Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Family friend wangu mmoja ambaye alikuwa waziri ktk awamu ya kwanza na ya pili amenisimulia visa vifuatavyo kuhusu Marehemu Sokoine;

Anasema Marehemu Mwalimu Nyerere alikuwa na tabia kuna siku akifanya kazi sana asubuhi mchana akienda lunch huwa analala kidogo kabla hajarudi Ikulu kuendelea na kazi. Kuna siku ilitokea dharura ya kikazi na Marehemu Sokoine akiwa ni PM alitaka maelekezo ya Mwalimu. Akapiga siku akaambiwa Mwalimu kapumzika kidogo, akasema muamsheni, Mwalimu akaamshwa tatizo likatatuliwa.

Anaendelea kusema huyu Bwana alikuwa mfuatiliaji SANA ktk utendaji wa kazi, alinipa mfano Sokoine alipokuwa PM alimwita waziri wa ulinzi ampe update ya silaha zilizopo katika makambi mbalimbali ya jeshi. Siku ya pili bila waziri kujua, Sokoine akawa anapiga simu kwa wakuu wa vikosi mwenyewe wampe data kazi ambayo imemchukua siku moja tu. Baada ya wiki 2 waziri anakuja na "update" yake na anakuta tayari mwenzie anayo na la kushangaza iliyo sahihi zaidi!

He was true leader, big loss to the nation.

sounds like mrema hivi[enzi zake serikalini].....ila wanatofautiana sana katika baadhi ya mambo!
 
Mrema alipoanza kushika madaraka baada ya kutoka kule usalama, alianza kama sokoine, tatizo la Mrema anamatatizo kidogo.

Nadhani ni ile Ajali ya kichwa aliyopata zamani...
Maana vikimchachia mmmmmmmh...!!
 
Tunaye Sokoine aliye Hai- EL, kijana, mchapakazi, mmasai. Anajua kutoa maagizo na kufuatilia. Huchukia mambo yakienda vibaya. Si unaona anavyosimamia ujenzi wa madarasa?

dada asha ,sokoine tunayemuongelea hapa alikuwa mwanamapinduzi mjamaa wa imani na vitendo,hakupenda utajiri wala kujilimbikizia mali,kama alivyokuwa mwalimu....

wakati damu ya kijamaa ikiwasha kwenye damu zetu kulikuwa na viongozi kama kingunge ngombale mwiru ambao nae tlimuona kama mjamaa wa kiimani na mfano alikini wameshindwa kuhimili utandawazi ,na sasa wamekuwa makuwadi wa soko huria..

lowassa anaweza kuwa na sifa nyingi kama za sokoine bahati mbaya amekosa zile sifa za msingi za marehemu sokoine..na kufanya wasifanane kabisa!!!!!!!!!!!

katika historia ya taifa hili viongozi walioweza kuvutia hisia za watu hadi wa vijijini ni,mwalimu nyerere,moringe sokoine ,augustine mrema[wakati ule],..jakaya kikwete these comes down in history as populist and charismatic leaders in tanzania...viongozi wenye vipawa hivi kwa wakati wao wamekuwa ma influence kubwa ..tatizo kwa jk kadiri anavyokaa madarakani ile charisma nayo inaendelea kupungua
 
sokoine ,mrema and lowassa kiutendaji same but ,true is far much better kumfananisha sokoine na mrema zaidi kuliko na lowassa.....
 
naweza kukubali hilo.. ila Lowassa huko aliko nadhani itabidi ashike kichwa ajiulize.. hivi yeye ataitwa "mtu wa watu"?
 
1938 Born in Monduli, Tanzania

1948-1958 Primary and Secondary Education, Monduli and Umbwe

1961 Joined Tanganyika African National Union (TANU)

1962-1963 Took studies in Administration, Federal Republic of Germany

1963 District Executive Officer, Masai District

1965 Elected to the National Assembly - Member of Parliament for Masai Constituency

1967 Deputy Minister of Communication, Transportation and Labour

1970 Minister of State, Vice President’s Office

1972 Minister of Defence and National Service

1975 Elected to the National Assembly - Member of Parliament for Monduli

1977 Member of the Central Committee of the ruling party Chama Cha Mapinduzi (CCM)

1977 - 1981 Prime Minister of the United Republic of Tanzania

1983-1984 Prime Minister for the second time

1984 April Passed away in a tragic car accident

Kutokana na wasifu na utendaji wake kazi nathubutu kusema kuwa shule si kipimo cha uteandaji, Moringe alikuwa na shule ndogo lakini aliwatingisha na kuwanyima usingizi watu waliokwenda shule.

daima tutamkumbuka sokoine
 
Kutokana na wasifu na utendaji wake kazi nathubutu kusema kuwa shule si kipimo cha uteandaji, Moringe alikuwa na shule ndogo lakini aliwatingisha na kuwanyima usingizi watu waliokwenda shule.

daima tutamkumbuka sokoine


Shule inasaidia katika uwezo wa kuelewa na kujiuliza kuhusu mambo mbalimbali...lakini sio lazima shule imsaidie kila mtu.

