukiwa na vyeti vya hizo nchi, na sio siri kuwa watoto wa viongozi hao wawili mpaka leo ni wananchi wa kawaida as opposed na watoto wa viongozi wa hivi karibuni, kuacha mmoja tu aliyeko DC, ambaye naye pia alipelekwa huko kwa huruma ya Mzee Kibelloh akiwa katibu mkuu foreign, kwa hiyo dhana ya kwamba watoto wao walisoma "First Class" nayo pia sio loaded!

Leo Mwalimu, hakuacha mali kabisaa, the matter of fact siku amefariki nyumba yake kule Msasani ilibidi ifanyiwe ukarabati wa haraka haraka na serikali, ama sivyo ingekuwa aibu ya Century, Marehemu Sokoine, yeye aliacha ng'ombe wengi sana ambao alikuwa nao hata kabla hajawa waziri mkuu, otherwise hakuwa na mahekalu, kama tunavyojionea viongozi wa hivi karibuni,

Kuhusu madakitari wa Muhimbili, ni kweli kabisaa, kama tuna kiongozi wa taifa anaumwa, ni sawa kabisa kwa dakitari bingwa pale Muhimbili kutoa huduma kwa kiongozi huyo kwanza ili aweze kuwahi kurudi kuliongoza taifa, ama sivyo taifa litaenda mrama hivi kweli hili linahitaji kujadiliwa nalo? wanaotangulia vitani ni wanajeshi wa vyeo gani?

Ninarudia kuwa viognozi hao wa zamani walikuwa na nia njema, lakini hawakuwa na mipango kamili namna ya kutekeleza nia zao, ndio maana yakatokea matatizo au mapungufu katika maamuzi yao! Cha muhimu tunachoweza kufanya leo ni kurekebisha waliposhindwa, na kuendeleza mazuri waliyoyafanya!
 
Mzee ES,
kama walisoma nchi za Kikomunisti basi ujue huko ndiko walikoweza kwenda, it was not a matter of choice. kwa viongozi walioishi oysterbay watoto wao walisoma O'bay, walioishi Upanga walisoma Muhimbili, maeneo ya Ikulu walisoma Bunge. Hizo hazikuwa shule za daraja sawa na Gerezani,Mtendeni,Ilala Boma, Mzimuni n.k n.k.

Ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba viongozi walipeleka watoto wao kwenye shule ambazo waliamini zinatoa elimu nzuri. Sidhani kama lilikuwa ni suala la uzalendo hapo.

Mimi naendelea kusisitiza kwamba viongozi wetu wamekuwa wakiishi maisha ya kifahari kwa muda mrefu tu. Mabenzi waliyokuwa wakitumia yalikuwa ni latest model ya miaka hiyo. Kama ingekuwa uzalendo wangeweza ku-downgrade na kutumia 504. Infact, Nigeria kuna kipindi viongozi wao walikuwa wanatumia 504s that were assembled in Nigeria.
 
jokaKuu

Hebu tuelezee tofauti ya msafara wa Julius Kambarage Nyerere (RIP), Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na sasa Jakaya Mrisho Kikwete. (Anapotoka Ofisini kwenda nyumbani au vice versa).
 
Mzee Joka,

Enzi hizo shule zilikuwa by location, kwa hiyo viongozi waliokuwa wakiishi hayo maneno ya uzunguni watoto wao walisoam shule za karibu na majumbani mwao, yaani uzunguni na moja ya priviledge ya hsule hizo, ni kwamba zilikuwa bado zina standards za kizungu kwa sababu bado kulikuwa na wazungu wengi waliokuwa wakiishi maeneo hayo,

na wale waalimu wa kimarekani wa volunteers ambao waliletwa kwa kuombwa na Mwalimu, wengi wao waliweza kuishi maeneo hayo kwa muda mrefu kidogo ndio maana wakaweza kuzifanya shule hizo ziwe na level tofauti kidogo na zingine ulizozitaja, that is all,

shule zingine ulizozitaja hazikuwa na level sawa na hizo za uzunguni kwa sababu hasa ya location, lakini kwenye hizo shule ulizozitaja vijana wengi mpya waliofeli darasa la saba mikoani walikuwa wakija na kuzitumia kupasi darasa la saba kwenda la tisa, maana wanafunzi wake wenngi walikuwa hawajali masomo, sasa wa kulamuiwa ni nani hapo wanafunzi au location, hiyo debate by itself,

