Tunakusanya Kero ambazo ungependa zisemewe Bungeni na Nje ya Bunge na Viongozi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Kuna mambo manne tu ambayo watanzania ni lazima yafanyike ili kuikomboa nchi yenu katika kuondoa kero na kuleta hali nzuri kiuchumi kwa wananchi wenu.
1. Kupata Katiba iliyo bora.
a. Katiba yenye kulinda maslahi ya taifa lenu na kujali maslahi ya wananchi kwanza.
b. Katiba yenye kulinda rasilimali za Taifa lenu na kuzimilikisha kwa wananchi
c. Katiba itakayowafanya viongozi wote waliochaguliwa na wananchi waweze kuwajibika kwa wananchi na sio vyama vya siasa.
d. Katiba itakayoangalia uwezekano mkubwa wa kuinua hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja mpaka kwa taifa zima kwa kifupi katiba yenye utashi wa kujenga uchumi wenu na kuondoa utegemezi.

2. Wananchi kupenda kuwajibika katika kulijenga taifa lenu. Hapa panahitajika zaidi kujenga msukumo na tarbia yya wananchi kulipenda kwa dhati taifa lenu na kuwa na kiu ya maendeleo . Kuchukia rushwa na ubinafsi na kupenda kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yenu

3. Viongozi kuacha kutumia afisi za umma na madaraka katika kujilimbikizia mali binafsi. Hapa panatakiwa kuweka sheria kali kulidhibiti hili


4. Taifa kuwa na mtazamo wa kiuchumi zaidi na sio siasa. Kila kitu kinachohusi maslahi ya taifa ni lazima kitazamwe kimapana zaidi katika angle ya kiuchumi na si kisiasa

Mkifanikiwa kurejesha hayo juu basi pasi na shaka mtaanza kusonga mbele.

Kila la kheir

Tunaweza kuambulia chochote kwenye KATIBA yenu au unatupenda sisi tu?
 
Regia,

Kero zipo nyingi sana za kufanyiwa kazi, na utatuaji wa hizo kero ni ubunifu na mawazo sahihi kuondoa hizo kero.

Kwa watu wanaoishi vijijini, kwa wakati huu tunaokwenda nao wapo katika mashaka makubwa juu ya maisha yao pamoja na Ardhi yao wanayoishi. Kwa kiasi kikubwa rasilimali yetu tuliyonayo ardhini ndio inayochangia wananchi kunyanyaswa na kotolewa thamani ya ubinadamu, tuliangalie hili kwa unyenyekevu kwa hao wanaoteseka na waliokwisha teseka.

Vijiji vigeuzwe miji midogo midogo kwa ufanisi wa kuwapimia viwanja vya kujenga nyumba na hati miliki. Na wale wanaokaa mmoja mmoja wajumuishwe katika kijiji husika, na mashamba yanahitajika wapimiwe na wapate hati miliki, Ardhi Tanzania bado ni kubwa kuliko watu tunaoishi, bali mfumo wa ubadhilifu ndio unaoleta mashaka makubwa Tanzania. Kwa sababu mtu anaondolewa sehemu anayoishi eti sababu kuna
muwekezaji, na anakuwa ana haki yeyote na anakuwa ajui aendapo.

Kufanikisha, jitahidi kushirikiana na wasomi chuo Kikuu kitengo cha Ardhi watoe mchango wao katika hilo.
 