Mimi pia nilikuwa yank sana wakati huyu Mhe Sokoine anatutoka duniani. Ila nimepata kusikia juu juu tu. Hebu naombeni kwa wale wenye kumbukumbu za Sokoine na waliokuwa na akili ya kuelewa wakati huo watuambie ni kipi alichokifanya ambacho mpaka leo kipo au kimeondolewa na Mwinyi au BWM au JK..?? Mfano, najua Mrema alileata sungusungu, alileta ile sera ya wafungwa na wananchi kutaja majambazi katika maeneo yao, alileta sera za siku 7 kutaka watu wajieleze n.k Sokoine tumkumbuke kwa sera ipi/zipi..??
 
Mzee Heshima mbele mkuu,

Lakini kumbe huyu mzee shule ilikuwa haipandi kabisaaa, duh! I mean ndio alikuwa babu kubwa na nini, lakini damn!

Ni lazima tuwakumbushe watoto wetu kuwa shule ni muhimu sana, mzee alifanya vitu vyake, heshima mbele, lakini huenda kwenye mapungufu yake shule ilichangia sana, maana kukamata wauza colgate ukawaacha kina wahujumu uchumi hasa kina Ravji na marafiki zao kina Rupia, huenda shule ilichangia,

Hakuna apoligies kwa kutokwenda shule, ni lazima tuende shule ili angalau kuwa viongozi safi, maana kuna kiongozi mmoja dizaini ya Sokoine, anaitwa Kaisi, akiwa RC Bukoba alimuweka ndani Barongo, na akajaribu kumkamata Kahama, lakini Mwalimu akaingilia kati, alisema hawa na Singa singa mmoja kule Bukoba akiitwa Kugisi ndio wahujumu wa Bukoba namba moja, hakunyanyasa wauza Colgate,

Wote tuna mapungufu, lakini ya huyu mzee wetu mengi yalilkuwa matokeo ya kitabu kidogo!
 
Wazee, heshima yenu kwanza,

Mimi natofautiana na nadhalia ya kumfananisha Moringe Sokoine na Ngonyani Lowasa au Lyatonga Mrema. Sokoine alikuwa na sifa ya Uongozi, kwa maana ya kudhamilia kuonyesha njia. Pia, alikuwa ni mfanyakazi mwenye juhudi na maarifa. Dhamila ya Sokoine ilikuwa haimsuti katika utendaji wake wa kazi, ndio maana alifanikiwa kuthubutu kupunguza kero zilizowasibu watanzania. Mrema na Lowasa hawana sifa ya Uongozi, bali wana sifa ya kutawala. Pia, Mrema na Lowasa hawana sifa ya kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, bali wana sifa ya kushughulika. Dhamila zao wote wawili zinawasuta katika utendaji wao wa kazi, ndio maana hawawezi kufanikiwa, sio tu kupunguza, bali hata kugusa kero zinazowasumbua watanzania.

Lowasa na Sokoine wanafanana katika mantiki ya kuwa wote wameshika cheo cha uwaziri mkuu, lakini tofauti ni kuwa Sokoine alikitumia hicho cheo kuongoza watanzania, na Lowasa anakitumia hicho cheo kutawala watanzania. Katika michango yangu ya nyuma, nilikwisha elezea kwa kinaga ubaga tofauti kati ya cheo na uongozi, kwa maana ya kuwa uongozi si cheo, na cheo si uongozi. Hii ndio tofauti ya msingi kati ya ndugu yetu marehemu Moringe Sokoine ambaye aliunganisha cheo na uongozi katika nafsi yake, na kiongozi wetu mheshimiwa Ngonyani Lowasa ambaye amepata cheo cha uwaziri mkuu. Ili tuwajue hawa viongozi watatu, lazima pia tufahamu tofauti kati ya shughuli na kazi. Shughuli si kazi, na wala kazi si shughuli.