Nigeria walitumia 504s kwa viongozi, halafu viongozi hao waliweka hela ngapi mabenki ya Ulaya? Unajua Gowon alichukua hela ngapi za nchi hiyo? Viongozi wetu wa enzi zile hawakuwa sawa na wa sasa, the matter of fact viongozi wengi wa zamani alianza kushituka baada ya kuona Mwalimu ame-retire, lakini anaendelea kugharamiwa na serikali huku wao wakifa njaa, ndio kina Kingunge wakaanza na wengine wote wakashituka!
 
Hii issue ya kusema kuwa viongozi walipeleka watoto wao shule expensive sikubaliani nalo, sidhani kama ingemake sense kiongozi anaakaa Oysterbay apeleke mtoto akasome Makurumula ama Temeke kama angefanya hivyo najua lazima wananchi wangepata la kusema "Oh anatumia gari na mafuta ya serikali kumfuata mtoto shule ya mbali wakati angeweza kumpeleka shule za karibu".Nimebahatika kusoma na watoto wa vigogo wa enzi hizo na wa sasa kulikuwa na tofauti kubwa sana wale wa zamani watoto wao tulikuwa tunauchapa mguu vizuri tu kwenda nyumbani wakati hawa wa sasa wanafutwa na gari la mheshimiwa na linasubiri.

Kitu kimoja ambacho namshukuru nyerere aliondoa mambo ya madaraja(Upper/Middle/Lower class) kwenye elimu, kulinganisha na nchi nyingi za jirani.

Kuhusu misafara ya viongozi jamani inabidi tukubaliane kuwa Rais au waziri mkuu sio mwenzetu kwa hiyo lazima asafiri in class ata hao unaosema wanatumia 504 nina uhakika zilikuwa sio 504 ambazo wewe au mimi tunanunua kila siku lazima zilikuwa zinameet Presidential Needs I.e enhanced Security features and other things of that sort, Nigeria kutumia hayo magari ilikuwa ni kusupport mali zinazozalishwa kwao, nadhani wengi wetu tumegundua kuwa nchi zote zinazojiweza kiuchumi zinatumia magari/ndege zinazotengenezwa kwao(uzalendo).
 
wakati tunajadili mada kuu tusipuuzie matisho aliyopewa kyoma.
Inanipa wasiwasi kuwa kuna kitengo cha ufuatiliaji wana JF. naomba kutolewa wasiwasi please...Kyoma, are you there?
 
Joka kuu!

Mzee Es Na Icadon!

wamekujibu na mimi kwa kuweka msisitizo wakati wa mwalimu hata baadhi ya watoto kama kina John na Obote wakati huo walisoma shule za kawaida na walikuwa hawapelekwi shule na usafiri.Kina Rosemary walisoma Zanaki na Usafiri walichukua wa kawaida hebu nipe mfano wa viongozi wakuu wetu wa leo watoto wao wanaosoma Government School Kuanzia msingi hadi sekondari.

Maisha kwa walisoma wakati ule yalikuwa na thamani bila ya kujali wewe una mtu wa kukupendelea au laah,Usawa kwa kiasi fulani ulikuwepo.Angalia watoto wa wakubwa mbali mbali tulivyokuwa tukisota nao kule JKT,Kuhusu hao viongozi wengi waliokuwa wakitibiwa nje ni baada ya Muhimbili kushindikana na hata wasiokuwa viongozi walikuwa wakipata nafasi hiyo,Na wale viongozi waliotajwa hapo kama kina sokoine na Kawawa kwamba walienda kutibiwa nje ni mara chache na wengi ilikuwa ni mashariki kama msaada kama tulivyokuwa tunasomeshewa wanafunzi wetu na hao wakomunisti.Si kwamba walikuwa wanaenda huko kwasababu hawakuwa na alternatives au kwasababu walisoma huko hilo si kweli walikuwa na uwezo hata kwenda kutibiwa London lakini hawakufanya hivyo.