Dear Regia,

Nina kero kubwa mbili:
  1. Watendaji HAZINA na TRA kujipendelea kuibia wananchi: Kuna misamaha ya Import duty na excise duty kwa wafanyakazi wa serikali wanapoingiza magari toka nje. Bahati mbaya sana wafanyakazi wa TRA na HAZINA ndio pekee wanaopata exemption ya excise duty (labda na wengine wanaokubali kutoa rushwa). Kwa sasa haijulikani ni nani anapaswa kupata hiyo misamaha (vyote viwili au kimoja wapo) japo fomu inayojazwa hutamka vyote viwili. Pia kiwango cha hiyo exemption hakipo wazi kuwa ni kiasi gani. Bahati nzuri, TRA wanatoa orodha ya waliolipa na kiasi kwa miezi mitatu mitatu kwenye mtandao na unaweza kupakua hiza documents. Ukizichunguza, kuna waliopata msamaha wa vyote na wengine import duty yenyewe. Nimeangalia orodha ya Jan-March 2007 na kuona kuwa wengi waliopata vyote ni wa TRA na HAZINA. Wengine wengi ni import duty tu! Je hawa wanatuibia? Je, na wao kweli wanasubiri miaka minne ili kupata msamaha mwingine au wanafanya biashara ya kuwatolea watu magari kwa kukwepa ushuru?
  2. TRA haina kitengo cha kuelimisharaia??? Kwenye tovuti yao inaonyesha idara nzima ya elimu kwa raia lakini hakuna namna ya kuweza kuuliza (elecrtonically au kwa simu) pale unapoona unatendewa isivyo haki. Wananchi tulie na nani tunapopata matatizo na TRA? Hiyo page wakati wote haiko active na haijakamiika.
  3. VYUO VIKUU: Serikali imeingiza Siasa kwenye vyuo vikuu kwa kuwanyang'anya mabaraza ya vyuo uwezo wa kuajiri na kupeleka jukumu hilo kwa Katubu Mkuu Kiongozi. Hii inasababisha udhaifu ule ue wa Serikalini ambapo appointments zinategemea unamjua nani au utatunza maslahi ya nani. Matokeo yake ni vyuo kuoza kwa uzembe na incompetence kwenye leaderships, upendeleo kwenye appointments na kukomoana kama hukubaliani na Walanchi (case of Prof Baregu and Mlambiti). Tunaomba utaratibu wa awali wa Mabaraza ya Vyuo kuajiri urudishwe.
Nawasilisha
 
a) Kwakuwa Tanzania imejaliwa kuwa na rasilimali rasilimali lukuki kama madini, mali asili na ardhi safi, ni kwa nini imetajwa kuwa ni nchi ya tatu ikifuatia Iraq (iliyoathiriwa na vita) kwa kutegemea misaada hadi kufikia kuwa kero kwa nchi kama Uingereza hadi kufikia kubezwa kwenye vyombo vya habari?

b) Uchunguzi uliofanywa na nchi watoa misaada unaonyesha kuwa 20% ya fedha za misaada na za walipa kodi zinazoigia Hazina huenda kwa viongozi (wizi na ufisadi). Tunaomba tuhakikishiwe fedha hizo zitarudishwa lini maana wananchi wanahitaji zirudi mara moja ili zisaidie huduma za jamii na kupunguza umasikini nchini.
 
Dada Regia Hongera kwa wazo Zuri

1. Kwa sababu gharama za kuendesha serikali zinapanda siku hadi siku, kwa nini tuendelee kuongeza mikoa na wilaya?
2. Je ni lini katiba itaweka wazi idadi ya mawaziri na manaibu badala ya sasa raisi anajipangia namba akijisikia? Na kuongeza ukubwa wa bajeti na matumizi?
3. Je ni lini wizara ya Elimu itakiri kuwa imeshindwa zoezi zima la kusimamia Elimu Tanzania. Ni kosa kubwa sana kumwadhibu mtoto mwenye miaka kati ya kumi na kumi na tatu eti kaiba mtihani, huyu mtoto hana kazi, hana fedha, hana uwezo wa kujua hiyo mitihani inatungwa wapi kwa nini wasiadhibiwe wanaiba, vujisha, na sambaza? Na kwanini tusione kwamba zoezi la mitihani kutoka wizara ya elimu halina tija tena wala halimpimi mtoto?

4. Kwakuwa Wabunge wamewasaliti wananchi badala ya kuwatetea na kuwasidia ili serikali inawatumikie wanajitetea wenyewe na kujilimbikizia posho na mishahara minono huku wakikopeshana fedha kwa ajili ya magari ya kifahari na kusahau kutetea ujenzi wa taifa kwanini wananchi waendelee kuliamini bunge la sasa, Je kwanini wananchi wasipige kura ya maoni ya kutokuwa na imani na bunge tena.