Kwa sababu nina mengi ya kuongea kuhusu Lowasa, naona nimuweke kiporo kwa leo, na nianze na tofauti kati ya Mrema na Sokoine. Mwaka 1973, nchi yetu ilikumbwa (off-guard) na ongezeko la bei ya mafuta ya petroli duniani. Hii iliathili ubadilishaji wa fedha ya kigeni. Mwaka huo huo mpaka 1974, tulikumbwa na ukame usio na kikomo, hivyo kusababisha upungufu wa chakula. Sukari, Mahindi, Unga wa ngano, na vifaa vya ujenzi ka simenti, na mabati vilikuwa hadimu. Serikali ililazimika kuingilia mgao wa chakula pamoja na mafuta ya Petroli kwa kutoa vibali kwa wale waliotaka kununua ili kulinda wananchi waliokuwa hawana uwezo wa kuchuana.

Tulichechemea mpaka mwaka 1977 wakati jumuia ya nchi za Afrika ya Mashariki ilipovunjika. Serikali ililazimika kutumia fedha ili kugharamia huduma ambazo mwanzoni zilikuwa zinatolewa na jumuia. Kumwaga tindikali kwenye kidonda, mwaka 1978 tukajiingiza kwenye vita dhidi ya Idi Amin. Kwa kiasi kikubwa, ile vita tuliigharamia sisi wenyewe bila ya fedha za mikopo. Resources zote zilienda kwenye vita, hivyo, uhaba wa kweli wa bidhaa ukaifadhaisha nchi yetu (kumbuka Sembe ya njano kwa foreni).

Tatizo kubwa lililozaliwa ni baadhi ya maafisa watendaji wa serikali katika ngazi za mikoa na wilaya, kutumia udhaifu wa uhaba wa bidhaa kwa kujilimbikizia mali. Mtindo waliotumia ulikuwa ni rushwa, kwa maana ya watendaji kuongwa na wafanya biashara ili wapewe vibali vya kulangua bidhaa zote hadimu katika bei ya serikali, na kuzificha hizo bidhaa mpaka kipindi fulani, alafu wanakuja kuziuza kwa bei ya magendo na kupata faida maradufu, wakati wananchi wakiteseka. Wafanyabiashara walipata faida isiyo kifani, na watendaji wa serikali walipata hongo kutokana na kuwauzia vibali walanguzi. Sokoine alikuwa kiongozi wa kwanza kustukia hiyo janja ya watendaji wa serikali walioshirikiana na walanguzi.

Sokoine alitoa matamko kuwa katika hali ya uchumi tuliokuwa nayo, mkate wa umasikini ilibidi ugawanywe kwa wote. Alisema, watu wanaolangua bidhaa zote na kuzificha kwapani, alafu wananchi wakiuliza tatizo ni nini wenyewe wanasema eti hali ya uchumi ni mbaya, lazima wasakwe mijini na vijijini. Akaimarisha jeshi la polisi ili liweze kupambana na hiyo tabia. Ili watu wanaojihusisha na vitendo hivyo wapate adhabu kali, akaliomba bunge kupitisha muswada kwamba wale wanaouza vibali na kulangua bidhaa hadimu wapatikane na hatia ya kuhujumu uchumi badala ya kosa la kula rushwa. Akaifanya iwe kampeni ya kitaifa.

Niliwahi kusoma paper ya Maliyamkono T. na Bagachwa, M.S.D (1990) ambayo haikumuongelea Sokoine lakini iliyoonyesha dhamila ya serikali ya kupambana na wahujumu uchumi. Inaonyesha idadi ya watu toka mwaka 1980 mpaka 1983 waliokamatwa, fikishwa mahakamani, na kufungwa jela baada ya kupatikana na hatia. Kwa Sokoine, hii haikuwa shughuli, bali ilikuwa ni kazi, kwa maana kuwa aliona kero, akaimarisha taasisi ya jeshi la polisi kwa kuiwekea mazingira ya kisheria baada ya kupata kibali kutoka katika taasisi ya bunge.

Kazi ya waziri au waziri mkuu ni kuimarisha taasisi zote anazoziongoza. Mwalimu aliwahi kusema kuwa, nchi inaongozwa na sheria. Watu lazima wajue kuwa sheria zimebadilika ili waweze kuzitii. Nchi haiongozwi na akili za mtu. Mambo ya kuona kiongozi anatoka kwenye vilabu vya pombe, au anaamka usingizini na kuanza kutoa hamri, au kufungia taasisi mbalimbali bila mpangilio, ni mishughuliko sio kazi.

Kifo cha Sokoine, kilikatisha watu huondo wa mechi kati yake na Msuya, ambapo mwamuzi alikuwa Nyerere na Kawawa. Sheria ya kuhujumu uchumi ilikuwa ni msumeno, na yeye hakuwa na hitilafu ya kuhofia. Inasemekana vijana wenye Land lover zilizokuwa ma matunubali walionekana nje ya nyumba ya Msuya. Waliulizwa wamepata wapi mamlaka ya kumpekua waziri, lakini vijana walimuonyesha kibali cha kufanya upekuzi. Inadaiwa Kawawa ndiye aliwaondoa vijana nyumbani kwa Msuya, kitendo kilichomuhudhi Sokoine. Nyerere alimwambia Moringe kuwa mambo mengine yanahiyaji tuyafanye taratibu, na Moringe akamjibu kuwa sheria lazima zichukuwe mkondo wake. Alisema kama tunaamua kuwa wajamaa, basi iwe hivyo, vinginevyo tufatute sera zingine.