Angalia viongozi wetu wa leo Muhimbili wameicha bila ya uangalizi wa maana na wao wakiumwa kidogo ni west au Bondeni.

Hivi kama unaelewa Nyerere hata mama yake alilazwa pale mwaisela mara kadhaa na hata mwalimu alikuwa akienda kumuangalia na watu kama mimi kina mlalahoi nilikuwa ninapishana na mwalimu anatoka kumtizama Mama yake wa Kumzaa,Hivi hawa viongozi wetu wa leo ni nani atampeleka mzazi wake akatibiwe muhimbili ktk hali ya ugonjwa mkubwa na hata mdogo...

Nafikiri cha kwanza watafikiri mahospitali binafsi kama ni ugonjwa mdogo then kama ni mkubwa ni nje kwa kimemo haraka wizara ya Afya au kupitia kwa Mwakyusa Bungeni.

Kuna tofauti kubwa.Hivi Unaelewa kwamba sokoine mara kadha alikuwa akiendesha mwenyewe kwenda kanisani na mara kadha alikata kusindikizwa kwa msafara kwa kusema hapendelei kuwaweka watu mabarabarani,

Leo viongozi wanaona fahari kuweka msururu wa watu barabarani kwa kutanguliza ving'ora.
 
Mkuu Invisible

Heshima yako mkuu, hebu tuhabarishe nikitu gani kimetokea kwa Kyoma?

Mzee Kyoma,
Mwaga mavitu, na kwa kukuhakikishia tu, mpaka hivi sasa hakuna doa ktk maandishi yako. huyu mpuuzi tutakula naye sahani moja.
 
Mimi nilikuwa mdogo sana kujua uzuri au ubaya wa Sokoine, lakini nakumbuka alikuwa akisifiwa sana kwa utendaji wake wa kazi wakati huo.
Most importantly, your WB & IMF thread has made my weekend. Hiyo nitaicopy and paste somewhere.
I salute you!!
 
Mzee Kyoma
Hii analysis ya WB na IMF ingefaa kutoka kama kachapisho kwa ajili ya consumption ya waTz wa kawaida kama mimi, just my opinion.
 
Waheshimiwa,

Hapa nilipo inakaribia saa kumi na mbili asubuhi. Kuna mtu amenipigia simu na kuacha ujumbe kuwa jumbe zangu ninazoandika Jambo Forums zitanitia matatizoni. Sijuhi ni nani, na amepata wapi namba yangu, na amejuaje utambulisho wangu. Ngoja kwanza niwasiliane na provider wangu wa simu ili nijue hiyo simu imetoka wapi, kwa sababu haionyeshi namba kwenye call Id, pia, hata nikiwa nasikiliza ujumbe, namba haitajwi. Mtu mwenyewe anaongea Kiingereza lakini sio lafudhi ya kitanzania.

ujumbe wenyewe sio mzuri, una vitisho.

Kyoma, fanya kila liwezekanalo ID ya huyo mtu ifahamike. Huyo mtu au watu ni adui wa Taifa la waTanzania. You can count on me should you need help in this issue.

Nimesoma taarifa yako yote uliyoiandika humu, pamoja na kwamba ni ndefu kiasi kwamba wengi ya wasomaji walio na mazoea ya ku-scheme through taarifa ndefu hawataimudu. I am impressed by your outlook on such issues.

Kitabu kuhusu Sokoine kitakuwa tayari lini?
 
Wazee wote, Heshima kwenu,

Kwanza nimefarijika sana na ujumbe kutoka kwa kila mmoja wenu. Binafsi, mwanzoni nilidhani hiki ni kijiwe cha kupiga soga, lakini nimekuja kugundua vinginevyo. Hakika jumbe zenu zimenifanya nitambue kuwa siko pke yangu. Pamoja na kusigishana kimawazo na mikwaruzo ya hapa na pale, mmoja wetu akipatwa na misukasuko, wote mnakuwa kitu kimoja hata kama tunatofautiana mawazo. Nimefarijika na nawashukuru sana kwa hilo. Hata hawa watu wanaosoma jumbe zetu kwa nia ya kutokutaka kujifunza, bali kuwanyamazisha wengine, naona watakatishwa tamaa na hali yenu mliyoonyesha ya kutokukubali kutishana.

