Tunamfukuza kazi JK kwa kudhoofisha uchumi ila twamwongezea Mahakama za kadhi na OIC.

Duh kuna watu wana hasira humu ndani! wakati ukienda mbali zaidi ukiwakuta wao kwa wao wanaanza tena kubaguana, mara ooh huyu kavaa suruali fupi...mara huyu ndefu...mara ooh huyu wakati anamuita sheitwani huwa anaelekea magharibi na mimi huwa naelekea mashariki hivo hatufanani!

Yaani Mafisadi kazi yao ni kuwapa vipande vidogovidogo ili muendelee kufarakana, Mkishtuka mnakuta nchi imeshabaki mashimo matupu!

Mchague Dr. Slaa Kwa Maendeleo ya Taifa!
 
Sawa!,lakini yakhe uzee unakusumbua.Una huruma sana na watu wasiostahiki kuhurumiwa kama vile mgombea fulani wa uraisi.

Mkuu nimejaribu kupitia baadhi ya thread zako nimeridhishwa na hasira ulizonazo, uko sahihi kabisa.....kila sehemu naona unajitahidi kwa nguvu zote kutetea kile kitu unachokiamini! Ushauri wangu wa bure kwako: si kila sehemu watu watakubaliana na itikadi yako, ukiingia kwenye siasa mambo yote ya dini kwa mujibu wa katiba ya JMT inabidi yaachwe nyuma!

Jf hapafai kabisa

Niwaonavyo wagombea watatu wa urais

Kumkosea heshima rais Kikwete

Udini ni nini?

Obama haogopi kuitwa muislamu

Aliyefungwa kwa baraghashia yu huru

Karibu mgeni wetu



Bakwata yaishtukia serikali
 
HUJAKOSEA, JAMAA KIBARUA BYE BYE.....!

ANGALIA JINSI UCHUMI ULIVYOKUFA TOKA ENZI ZA BEN MKAPA NA UTAWALA WA HUYU JK..AIBU!
---------------------------

AWAKATI WA MKAPA Vs KIKWETE!!

Unga 460 Vs 1000 = 217%
Mchele 600 Vs 1200 = 200%
Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
Mkate 250 Vs 700 = 280%
Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
Nazi 100 Vs 550 = 550%
Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%

unalipwa 100,000/-kwa mwezi kwa jedwali la hapo juu kila siku lazima
ununue unga robo 400, mchele nusu 300, uto kibaba 125, mafta taa
kipimo 300, sabuni nusu kipande 50, sukari robo 400, maharagwe robo
250, mkaa nusu kisado 300, nauli go & return 500, maji ya kunywa 500,
hapo ni bachalor kwa siku ni 3,125 mara 30 = 93,750 kwa mwezi. Okay
kodi kwa mwezi 20,000/- umeme 6000 kwa mwezi =total kwa mwezi ni
120,000/- je hiyo 20,000/- ziada katoa wapi????? ndo hizo mwisho wa
siku zina wapeleka jela au kuwanaachishwa kazi. Je maisha bora hapo
atoe wapi? Na je angekuwa na mtoto wa shule au watoto wawili? hapo
hajaumwa, hajatembelewa na mgeni akamnunulia soda, hajanunua nguo
nyingine!!!! Huyu mnaempigia kura hayajui hayo na hatambui kama una
familia kijijini pia. wao wanatibiwa na serikali, mafuta ya magari
kwao ni sawa na kumuuliza bibi akupigie story ya sungura. wenzie
wakitaka ongezo la mshahara wanajadiliwa in 2Hrs jibu tayari ila
waalimu na wenzao.........! 3 years.
 
Nyinyi na nani? Wewe si msemaji wa sisi waislamu ebo! Si wote ni mandondocha kama unavyofikiri....JK kafanya maisha yawe magumu kwa Waislamu na Wakristo na wasio dini...usilete uwongo hapa kwamba waislamu wote watampigia JK......

Halafu si kweli kwamba Waislamu wameburuzwa na Wakristo: kwa taarifa tu baba yangu ni shehe na mie nimesoma St Joseph Commercial School Tanga kwa msaada wa mastser, na nikaajiriwa nao mpaka nilipopata kazi nyingine....
Acha kutuweka kwenye kapu lako la uanafiki kwamba unaongea kwa ajili ya Waislamu....hatudanganyiki tena !

mkielezwa ukweli mnaanza kulalamika, ooh tunatukanwa! mmeshaambiwa serikali ya Tanzania Haina Udini kwa Mujibu wa Katiba ya Nchi! acheni kashfa, jadilini mambo yenye mwelekeo wa maendeleo ya Taifa letu!
 
Back
Top Bottom