Sokoine hakutumia vyombo vya habari kutangaza aliyokuwa akifanya. Tena mambo yake mengi yalikuwa hayatangazwi mpaka alipokufa.


Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani aliongoza vyombo vilivyopashwa kusimamia haki, sheria, usalama wa raia na mali zao. Hata hivyo, kipindi cha uangalizi wake, tulishuhudia utawala uliokiuka misingi ya sheria, usio tenda haki, na ulioshindwa kusimamia usalama wa raia. Badala ya kuimarisha taasisi ya jeshi la polisi, alitoa amri za kuwalazimisha raia kulala nje wakiliwa na mbu eti wanajilinda pamoja na mali zao kwa mtindo wa jadi wa Sungusungu. Polisi walibaki maofisini wakila rushwa, kulinda wahalifu waliohujumu nchi yetu, na kuota vitambi. Raia walikuwa na nondo, majembe, mapanga, visu vya jikoni, uma na vijiko, bila hata kupata mafunzo ya aina yoyote, wakingoja usiku kucha kupambana na majangiri yenye bunduki za SMG. Kwa Mrema, eti huo ndio ulikuwa usalama wa raia na mali zao. Watu wanasema huko ndiko kuchapa kazi kwa Waziri wa mambo ya ndani.

Mwaka 1993, chini ya uangalizi wake, Paspoti mpya za Tanzania 10,000 zilipotea wakati zinakabidhiwa wizara ya mambo ya nje kutoka uhamiaji (gazeti la Uhuru januari , 14 1993). Hapakuwepo na uzembe, bali vilikuwa ni vitendo vya rushwa ambavyo vilipelekea taifa kupata fedhea kwani hizo paspoti ziliangukia mikononi mwa raia wa Somalia na wale wabeba madawa ya kulevya. Hakuna aliyekamatwa. Packets 2,000 za madawa ya kulevya ‘Mandrax” ziliyeyuka zikiwa chini ya uangalizi wa polisi (Uhuru Januari 7 1994), Kilometa za mraba 4666 ziliuzwa kwa msukumo wa rushwa (Mfanyakazi januari 20 1993). Kila siku ya Mungu, magazeti yalikuwa yakiandika wizi upolaji wa mali ya Umma, na vitendo vya rushwa, huku Mrema akinguruma kutisha raia wasiokuwa na hatia kwa kutumia vyombo vya dola. Matukio yote makubwa yaliandikwa na kupita bila kumkamata mtu.

Sasa hivi mambo ya kuhujumu uchumi ni ya kawaida, lakini kipindi cha uwaziri wa mambo ya ndani wa Mrema, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, uchumi wa nchi ulikuwa unahujumiwa chini ya uangalizi wake. Yeye ndiye alipalilia msamiati wa vigogo, alipojifanya polisi pale airport kwa kuingilia mali za wakubwa zikiwa zinatoloshwa nje ya nchi. Kwake yeye, sheria zilibagua vigogo na hazikutakiwa kuchukua mkondo wake. Hata wakati sheria zilipobadilishwa ili kuruhusu mfumo wa vyama vingi, aliongoza vyombo vya dola kuwapiga mabomu ya machozi viongozi wote wa vyama vya upinzani. Aliwanyima haki ya msingi ya kuhutubia wananchi kwa kuwakatalia vibali vya mikutano. Majuzi wakati anahojiwa na Radio Butiama, akasema alifanya hivyo kwasababu alikuwa akimtumikia kafili, lakini hakusema mradi wake alioupata ulikuwa ni upi? Sokoine alikuwa hamtumikii kafili, bali aliwatumikia wananchi.