Siwezi wataja kwa majina, ila nawashukuru wote walioandika humu ndani, na wale walionitumia ujumbe binafsi ambao nimewajibu, na hata wale wanaojua identity yangu na kunipigia simu, nawashukuru pia. Mungu awajalie mibaraka fori. Baada ya kuhakikisha kila kitu kiko sawa, nikishirikiana na waliojitolea, tutawafikishia ujumbe niliopewa ili muusikilize.

Nimepitia mabandiko yangu karibu yote na kuyasoma kwa makini. Sioni mahala nilipoteleza mpaka kumshika mtu jichoni. Hakuna nyaraka za serikali nilizotumia, kwani hata habari za mikopo nilizifuatilia kutokana na press release zitolewazo na Benki ya dunia. Sio jando. Ndio maana niliandika kwa mfano habari namba 2006/400/AFR, ambalo ni faili la benki ya dunia. Sikuona sehemu nimemtukana kiongozi, bali hata kama nilitumia lugha ya kejeli, ninaweza nikaitetea kwa mifano zaidi. Nimenukuu mawaziri bungeni, na pia nimenukuu ripoti za mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali. Hivi vitu vyote viko wazi, nilichofanya ni kuviunganisha ili kujibu hoja.

Naamini hoja inakuwa nzito kama kuna takwimu na mifano. Nafikiri kuwa hoja inajibiwa kwa hoja, wala hoja haijibiwi kwa vitisho. Naomba yeyote anayeona nimekosea mahali fulani, aninukuu na kunisaihisha, nami nitamjibu. Niliandika humu ukumbini, na wala sikumpigia mtu simu. Naomba nijibiwe kwa njia hiyohiyo. Viongozi wetu ni wa kitaifa, hivyo lazima wajadiliwe. Anayeona hataki kujadiliwa, aje benchi huku tupige wote debe. Itakuwa si busara, kuwajadili baadhi ya viongozi na kuwaacha wengine. Naahidi kuwa nitaendelea kuandika pindi nipatapo nafasi.

Kwa ufupi tu, nimejua simu imetoka nchi gani, lakini bado hawajanipatia namba. Nimehamishiwa sehemu nyingine nitakapopatiwa namba by Monday. Mtu mwenyewe alitumia kadi ya simu, lakini nimeambiwa hilo sio tatizo. Nilikuwa sijalala, na simu ilikuwa inalia napokea alafu inakatika gafla. Mtindo huo ulijirudia kama mara nne, ndipo niliamua kutokupokea. Baadae nilipata signal kuwa kuna new message. Huyo mtu alianza kwa salamu, alafu akaendelea kwa kunitaja sir name yangu bila kutaja jina langu la kwanza. Akasema natumia jina la Kyoma katika mtadao wa mawasiliano unaoitwa JamboForums. Nitaishia hapa kwa makusudi.

Nikipata muda nitaendelea kuandika kwa kumalizia kiporo cha tofauti kati ya Lowasa na Sokoine. Pia nitamalizia kiporo cha mjadala wangu na JokaKuu kuhusu "Sera" za hawa majangiri. Jumbe zenu zimenihakikishia kuwa mnachukizwa na hawa wababaishaji wenye vitisho visivyokuwa na kichwa wala miguu. Nawashukuru wote.
 
KNKU,
Kyoma,
Sasa kama nilivyoeleza, hoja yako ni ndefu, pia umeitetea kwa data, hivyo ninahitaji kuvuta pumzi kabla sijaijibu.