5. Kwa sababu wabunge na viongozi wa serikali wameamua kutumia Hospitali ya appolo India na kwingineko nje ya nchi na kuacha Hospitali zetu hoi taabani huku serikali ikinyanyasa wauguzi na madaktari wanaotibu wananchi masikini katika hali duni, kuna haja gani ya kuendelea kulipa wabunge na watumishi wa ngazi za juu wa serikali wanaosababisha hali duni ya Hospitali zetu kwa sababu hawazitumii?

6. Je ni lini Viongozi watawajibika kwa lugha za kejeli na matusi dhidi ya wananchi?
 
Ragia

Bado naendelea.

[11] Jaji mkuu achaguliwe na majaji wa mahakama ya rufaa.Apigiwe kura na majaji wenzake.Jaji kiongozi achaguliwe na majaji wa mahakama kuu na atoke miongoni mwa majaji wa mahakama kuu.Iwepo bodi ya kuajiri majaji na mahakimu.

[12] Wabunge wawe na ukomo wa vipindi viwili au vitatu mwisho.Hii itaondoa wanasiasa aina ya Dr Mzindakaya au Jackson Makwete.

[13] Itungwe sheria ya kumfukuza mbunge / diwani aliyeshindwa kutimiza wajibu wake.Wapiga kura wakiorozesha majina na saini kwa idadi itakayokubaliwa kisheria mbunge au diwani anaweza kutimuliwa mara moja.
Namba 11 imekaa kisiasa zaidi kuliko kitaaluma. Tuige katiba ya jirani zetu KENYA tu namna wanavyompata JM wao.
 
Dada angu, naomba uulize hiki kituko cha serikali kutumia bilioni 64 kusheherekea miaka hamsin ya mateso ya umaskini Tz kina maana gani. Hzo pesa zmetolewa kutoka kwny bajeti ipi mloipitisha bungen?

Ilikua na mana gani kupoteza kias hcho chote cha pesa wakat, watumishi wa sekta za umma wakililia mishahara na malipo yao? Vijana 2memaliza vyuo hususan waalim mpaka sasa 2po mtaan na hatuna kazi.

Serikal inadai haina pesa za kuajiri wafanyakaz wapya, kwa nin istumie akil na busara kufuta mambo yasyo ya lazma kwa mfn hyo 64 ime2mika kwa upuuzi tu! Wananchi 2nataka kufaham kwa undan zaidi pesa iliyorudishwa na makampun hewa na ile ya ununuz wa rada imetumikaje, CAG watupe bajeti ya hyo pesa.

Nenda kaulizen hayo kwnza, mengne 2tatoa mara bada ya kupata majib sahih juu ya haya?

Naomba kuwasilisha.
 
Regia haya ya katazamaji sijui tuyaite ni kero au maoni au mchanganyiko wa mani na kero. Zaidi zinajikita kwenye matumizi ya TEKNOLOJIA na mwsho la posho.

TEKNOLOJIA
observation yangu a wanasiasa wengi wanangea Teknolojia mdomoni tu lakini hawajui itatatuae matatizo ya jamii

Googlemap
Ramani za google ni driving force kupata taarifa za sekta mbali mbali.Inashangza wakati wansiasa wetu wanaimba sayansi na teknolojia hata jiji la dar lenyewe ni sehemu ndogo sana tu bara bara na mitaa ndio zimeanishwa. Kama nyie Chadema mna halmashauri Onyeshini mfano wa kuingiza detail zote za ramani za maeneo yenu kwenye gogle na sio zikae makabatini. Vile vile wabunge mwambinei mama Tibaijuka pale wizara ya ardhi anatakiwa kuwa na kitengo cha googlemap japo kwa miaka mitatu ili zoezi la kuingiza detail za tanzania lifanikiwe. kuingiza majina ya vijiji barabara,wilaya na maeneo mengine muhimu ni bure. Itapendza detail za tanzana wilaya na mikoa kufika 2015 ziwe zimekamilika. Karne hii sio ya kuweka ramani makabatini.