Aliyavalia njuga matokeo ya uhalifu kwa kujenga vituo vya polisi kila kona ya nchi, ili kuzuia vibaka na kuwaacha ‘vigogo’ ambao ni wezi wa kweli wakipeta. Badala ya kufanya kazi ya kuliwezesha jeshi la polisi kuwa na uwezo wa kuwakamata wahalifu wote ili wafikishwe mahakamani, akaanzisha utaratibu wa kutoa siku kumi kumi. Aligeuza ofisi na nyumbani kwake kilalacha kuwa kituo cha polisi, mahakama, na jela. Hakuna mhalifu hata mmoja aliyeitwa nyumbani au ofisini kwake, alafu akafikishwa mahakamani. Wizara zina miongozo, sheria pamoja na taratibu ambazo zinatakiwa kuheshimiwa na kiongozi yeyote. Alizinyamazisha taasisi za Mahakama na Polisi, badala yake hizi taasisi zikaanza kuwa mapango ya wala rushwa. Wahalifu walitakiwa kupelekwa polisi sio nyumbani kwa Waziri. Eti watu wanasema huku ndiko kuchapa kazi.

Akaanzisha tabia mbaya ya kulala uvunguni mwa vitanda vya wanandoa. Hizi ni busara alizokopa kutoka kwa mabibi wa kijadi waliokuwa wanataka kuhakikisha kama mke aliyeolewa na mjukuu wao ana bikira au la!. Waziri unamwita mke wa mtu ofisini kwako, tena kupitia kwenye vyombo vya habari? Kwa nini Waziri anaingilia ndoa za watu? Kwa nini asiimalishe taasisi zinazoshughulika na mambo ya jamii? Nchi inaporwa, vyombo vya dola vimewekwa kibindoni, Waziri anayeongoza taasisi zote hizo yuko ofisini na mke wa mtu akisuluhisha ugomvi wa makonde yatokanayo na wanandoa kunyimana uroda, au kufumaniana. Hizi zote ni shughuli na sio kazi.
Kwa nini Mrema alipata umaarufu wakati ule na sio sasa hivi?

Kila Mrema alipokwenda, alilakiwa na ‘umati mkubwa” wa watu ukiongozwa na kitengo cha umoja wa vijana, huku wakijivinjari na mapikipiki, bendera, pamoja na jezi zao za kijani na nyeusi. Ikasadikikika kuwa Mrema alikuwa na ‘mvuto wa watu”. Yote haya yalitangazwa kila siku na vyombo vya habari. Alipojiengua CCM, na kuamua kugombea uraisi mwaka 1995, matangazo ya Radio Tanzania na magazeti ya chama yalienguliwa pia. Mrema aliendeleza matangazo yake ya kuwa na mvuto wa watu kupitia kitengo cha vijana wa NCCR –Mageuzi.

Walitueleza kuwa Mrema alikuwa na mvuto wa watu kiasi cha kubebwa kila anapotokeza. Wengine walimlilia Mrema kama wafanyavyo wapenzi wa Michael Jackson. Matangazo mengine yalisema Mrema alikuwa njiani kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, lakini wakazi wa Dodoma wametembea kwa miguu kutoka Dodoma mpaka Chalinze ili kumpokea. Matangazo hayo yalionekana kuishawishi serikali kutumia vyombo vya dola ili kuzuia watu wasiende kupokea kipenzi chao. Hata hivyo, kinara wa mizengwe, Mwalimu Kambarage, aliona hiyo janja ya nyani na wakati akifungua kampeni za Mkapa pale Jangwani 1995, aliwaambia viongozi wa Serikali kuwa ‘Muacheni”. ‘Kama mtu anapenda sana kubebwa, na watu wa kumbeba wapo, hata wakipokezana maili kumi kumi kama jeneza, waacheni”.

Baadae Mrema alianza kuona haya, na mambo ya kubebwa bebwa yakayeyuka. Hakuwa na fedha wala ujanja wa kuendeleza matangazo yaliyokuwa yanavutia watu. Yeye hakuwa na sifa ambayo ingeendelea kuwapendeza, kuwashikilia na kuwavutia watu.

Kama mtu ana sifa fulani, mvuto wa watu unakuwepo hata kama matangazo yanakoma. Ni vema kutofautisha kati ya mvuto wa matangazo na mvuto wa sifa ambapo vyote viwili vinajenga mvuto wa watu. Matangazo yaligunduliwa ili kujaribu kuchukuwa nafasi ya sifa ambacho ni kiini katika mvuto wa watu. Hivyo basi, mvuto wa watu halisi sio sifa ya msimu kama ilivyo Kiangazi na Kipupwe, bali ni sifa ambayo mtu anakufa nayo kama Sokoine. Lakini hiyo sifa ikiwa ni matokeo ya kilemba cha ukoka kama ilivyokuwa kwa Mrema, ndipo inakuwa na tabia za msimu. Ndio maana amedolola kwa sasa.
 