Mzee JokaKuu,

Nitasubiri majibu yako kwa hamu, lakini wakati unapata pumzi, mimi niendelee na huu mjadala kwa kumalizia kiporo kilichobakia. Ukisha nijibu, ndipo tuanze mjadala wa nguvu kuhusu haya Majangiri. Kumbuka pia kuwa tofauti kubwa kati ya Sokoine, Nyerere na viongozi wetu wa sasa, ni kuwa Sokoine na Nyerere hawakuhujumu uchumi wa nchi yetu, bali viongozi wa sasa wanahujumu uchumi kwa kushirikiana na IMF na WB.

Saihisho, katika paragrafu ya nyuma, niliandika kuwa June 8, 2004 Serikali ya Tanzania ilipata mkopo wa dola za kimarekani milioni 43.8 kutoka katika Benki ya Dunia kwa sababu ya mpango wa dharura wa kupunguza makali ya mgao wa umeme uliokuwa ukilikabili taifa letu. Hata hivyo, kadili ya Ripoti iliyotolewa na (Transparency International), Serikali ya awamu ya tatu iliridhia na kukubali Tanesco isaini mkataba wa kuilipa IPTL dola za kimarekani 2.5. Isomeke kuwa Tanesco inailipa IPTL dola za kimarekani Milioni 2.5 kila mwezi, wawe wanazalisha umeme au hapana. Hivyo, tunakopa dola milioni 43.8 ambazo tunatakiwa kulipa pamoja na riba, lakini wakati huohuo, tunamlipa dola milioni 2.5 kwa kitu kilekile ambacho tunakopea fedha, hata kama hiyo kampuni haizalishi hicho kitu. Huku ndiko kuhujumu uchumi na kuwatia wananchi kilema cha umasikini. Hii ni biashara kichaa.

Anyway, tuendelee, Mei 9, 2006 Benki ya dunia WB ilitoa Press Release Washington kuwa iliikopesha Serikali ya Tanzania dola za Kimarekani Milioni 200 kwa ajili ya mpango wa kuondoa umasikini wa (Mkukuta). Serikali imetoa dola milioni 25 ambazo ni sawa na wastani wa Tshilingi bilioni 25 na kuziita fedha za Kikwete. Zilizobaki, yaani dola milioni 175 wanafanyia shangwe. Juzi tumesoma ripoti magazetini kuwa matumizi ya Ikulu yamekuwa mara mbili ya bajeti yake kwa kipindi ambacho hata mwaka haujaisha. Ripoti ya Mkaguzi mkuu wa Serikali ndio kwanza imetoka, hatujuhi mauzauza yaliyomo ndani. Nimesoma habari kuwa Raisi wetu alikuwa Zanzibar anafanya matanuzi hotelini. Kuna dosari gani na utamaduni aliouanzisha Nyerere na Sokoine wa Viongozi wetu wa kitaifa kufikia Ikulu ndogo?

Hata zile dola milioni 25 (maalufu kwa fedha za Kikwete), tunawakopesha watu kufanya miradi midogomidogo ya kuuza vitumbua, maandazi, maji ya miwa, na bamia sokoni (Refer; Waraka wa Mtei). Huwezi kurudisha dola milioni 200 + Fees + Riba kutoka katika miradi ya kuuza Sambusa, tena kwa fedha za madafu. Dola milioni 175, wanafanyia party, posho wakati wa vikao vya viongozi, na safari za nje zisizoisha. Kila unayemuuliza, anasema Tanzania watu wanafedha bwana! Lakini hatujiulizi fedha zinatoka wapi? Wananchi wanafurahia fedha za Kikwete, lakini hawajuhi kuwa watatakiwa kuzilipa hizi fedha mpaka jasho la ‘kamshange” liwatoke.

Kama umasikini ungekuwa unaondolewa kwa kukopa fedha, basi wananchi wetu wangekuwa matajiri. Mfano, Septemba 8, 2005 Benki ya dunia ilitoa Press Release Washington, kuwa imeikopesha Tanzania dola za Kimarekani Milioni 150 kwa ajili ya (Mkukuta). Hata kabla ya hapo, Julai 30, 2004 benki ya dunia iliikopesha serikali ya Tanzania dola za Kimarekani Milioni 60 (Poverty Reduction Support). Mei 29, 2003, Benki ya Dunia ilitoa Press release kuwa imeikopesha Tanzania dola za Kimarekani Milioni 100 (Poverty Reduction Supporty). Viongozi wetu wanakopa fedha kwa mgongo wa umasikini, alafu wanaishia kuzifuja.