Hii nilijaribu uandika wa urefu na upana kwenye chapisho hili

Hivi sasa kuna gari zinazotumia umeme Je wabunge na wizara huska zinajua?

Kama kweli wote tunaamini tuko kwenye karne ya sayansi a tenolojia basi mtakubalina nai kuwa sasa kua gari mabo znatumia umeme na sio mafuta. Na nyingine ni Hybrid. Sasa kwa serikali je wana taarifa za magari haya.Je kwa nini hawaafirri japo kuleta gari mbili au tatu kwa majaribio kuone utendaji wake kazi na ufanisi . Hapa hasa ni wizara ya sayansi a tenolojia au wzara ya mazingira. Kama ni watu wanaonkwenda na wakati basi tunataka tusikie wana mpango gani.

Ukiondoa magari ya umeme kuna kero je shangingi ndio standard gari analotaiwa kupanda nakutuia waziri? Kutoka masaki kwenda posta. Hivi mawazri na watendaji wengine wanana wamedharirishwa wakitumia japo VITARA au hata gari ndogo. Je si busara 50% ya VX za seriali zikiuzwa na kununua gari zinatumia mafuta kiodgo. Kufupisha hadithi soma hi kero/maoni wenye uzi huu

Yaani Naomba mkiweza waulzieni Je waziri na watendaji wengine wanajisiiai wanaptomua gari inayotumia zaidi ya lita 200 kwa wiki wakiwa jijini wakati wangewewza kutumia gari inayoweza kutumia lita hata 100 wa wiki?

ELIMU
Kuna shule hazina maabara,kama maabara zipo basi hazina vifaaa . kuna shule hazina waalimu wa sayansi . ICT(TENOHAMA) ina toa fursa za kufukia mapungufu haya. Je serialina wanasiasa wetu wanayajua.......
How?
Ni kiasi cha wizira au Idara, NGO au Mbunge au hata shule binafsi au hata mtu binafsi anayejihusiha na elimu kutafuta mwalimu mzuri wa somo fulani na watalmu wa kurekodi video, Kurekodi video akifunidisha au akifanya practical ya somo fulani. Then kutoa kuuza copi ya DVD kwa shule na wanafunzi. Shule zitahitajika kununa TV na DVD player kwa ajili hii. Naamini shule nyingi zinavyo hivi vifaa . One time cost inafanya kazi kwa miaka kadhaa. Wanafuzi na wazazi wanatkiwa kujua video sio lazima iwe ya kanumba .
Faida zake nini

  • Tatizo la maabara litakuwa limekiwisha na hakuna ulazima shule kuwa na maabarabadla yake wanaweza kuwa video room ya wanafuzi kuona kila practical inafanyikaje. kama shule haina mwalim au zile topic ngumu practical. One time cost. na hivyo ufanisi na matoek ya mwnaafunzi kuboreka.

  • kwa mwanafuzi itasaidia akiwa nyumbani anaweza kuona zaidi ya video ya anumba. anaweza kuona video ya lawas of motion.zaidi kuelew kama hakuelewa mwalimu darsani. mwnafuzi kuuliza maswali na kuongeza ubora wa elimu. Kuona kwenye video chemical distalltion process inavyofanyika ni tofauti na kusoma kwenye kitabu
Unaweza kuipata hii kiukamilifu kwenye uzii huu.



MICHEZO

Je kwenye mashindano ya london 2012 olympic tunajatarajia kupata medali ngapi na za aina gani.Je tumeridhka na kushiriki si kushindana .
Serikali kupitia JWTZ, JKT isaidie kutafta kuibua na kuedeleza vipaji ?