Wazee, heshima yenu kwanza,

Kama mtu ana sifa fulani, mvuto wa watu unakuwepo hata kama matangazo yanakoma. Ni vema kutofautisha kati ya mvuto wa matangazo na mvuto wa sifa ambapo vyote viwili vinajenga mvuto wa watu. Matangazo yaligunduliwa ili kujaribu kuchukuwa nafasi ya sifa ambacho ni kiini katika mvuto wa watu. Hivyo basi, mvuto wa watu halisi sio sifa ya msimu kama ilivyo Kiangazi na Kipupwe, bali ni sifa ambayo mtu anakufa nayo kama Sokoine. Lakini hiyo sifa ikiwa ni matokeo ya kilemba cha ukoka kama ilivyokuwa kwa Mrema, ndipo inakuwa na tabia za msimu. Ndio maana amedolola kwa sasa.


Mzee Kyoma

Heshima yako. Maelezo mazuri yanayothibisha kuwa Mrema na Sokoine hawana ufanani hata kidogo. Mimi nimekubali mia kwa mia...katika hiyo ya "matangazo" naomba maoni yako kuhusu umaarufu alionao JK kwa sasa.

Pia, kwa jinsi ulivyomuelezea Sokoine na sifa zake kwa kuainisha tofauti kati ya kazi na shughuli, na pia cheo na uongozi....nashindwa kujua kwa mtazamo huo iwapo tuna kiongozi yoyote katika Tanzania ya leo.
 
Wazee, heshima yenu kwanza,

Akaanzisha tabia mbaya ya kulala uvunguni mwa vitanda vya wanandoa. Hizi ni busara alizokopa kutoka kwa mabibi wa kijadi waliokuwa wanataka kuhakikisha kama mke aliyeolewa na mjukuu wao ana bikira au la!. Waziri unamwita mke wa mtu ofisini kwako, tena kupitia kwenye vyombo vya habari? Kwa nini Waziri anaingilia ndoa za watu? Kwa nini asiimalishe taasisi zinazoshughulika na mambo ya jamii? Nchi inaporwa, vyombo vya dola vimewekwa kibindoni, Waziri anayeongoza taasisi zote hizo yuko ofisini na mke wa mtu akisuluhisha ugomvi wa makonde yatokanayo na wanandoa kunyimana uroda, au kufumaniana. Hizi zote ni shughuli na sio kazi.
Kwa nini Mrema alipata umaarufu wakati ule na sio sasa hivi?

NAUNGANA NA KYOMA NEITHER MREMA NOR LOWASSA COULD BE COMPARED BY SOKOINE, THEY R MILES APART! INDEED SOKOINE WAS BELONGING TO A DIFFERENT LEAGUE. MAY GOD REST HIS SOUL IN PEACE.
 
Kama huna sababu mhimu sana inayokuzuia kukusanya habari za marehemu Sokoine na kuziweka kwenye kitabu, basi inafaa ufikirie kuifanya kazi hiyo.
Sababu ya wewe kuwa mdogo wakati huo sio ya msingi. Si lazima uandike peke yako, lakini unaweza kuwa chachu na mshiriki imara kati ya kundi la watu kama akina Mawado mnaoweza kuendesha na kuifanikisha shughuli mhimu kama hiyo.
Baadhi ya matatizo yetu mara nyingi ni haya ya kutegeana. Kumsubiri mtu mwingine afanye.

Kalamu, heshima yako mkuu,

Naona unanichokoza kwa kunifanya nianze kuboronga mjadala huu wa Sokoine kwa kupenyeza mada nyingine ya utamaduni wa kuandika na kujisomea. Nakiri kuwa mjadala wa Sokoine utatusaidia kutafakari mambo mengine ya msingi kwa taifa letu ambayo naona ni bora baadae tukayaanzishia mada yake. Nakubaliana na hoja yako kuwa wale wanaomjua au waliofanya kazi na Sokoine hawawajibiki peke yao kuandika vitabu vinavyohusu historia yake. Huu ni wajibu wa kila mtanzania. Hoja yako ni muhimu sana kwasababu tumekuwa na kasumba ya kuamini kuwa Tanzania hakuna wasomaji wa vitabu. Dhana hii imewafanya waandishi wa kusadikika kulala usingizi mzito wa fofofo kwa kisingizio kuwa, hata wangeandika vitabu, hakuna ambaye angevisoma.

Hivyo, kwa mawazo yao, kuandika vitabu ni kupoteza muda, kwani havitasomwa, na badala yake vitaishia mitaani kufungia Chapati, Maandazi, na Balagala. Hata hivyo, wadadisi wanaamini kuwa nchi yetu ina wasomaji tele wa vitabu, lakini waandishi ndio haba. Mjadala huu, wa kutafuta visingizio vya kuhalalisha uvivu wa kuandika na kusoma, naufananisha na ule wa kuku na yai ni kipi kilianza. Hii ina maana kwamba, waandishi wanasubiri upatikanaji wa wasomaji ili waweze kuandika vitabu, wakati, wasomaji wa kusadikika nao wanasema wanasubiri vitabu viandikwe ili waweze kuvisoma.