Pamoja na mikopo yote hiyo, mbona umasikini miongoni mwa watu wetu unazidi kuongezeka? Mkukuta kwanza si Sera yetu, bali ni matokeo ya vikao vya mataifa makubwa, ambayo imechomekwa ndani ya mpango wa Umoja wa Mataifa kinyemela, kwa kusimamiwa na wajuba wa IMF na WB. Hivyo Sera zinazoongoza nchi yetu zinatoka nje. Ndio maana viongozi wetu wanatalii, kwasababu sera zinaagizwa nje kama bidhaa. Siku hizi sera imekuwa bidhaa, inaagizwa nje. Si biashara soko huria. Kumbuka Nyerere na Sokoine, walikuwa na mpango wa kuondoa umasikini ambao uliwashirikisha watanzania wote. Mfano, walitambua umuhimu wa kuwapa watu wote elimu kwa kumtokomeza adui ujinga. Hawakukaa Paris, Rome, au Washington, bali walikaa Musoma na kuja na Azimio la Musoma-Elimu.

Azimio la Musoma, linajulikana kwa matendo kuliko maneno, kwa maana kwamba, msisitizo uliwekwa katika Elimu kwa wote. Mkazo ulilenga kukuza maarifa ya ufundi na Sayansi. Pia, elimu na kazi vilitakiwa kwenda pamoja. Pamoja na matatizo yote tuliyoyapata miaka ya sabini, hata tukapigana vita na Nduli Amin, ambayo kwa kiasi kikubwa tuliigharamia sisi wenyewe, bado tuliweza kuwapeleka watoto wetu shule, tukawanunulia vitabu, Madaftari ya majaribio, vifaa vya Mahabara, Chaki za kufundishia, na chakula ili wapate lishe bora wasije wakashindwa mitihani kwa kusingizia njaa. Tuliwalipia nauli (unakumbuka TMO?). Nchi yetu ilikuwa mfano wa kuigwa, kwa maana kwamba tunaweza kupigana vita wakati huohuo tukawapeleka watoto wetu shule kwa kuwafanyia yote niliyoyaeleza. Wamarekani pamoja na utajiri wao, wanatoka makamasi. Hawawezi kuwafanyia raia wao kama tulivyofanya wakati wa vita.

IMF na WB walitushauri tupunguze bajeti za mipango mashuleni ambayo kwa mitizamo yao ilikuwa haitusaidii sisi watanzania. Walisema sisi ni masikini hivyo, hatuwezi kuwalipia shule watu watu. Viongozi wetu walisalimu amri. Wakaacha kuwalipia watu shule, wakapiga kwanja masomo ya ufundi, na kusitisha masomo ya michezo, kwa kuondoa mashindano ya michezo mashuleni. Eti wanadai Umiseta ni gharama. Ni gharama gani? Vijana walikuwa wanakula Ugali na Maharage wakati wa mashindano ya mashule. Walikuwa wanalala kwenye madarasa ya mashule ambapo mashindano hayo yalikuwa yanafanyikia. Kwani walitakiwa kupelekwa Brazil kwa mazoezi? Uliwahi kusikia wanafunzi wa umiseta wanataka kulala mahotelini?