Michezo mbali mbali ina nafasi kubwa ya kuzalisha nyota lakini tumelalala. Kwa nini

  • JWTZ au JKT Kigamboni isianzishe chuo cha kuongelea. Kuna vijana nawaona wanakimbiza na viongozi wa fery sababu wanapenda kuchezea maji. Vijana wale ujuzi wao ukitumiwa mapena wakapata wakufunzi wazuri Tanzania itakuwa mbali kimchezo.​
  • JWTZ JKT Mkoni Arusha ianishe kituo cha mafunzo na mazoezi ya riadha ambapo wanafunzi wa shule mbali mbali za primary na sekondary wanaweza kuhudhuria kwa muda fulani na​
JWTZ JKT Mwanza wanaweza kushirikiana na wavuvi. Kule kun watu wanapiga kasia . Pia Kuna watu pia wanaendesha basikeli kama kina armstrong


POSHO NA MASLAHI YA WANASIA VS WATENDAJI
Wanasiasa wakiwemo wabunge wanatakiwa kutambua kuwa wao ni watchdog na sio watendaji. Kwa mana hiyo mafao na mapato ya mbunge kwa logicla nyepesi hayatakwiwi kuziki mapatao ta afisa Elimu , kilimo, mifugo Maji, Madini,Mhandisi,RPC, Mganga mkuu wa mkoa.

Kwangu naona ni kero kubwa kuona mbunge anastahiki za juu kuliko afisa elimu . kilimo au mifugo , n.k wa mkoa . Na kero zaidi sijasikia wabunge wakihoji kutaka watu hawa amabo ni watendaji mafao yao yangezewe. Maana ni watu hawa ndio wanataiwa kuleta changes kwenye jamii a sio wanasiasa. Tunaomba wabunge wastopishe kufanya Siasa ndio ajira inayolipa zaidi badala yake wafanya utendaji. Ni kero mbunge kuwa ndio mfanyakazi wa umma anayepokea mshahara mkubwa wilayani au mkoani na sio Afisa kilimo, mifugo au maji RPC etc . Jribuni kungalia na kulinganisha hata huko majuu hali ikoje.....

Ngoja niishie hapa .........










 
Siku zote nilikuwa na wasiwasi na uraia wako ila leo ndo nimejua wewe Sio Mtanganyika wala Mzanzibari....wewe ni mzamiaji.......kweli we Barubaru....mawazo yako yanaweza kuwa mazuri lakini kwa nini urumie neno lenu......yenu........ikimaanisha wewe si mmoja wetu. Angalia maandishi ya wenye uchungu na nchii hii wanasema nchi yetu..taifa letu.... lakini wewe...haumo!!!!Tueleze wazi we wa wapi. Au we Rostam nini?

Ntakushangaa sana kama wewe ulikuwa ulijui hilo.

Mimi ni Raia wa Oman, mzaliwa wa Kianga , Mwera, Zanzibar na nimesoma Tanzania Bara na nimewahi kufanya kazi Serikalini Muungano kwa miaka 8 .

Kumbuka Jf ni kwa wote. Soma rules zake utaligundua hilo. Na ndio maana najipambanua pasi na kujificha.

Sijui kama una la ziada.

 
Ragia

Bado naendelea.

[14] Idadi ya mawaziri isizidi kumi na tano.Hii yafaa zaidi ikawemo kwenye katiba.

[15] Serekali ya Tanganyika irejeshwe mara moja ili kuondoa kero za muungano.

[16] Raia wa Tanganyika hawana haki ya kumiliki ardhi Zanzibar sheria pia iwabane wazanzibar wasimiliki ardhi Tanganyika.

[17] Zanzibar ichangie gharama za uendeshaji wa serekali ya JMT.Tumechoka kila siku wanalilia mgao wa misaada lakini sijawa kusikia mchango wa Zanzibar katika uendeshaji wa vyombo vya muungano eg Wizara ya mambo ya ndani,Wizara ya Ulinzi,Wizara ya fedha na nk.

[18] Idadi ya wabunge toka visiwani ipunguzwe hili ilingane na idadi ya wananchi wa Zanzibar.
 
Ningependa kujua kama John Mnyika anakerwa na uchafu uliopo stendi ya mabasi hapo Ubungo. Kama anakerwa amechukua hatua gani kama kiongozi na mwakilishi wa jimbo la Ubungo.

Na kama hakerwi na huo uchafu, kwa nini ni hivyo?
 
shikamoo dada regina,

mi yangu ni haya...