Wengine wanadai kuwa vitabu vichache vilivyopo mitaani, vina lugha ya kiwango cha juu ndio maana vinatumika kama nyenzo huko msalani. Dawa ni kama ulivyosema, tuache tabia ya kutegeana. Kazi ya mwandishi ni kuandika na wala sio kuhofia uhaba wa wasomaji. Sijuhi hii hofu huwa inatoka wapi, kwani sijawahi kuona mwandishi mzuri ambaye si msomaji mzuri. Yawezekana tatizo la nchi yetu sio ukosefu wa wasomaji au waandishi, bali ni tatizo la mawasiliano baina ya kundi dogo la wasomi ambao wanatarajiwa kuwa waandishi, lakini wamefunzwa kwa lugha tofauti isiyoeleweka vema miongoni mwa kundi kubwa la jamii ya Tanzania linalo mudu lugha isiyo ya wasomi.

Tatizo hili limejumuishwa katika mfumo wetu wa elimu wa Kiswa-Nglish. Naona Mzee Mwanasiasa amegonga msumari kwenye mfupa kwa kuanzisha mada ya mfumo wa elimu, na mimi nimekwisha weka mawazo yangu huko. Wale wachache waliofanikiwa kupata elimu ya juu na kuongea lugha ya kisomi, kwa maana ya Kiingereza, wanapata kigugumizi kuelezea utaalamu wao kwa njia ya maandishi ambayo yataeleweka miongoni mwa watu waliowengi lakini waliachwa katika kituo cha Saranda na treni letu la mfumo wa elimu. Hawa waheshimiwa wanamudu lugha yao inayodhalauliwa na wasomi, kwa maana kuwa wasomi wakitumia lugha ya waliowengi ambao hawajasoma, wote wataonekana kundi moja, yaani hawakusoma.

Mathalani, majuzi tu, wakati wa sakata la Rada, Prof. Mwesiga Baregu pamoja na mdau mwenzetu Mzee Mwanakijiji walitoa mitizamo yao kuhusu mtafaruku mzima wa ununuzi wa Rada. Matamko yote mawili yako humu ukumbini na kila mmoja wetu anaweza kuyapitia kwa lengo la kuwianisha. Nilibahatika kuongea na ndugu yangu kijijini Kitendagulo, Bukoba, ambaye naye ni miongoni mwa wale walioachwa Saranda na treni letu la elimu. Niliduwaa alipoanza kunisimulia sakata zima la Rada kwa kinaga ubaga. Alinishauri nitafute makala ya mtu anaitwa Mwanakijiji kwani yeye ndipo alipopata hizo busara alizonimegea. Nilimwambia nilikwisha isoma.

Hata hivyo, ujumbe nilioupata, ni kuwa lugha aliyotumia Mwanakijiji imewafikia wengi walio vijijini na wakaelewa na kuthubutu hata kuwasimulia akina Kyoma kama vile bibi yangu alivyokuwa ananisimulia hadithi za kale. Lugha aliyotumia Prof. Mwesiga Baregu ni ya wachache, kwa maana ya wale wanojiita wasomi. Hivyo basi, naamini wasomaji wapo, ila daraja linalounganisha wasomaji na waandishi, ndilo linahitaji kufanyiwa ukarabati, kwa maana ya kuwa lugha tunayotumia kuandika iwe ni lugha ya waliowengi.

Ni nadra kuona mtadao unaosomwa na watu wengi wenye viwango tofauti vya uelewa, na wanaotoka katika matabaka tofauti kama Jambo forums. Inawezekana pia ipo mitandao mingine yenye wadau wengi, lakini angalia tofauti ya lugha inayotumika kwa kulinganisha na mitandao yenye wadau wachache. Nakumbuka vitabu vya James C. Vilikuwa vinasomwa na watu wachache katika shule za Sekondari, lakini vitabu vya Msiba, Willy Gamba, vilisomwa Sekondari, shule za msingi, maofisini, vijijini, na mijini. Msiba alichofanya ni kunukuu yale ya James lakini kwa lugha ya watu wengi.

Niliwahi kusoma makablasha ya uzazi wa mpango yaliyoandikwa na waganga wetu mjini Dar-es Salaam. Nia ya hiyo NGO ilikuwa kusambaza ujumbe kwa wanawake mijini na vijijini. Kibaya zaidi makablasha yaliandikwa kwa kimombo. Kana kwamba haitoshi, lugha yenyewe ilikuwa ni medical terms, ambayo kwa mawazo yangu, ilibidi iwe translated into plain language, hata kama kingekuwa kimombo kilekile. Kuna dosari gani kwa mfano kutumia neno ‘can’t get pregnant” badala ya neno ‘infertility”? au neno ‘stopping periods, change of life” badala ya neno ‘Menopause” au hata ‘period’ badala ya ‘Menses”.