Lakini IMF na WB, wanazunguka nyuma na kutukopesha fedha za kuwalipa makocha wa timu ya taifa, timu ya taifa ya vijana, na eti daktari wa viungo wa timu ya taifa. Eti hizo sio gharama. Mishara ya hawa waheshimiwa watatu kwa mwezi, ni tosha kuandaa mashindano ya umiseta kwa miaka kumi. Tunasahau kuwa mipango ya michezo mashuleni iliwanufaisha wote na sio kundi la wapenda soka tu. Miongoni mwa walionufaika ni wasichana, wavulana, vilema, wanariadha, wanakambumbu, mipira ya nyavu, tenesi, vikapu, karate, kuruka vihunzi, kwaya, michezo ya alaiki, na mengineyo. In fact, hii michezo ilikuwa inadumisha utamaduni wetu, na kujenga uzalendo miongoni mwa vijana. Sasa hivi tumewatenga wote hawa, kana kwamba sio sehemu ya jamii. Tumebweteka kushangilia ujinga wa kukopa fedha kwa ajili ya kuneemesha familia za wabraziri. Eti huku ndiko kupenda michezo.

Hata haya hatuna, tunasema Nyerere na Sokoine hawakupenda michezo. Tumesahau busara za wahenga kuwa Samaki mkunje angali mbichi. Kwasababu ya ulimbukeni, bado tunamstahi kocha kutoka Brazil, lakini kwasababu pia nchi yetu imejengwa na mashabiki wengi wa mpira kuliko walivyo wapenzi wa mpira, tukipata vipigo vingine huko mbeleni (kitu ambacho kitatokea), tutaanza kuchapana makonde wenyewe kwa wenyewe, na kusahau hii misifa kemkem tunayowamwagia viongozi wetu wanaotumia njia ya mkato kuiangamiza michezo nchini kwetu. Hata tukichapana makonde, tusisahau kuwa tutatakiwa kulipa hii mikopo.

Nyerere na Sokoine, walitumia fedha za misaada kujenga viwanda na kuanzisha mashirika ya Umma. Pamoja na kazi hiyo iliyowakabili, hawakusitisha huduma za jamii. Zilijengwa dispensari vijijini, na zilikuwa na madawa. Watoto walisoma wakiwa na siha na afya njema. Siku hizi pamoja na mabilioni tunayokopa, hatujengi viwanda, hatuanzishi mashirika ya Umma, hatuwezi kuwasomesha watoto wetu, na Hospitali zetu hazina madawa. Fedha hizo zinakwenda wapi? Mzee Mkandara juzi ameandika ujumbe kutoka Tanzania kuwa watu wanafedha kichizi. Angalia mabangaloo, maghorofa, twin tower, magari, na nguo wanazovaa viongozi na familia zao. Eti hayo ndio maendeleo. Toka lini maendeleo yakalenga vitu badala ya watu? Eti majengo, wakati ndani hakuna umeme na maji ya kunywa, au ya kutumia msalani. Huko ndiko fedha tunazokopa zinapoishia. Nasema zamani tulikopa fedha kujenga viwanda, lakini sasa hivi tunakopa fedha kubinafsisha hivyo viwanda.

December 15, 1999 benki ya dunia ilitoa press release kuwa imeikopesha serikali ya Tanzania dola za Kimarekani milioni 45.9 (Privatization and Private Sector Development Project). Yaani tulikopa fedha kubinafsi mashirika kama Shirika la ndege, ATC. Juzi huyu marehemu wetu ATC, amerudishwa mikononi mwa serikali. Hata hivyo, kitendo hicho hakisamei deni. Tutatakiwa kulipa fedha tulizokopa kwa ajili ya kulibinafshisha hilo shirika, hata kama ubinafshishaji wake umeshindikana. Yaani hasara juu ya hasara. Tuliijenga benki ya taifa ya biashara bila kutumia mikopo, lakini tumekopa fedha kuiuza. Mimi nadhani unapouza kitu, unapata faida, sasa kwa nini ukope fedha ili kuuza kitu, tena kwa bei ya kuokota? Huwezi kudharau mapambano aliyoyaongoza Sokoine ya vita dhidi ya wahujumu Uchumi. Uchumi wetu sasa hivi unahujumiwa na Magenge ya viongozi, wakishirikiana na makampuni makubwa ya kimataifa, chini ya usimamizi wa IMF na WB.