1. kuna njia nyingi sana ambazo serikali inapoteza mapato yake, mengi yamezungumziwa lakini mnaonaje hili la kodi ya majengo?? em fikiria jengo kama lile la quality plaza linalipa kodi ya sh. 120,000/= tu je inastahili?? tunamagorofa mengi sana hapa dar..kama hiyo sheria itarekebishwa tutaongeza pato la taifa sana tu.

2.kuna hili swla lililotokea juzi kula geita, pale majambazi yalipotaka kupora madini, sasa naomba umuulize waziri wa fedha ni kiasi gani cha fedha serikali ilikipata kutokana na huo mzigo uliokua unasafirishwa?? je serikali iliwakilishwa na nani au mamlaka gani kuhakiki ule mzigo?? je kiwango cha uzalishaji ambacho kinatajwa na huo mgodi kinashabihiana na hali halisi(kwamba vile vipande vilivokamatwa vilikua ni uzalishaji wa week moja)
 
Regia:

Utekelezaji wa ahadi za serikali unapimwa kivipi?

Uwa mnakuwa na "review session" kama Bunge kuhusu yale ambayo serikali inaahidi kupitia Wizara mbalimbali zinaposoma hotuba zake bungeni?

Kwa mfano - tunaweza kujiridhisha very firmly kuwa tatizo la ukosefu wa nishati ya umeme limetatulia kwa asilimia ngapi? au kufikia 2014 litakuwa limetatuliwa kwa asilimia ngapi?

Kwa mfano - madai ya malipo ya malimbikizo ya walimu yameshughulikiwa kwa kiasi cha asilimia ngapi hadi sasa?

Kwa mfano - malipo ya wafanyakazi hewa yataendelea mpaka lini? 2025?

etc...
 
On a higher note @ R.Mtema though....baadhi ya kero za msingi za kuzungumzia bungeni......

  • Wabaneni Mkullo na waziri mkuu juu ya mwenendo hasi wa bajeti ya tz na jinsi gani wamejipanga kufidia pengo la bil.760 kwenye bajeti.......naona wamewatangazia IMF kuwa watapunguza matumizi ya bajeti ya maendeleo....hili tafadhalini msikubaliane nalo kabisa....wabaneni wapunguze matumizi yasiyo ya msingi kwenye bajeti..mfano posho etc
  • Wabaneni mawaziri husika haswa wizara ya madini na waziri mkuu kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya tume mbili..ile ya Mwakyembe ya richmond na hii ya juzi ya kina jairo......wabaneni watoe majibu ya jinsi gani wametekeleza mapendekezo yote la msingi likiwa kuwafukuza kazi wahusika....msikubaliane na majibu mepesi mepesi.
  • Fuatilieni kwa makini kama waalimu na wadai wengine wamelipwa madeni yao?.....(fanyeni kazi na kina Mgaya mjue)....msikubaliane na majibu mepesi mepesi kama kawaida yao.....these things have to end....
  • Fatilieni kwa kina hatma ya wanafunzi woote wa vyuo vikuu waliofukuzwa baada ya migomo ya kudai haki zao na hawaelekei kurudishwa tena vyuoni....na pia madaktari waliofukuzwa juzi kama watakuwa hawajarejeshwa makazini.....hakikishen mtapata msimamo wa serikali juu ya hatma ya hawa woote kama watakuwa bado hawajarejeshwa vyuoni/makazini..
  • Hojini juu ya mapungufu makubwa yaliyojitokeza katika utendaji dhaifu wa spika na katibu wake kwenye suala la matamko yanayokinzana kwenye ongezeko la posho zenu....tunataka watu wakiri mapungufu yaliyojitokeza na kuwashushia credibility kwa kiasi kikubwa mwenye macho yetu wa tz...Briefly.....hizi hoja chache zifanyieni kazi pia please.....
 
Wakuu habari! Nimatumaini yangu kuwa tunaendelea vizuri na majukumu yetu ya kila Siku.

