Kyoma:
Nashukuru kwa michango yako mizuri. Nashauri uihariri itoke kama makala kwenye magezeti ya nyumbani ili watanzania wengi zaidi waisome. hata kama utatumia pen name. Mazenge kwa mfuga mbwa kumeanza kubadilika. Kutabadilika zaidi kama utakuwa wakala wa mabadiliko unayotaka kuyaona. Najua unanielewa nikizungumza hii lugha ya kiubungo ubungo.
JJ
Mkandara: Muhimu, jamani tuzungumzie issue zinazotugusa leo hii. Usafiri wa dala dala (Vipanya) ni adhabu kubwa sana kwa nchi yetu yaani aibu kubwa!..
Tanzania leo hii ni mwendawazimu anayetembea uchi kama mbwa na ajabu watu wanahesabu idadi ya mijibwa inayokuja kujisuuza kisha tunafikiri wingi huo kama ni sababu ya ubora na uzuri wa jibwa hili Tanzania...
Kumbuka vizuri ile hadithi ya maisha ya mama yetu Tanzania... ukisha ichambua na kuelewa nini maana ya maelezo yale, hakika utakuwa umeelewa zaidi tofauti ya Viongozi wa leo hii na wale waliotangulia...
Ogah,
Shukran mzee mwenzangu, hiki kijiwe kimefika mahala ambapo sina uwezxo tena wa kuchangia mengi ila nitabakia nyuma hadi hapo nitakapo rudi mjini!... bado nafukuzana na kuku wa kuchinja. Internet cafe wizi mtupu, simu wizi mtupu na mengine mengi yasiyosemekana...