Mei 28, 2003 Benki ya dunia ilitoa press release kuwa imeikopesha Tanzania dola za Kimarekani Milioni 61.50 (Dar Es Salaam Water Supply and Sanitation Project). Shirika la Oxfam international, lilibaini kuwa mkopo tuliopewa, unafanana na ule waliopewa Ghana na hiyohiyo benki ya dunia kwa masharti ya kubinafsisha sekta ya maji (Refer: Oxfam international submission to world Bank review of conditionality, May 2005). Wote tunajua kilichotokea. Tulitapeliwa, lakini wananchi wanatakiwa kulipa hizi fedha, riba, pamoja na fees. (hii nitaielezea kwa undani zaidi wakati nachambua tofauti kati ya Lowasa na Sokoine).

Waghana waliingia mitaani kupinga ubinafsishaji wa sekta ya maji uliosimamiwa na benki ya dunia kwa kuanzisha taasisi za wananchi kama National cap of water in Ghana. (Refer: Privatization tidal wave IMF/World Bank water policies and the price paid by the poor – by Sara Grusky). Sisi wabongo tumelala fofofo, huku viongozi wetu wanagawana fedha na makampuni ya kitapeli, alafu baadae, eti wanayafukuza hayo makampuni nchini ili kufuta ushahidi. Tunasema huko ndiko kuchapa kazi, na tunawapandisha vyeo. Kila siku tunasoma habari za jinsi watu wanavyotaabika na maji pale Dar-es Salaam, hasa akina mama na watoto.

Wanasema sikio la kufa halisikii dawa. February 13, 2007, Benki ya dunia imetoa press release kuwa imeikopesha serikali ya Tanzania dola za kimarekani milioni 200 kwa ajili ya (Water sector Support Project). (File attached). Tunarudi palepale. Sasa badala ya Net Group, sijuhi nani atapewa hizi dola milioni 200, alafu akafukuzwa kwa mikwara isiyokuwa na kichwa wala miguu.

Mashirika mengi ya kimataifa yamepiga kelele kuwa kwa kipindi kifupi kuanzia mwaka 2005 mpaka 2007 mwanzoni, deni la nchi yetu Tanzania, limekwisha fika pale tulipokuwa kabla ya kusamehewa madeni. Hata wabunge katika kikao kilichopita, wamelalamikia kasi ya ongezeko la deni la taifa. Mikopo karibu yote tunayoikopa, hakuna fedha zinazokwenda ku-generate hard cash. Tutazirudisha vipi hizo fedha? Kwa miaka miwili na robo, tumekopa kiasi cha fedha kinacholingana na fedha tulizokopa toka tupate Uhuru mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2004.

Mimi nilitegemea mikopo yetu yote iwe katika sekta zinazo-generate hard cash. Mathalani, Agricultural Sector Development Projects. Lakini tunakopa kulipa posho na mauzauza mengine ya kuimalisha miundo. Mfano, May 15, 2006 benki ya dunia ilitukopesha dola za Kimarekani Milioni 15 (Finacial Sector Project). Hii ni fedha inaishia kwenye matumbo ya watu. Tutazirudisha vipi hizi fedha? Mfano mwingine, Juni 15, 2006 benki ya dunia ilitukopesha dola za Kimarekani Milioni 98 (Local Government Support Project), Januari 24, 2006 Benki ya dunia ilitukopesha dola za Kimarekani Milioni 184.02 (East Afrika Trade and Transport Facilitation Project). Kila mkopo hapo juu unajitegemea. Kadiri ya Benki ya dunia, makubaliano ya kila mkopo niliyoiongelea hapo juu ni pamoja na ada ya uazimaji (commitment fee) asilimia 0.35, gharama ya kuhudumia mkopo (service charge) asilimia 0.75 kwa kipindi chote cha miaka 40 ya ukomavu (maturity) na kipindi cha madahiro (grace period) cha miaka 10. Hivi ni viwango vya Jumuia ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA).
 
Ukipata muda, unaweza pitia baadhi ya files hapo chini
 

Attachments

  • Water Privatization Tidal Wave by Multinational Monitor.pdf
    38.2 KB · Views: 128
  • World Bank and Oxfam.pdf
    64.4 KB · Views: 113
  • Water Source Project.pdf
    16.5 KB · Views: 96
Back
Top Bottom