Tunalaani kitendo cha Maafisa wa PCCB kutoa taarifa za ndani kwenye vyombo vya Habari.

Thomas Sankra Jr

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
418
128
Nalaani utovu wa nidhamu uliofanya na baadhi ya watumishi wasomi TAKUKURU.

Kitendo cha maafisa wa Taasisi hii nyeti ya kuzuia Rushwa, kutuo nyaraka za siri za ndani ni utovu wa nidhamu na ni vyema watafutwe, wakibainika waonywe na kuchukuliwa hatua ya kinidhamu. TAKUKURU ni moja ya Taasisi nyeti sana ya kupambana na rushwa inayoongozwa na sheria namba 11 ya mwaka 2007.. Leo katika Gazeti la Tanzania daima imetolewa barua ya ndani ya taasisi hiyo kuwazuia baadhi ya maafisa kwenda masomoni kwa mwaka 2016/2017. Kusoma ni haki ya kila mtumishi wa umma tena ni vyema kuwaendeleza watendaji wao katika dhana ya mapambano dhidi ya rushwa.

Lakini kitendo cha wao kutoa habari za ndani ya taasisi kilaaniwe na kila mtu, maana shaka yetu ni kutolewa kwa siri za watoa taarifa kwa taasisi hiyo, tuungane kulaani kitendo hicho. TAKUKURU ni taasisi pekee yenye wasomi wengi wenye ngazi zote za elimu kuanzia Cheti, Diploma, shahada ya kwanza, ya pili na ya tatu. Hivyo wasomi hawa kutoa siri za ndani ni utovu wa nidhamu ikizingatiwa wote wamepitia mafunzo ya kijeshi.
 
Wamefanyaje, wametoa taarifa gani za siri. Unapoandika jambo elezea kwa ufupi watu wengine wajue usidhani watu wanajua unachokijua.

Andika jambo lililokamilika.
 
Nalaani utovu wa nidhamu uliofanya na baadhi ya watumishi wasomi TAKUKURU.

Kitendo cha maafisa wa Taasisi hii nyeti ya kuzuia Rushwa, kutuo nyaraka za siri za ndani ni utovu wa nidhamu na ni vyema watafutwe, wakibainika waonywe na kuchukuliwa hatua ya kinidhamu. TAKUKURU ni moja ya Taasisi nyeti sana ya kupambana na rushwa inayoongozwa na sheria namba 11 ya mwaka 2007.. Leo katika Gazeti la Tanzania daima imetolewa barua ya ndani ya taasisi hiyo kuwazuia baadhi ya maafisa kwenda masomoni kwa mwaka 2016/2017. Kusoma ni haki ya kila mtumishi wa umma tena ni vyema kuwaendeleza watendaji wao katika dhana ya mapambano dhidi ya rushwa.

Lakini kitendo cha wao kutoa habari za ndani ya taasisi kilaaniwe na kila mtu, maana shaka yetu ni kutolewa kwa siri za watoa taarifa kwa taasisi hiyo, tuungane kulaani kitendo hicho. TAKUKURU ni taasisi pekee yenye wasomi wengi wenye ngazi zote za elimu kuanzia Cheti, Diploma, shahada ya kwanza, ya pili na ya tatu. Hivyo wasomi hawa kutoa siri za ndani ni utovu wa nidhamu ikizingatiwa wote wamepitia mafunzo ya kijeshi.
Mtoa barua tutamfuatilia tutamtumbua tu
 
Rais kasema hakuna haja ya kusomesha mfanyakazi wakati mtaani wenye degree zao ,ujuzi wapo.TCRA wanatumia mabilioni kusomesha
 
Mi nilifikiri Siri za Usalama wa Taifa letu kumbe hawa jamaa ambao kila siku wanapigwa chini Mahakamani kwa kukosa ushahidi.
 
Back
Top Bottom