Ukija kwenye masuala ya kijamii au siasa, utabaki hoi bin taaban. Angalia kitabu cha Mwalimu, The Influence of Nyerere, au kile cha Who votes in Tanzania, and why cha Maliamkono. Utajiuliza hivi walengwa ni akina nani? Lakini soma kitabu cha Mwalimu cha Uongozi na Hatima Yetu, ndipo utatambua kuwa tatizo letu sio wasomaji, au waandishi bali ni ubovu wa daraja linalounganisha wasomaji na waandishi.

Nyumbani tuna utamaduni wa kupenga makamasi kwa mikono, alafu tukikutana na mtu, tunasalimiana kwa kutumia mikono. Mtu anashika uchafu wa aina mbalimbali, alafu akirudi nyumbani kwa sababu ya uhaba wa maji, familia nzima wanatumia sufuria moja kunawa mikono kabla ya kula. Vijidudu vya kuleta magonjwa vinasambazwa kwa kila mwanafamilia. Vijijini vyombo vinaanikwa chini bila kuwekwa kwenye chanja, hivyo Konokono wanapata vitanda vya chee kwa ajili ya kujamihiana. Mtu analazwa hospitali kwa sababu ya Malaria, lakini anakufa kwa ugonjwa mwingine alioupatia pale pale hospitali kutokana na wadudu wanaoishi kwenye mazingira ya uchafu pale hospitalini.

Serikali ingetenga fedha za madafu, tena kidogo sana, tukawapa waganga wetu waliohitimu pale Muhimbili, wakaenda KIUTA na kutuchapishia vikablasha vidogovidogo vyenye lugha inayoongewa na wengi, kwa lengo la kutoa elimu kwa Umma. Tungeokoa maisha ya watu wetu waliowengi wanaokufa kwa magonjwa ya kuhara, kipindupindu, na mengine yanayofanana na hayo. Badala yake, Serikali inakwenda kukopa mabilioni ya dola ili kununua madawa. Hata hivyo, wajanja wanazitumia hizo fedha kununua madawa hewa, huku wakiacha watu wanateketea.

Umuhimu wa kujenga utamaduni wa kuandika na kujisomea bila visingizio visivyokuwa na kichwa wala miguu vya kutegeana, unaweza kutuepusha na majanga yanayotukabili sasa hivi. Wakati mwingine hatuhitaji mabilioni ya fedha za mikopo kutatua matatizo yetu, we only need twelve lines of an exercise book. Hivi ndivyo Waganda walivyofanya kugeuza kasi ya kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi. Uganda ilikuwa ni nchi ya kwanza duniani kufanya namba za maambukizo ya ukimwi duniani zianze kurudi nyuma. Yalikuwa ni mawasiliano ndani ya wanajamii kwa kutumia mistari kumi na miwili ya daftari la majaribio na sivinginevyo. Wazungu walipoona takwimu za Uganda zinaishangaza dunia, wakamwaga fedha kwa mabilioni. Nimesoma ripoti ya umoja wa mataifa ya mwaka jana, kuwa zile namba sasa zinayakimbiza mabilioni, kwa maana ya kwenda juu, na sio chini tena. Ukimwi umeanza kuenea kwa kasi kupiku idadi ya fedha zinazoingizwa.
 
Mzee Kyoma,

Hii shule yako imetulia sana, we have to put things as simple as possible to reach a wider circulation. Mimi nahisi tunahisia potofu kuwa kazi ya uandishi ikiwa complex ndio it counts a lots. Wenzetu walisema KISS= Keep It Simple St**idy!
 
Watu wengi wamejaribu kuandika jinsi marehemu Sokoine alivyokuwa na jinsi alivyofanya kazi lakini ni wachache sana hususani wale waliokuwepo kwenye ule msafara ambao wapo hai na wengine ambao walikuwa wanafanya kazi naye siku hadi siku.

Ni matusi makubwa kumlinganisha Sokoine na wezi (vibaka wa kutisha) waliotajwa na baadhi ya members. Nafikiri ni vizuri kukaa kimya kama huna cha kuchangia au usome kuliko kuibuka na ujinga ujinga ambao wengine wameonyesha kwenye hii mada. Utafika wakati mambo yake mengi yatawekwa hadharani ambayo yalikuwa ni ya kulisaidia taifa. MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI.
 
Back
Top Bottom