Nimeamua kuanzisha Uzi huu kwa lengo la kukuza ya kero,maoni,ushauri na chochote toka kwenu ili tuweze kuyasimamia ndani na nje ya Bunge.Kwa kutambua kuwa wanaJF wamesambaa kila mahali,maofisini,mashuleni,mitaani,majumbani na huko kote kuna kero mbalimbali zinazohitaji attention ya Serikali lakini mambo hayaendi na ungpenda kuona suala hilo linafanyiwa Kazi na hivyo unapendekeza Kambi ya Upinzani izibebe na kuzisimamia. Basi tafadhali toa kero,maoni,ushauri au hata mapendekezo yako hapa.

Tafadhali kero ziwe za kijamii na sio za mtu binafsi.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati kwa Ushirikiano wenu.

Wenu katika Ujenzi wa Taifa
Regia Mtema

Regia Regia Regia tafadhali sana!
Frankly speaking, kwa upande wangu hii haijanivutia hata kidogo. Hivi mpaka leo kuna mtanzania yeyote bila kujali ni mbunge au mwananchi wa kawaida asiyekuwa na cheo chochote, asiyejua kero za watanzania hadi inabidi awaulize ndiyo azielewe? Aisee Regia tumekutuma huko Bungeni tukiwa tuko siriazi, unataka kuanza kufanya nini? Kumbe umeingia Bungeni ukiwa hata kero za wattanzania huzijui? Kwa nini? Ungeniambia unakusanya mawazo ningekuelewa, mawazo yanakava vitu vingi kuliko kero. Kero ni too specific kiasi ambacho sitarajii mbunge kama wewe urudi kwetu kuja kutuuliza. Tafadhali tafadhali tafadhali
!
 
mi kero yangu ni kuhusu wakazi wa kigamboni kilometa 15,000 watahama.muishinikize serikali ipange sehemu nyingine kwa sababu tanzania ina maeneo mengi ya wazi zaidi ya km 15,000. mfano chanika, morogoro n.k. na tatizo watahamishwa baada ya kutungwa sheria mpya...ni kwenye mchakato wa katiba. sehemu pekee kuona kama sheria ya kuwahamisha wananchi haivunji katiba. bila hivyo wananchi watapoza haki zao.nashukuru.
 
Regia Regia Regia tafadhali sana!
Frankly speaking, kwa upande wangu hii haijanivutia hata kidogo. Hivi mpaka leo kuna mtanzania yeyote bila kujali ni mbunge au mwananchi wa kawaida asiyekuwa na cheo chochote, asiyejua kero za watanzania hadi inabidi awaulize ndiyo azielewe? Aisee Regia tumekutuma huko Bungeni tukiwa tuko siriazi, unataka kuanza kufanya nini? Kumbe umeingia Bungeni ukiwa hata kero za wattanzania huzijui? Kwa nini? Ungeniambia unakusanya mawazo ningekuelewa, mawazo yanakava vitu vingi kuliko kero. Kero ni too specific kiasi ambacho sitarajii mbunge kama wewe urudi kwetu kuja kutuuliza. Tafadhali tafadhali tafadhali
!
Mbunge anayejua kila kero ya nchi hii huyo hatazaliwa. Endelea Regia kutushirikisha kwa njia kama hizi na nyingine. Kero, mawazo, hoja, mapendekezo, maoni hayawezi kuwa ya mtu mmoja.
 
Regia Regia Regia tafadhali sana!
Frankly speaking, kwa upande wangu hii haijanivutia hata kidogo. Hivi mpaka leo kuna mtanzania yeyote bila kujali ni mbunge au mwananchi wa kawaida asiyekuwa na cheo chochote, asiyejua kero za watanzania hadi inabidi awaulize ndiyo azielewe? Aisee Regia tumekutuma huko Bungeni tukiwa tuko siriazi, unataka kuanza kufanya nini? Kumbe umeingia Bungeni ukiwa hata kero za wattanzania huzijui? Kwa nini? Ungeniambia unakusanya mawazo ningekuelewa, mawazo yanakava vitu vingi kuliko kero. Kero ni too specific kiasi ambacho sitarajii mbunge kama wewe urudi kwetu kuja kutuuliza. Tafadhali tafadhali tafadhali
!
Mpaka leo hii sijui ni kwanini watanzania ni maskini. si ajabu kwa bibie kutokujua kero za wa tz wenzake.najumlisha hoja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom