Tunakusanya Kero ambazo ungependa zisemewe Bungeni na Nje ya Bunge na Viongozi wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Regia,
Kero kubwa wakazi wanaoishi Ukonga DSM. Ni kama vile hatuna mwakilishi. Barabara za kwenda kitunda, Kivule Moshi bar, kwa diwani ni barabara mbovu ajabu. Mvua ikinyesha hata kidogo tu nauli ya daladala inafikia shilingi 1,000 kwa mtu mmoja. Watoto wanashindwa kwenda shule na hata wafanyakazi wanatembea kwa miguu kwa masaa mpaka 3 ili kufika barabara ya Nyerere kupata usafiri.

Sasa swali langu: Kwanini Serikali imewatenga wananchi wa maeneo haya bila kuwapelekea huduma ya barabara?

Changamoto kwa chadema:Regia kwanini chama chako hakijizatiti katika maeneo hayo ili kuliteka jimbo hilila Ukonga? Kwa hakika shida ya barabara wanayopata wakazi wa maeneo haya wataipokea chadema kama mfalme endapo mkiwekeza huko.

Watu wamechoshwa na madiwani na mbunge wa chama cha CCM ambaye hana muda wowote na wananchi wa maeneo hayo.Chadema kwa vile wabunge wake ni wa Taifa basi lipiganieni jimbo hili kwa sababu lina mbunge picha tu.
 
Naomba mkatupiganie wafanyakazi, kodi ya PAYE ni kubwa sana inatuumiza sana sisi wafanyakazi, kwani hatuna sehemu ya kukwepea, bora wafanyabiashara wanauwezo wa ku collude na TRA wakakwepa, lakini sisi inakatwa juu kwa juu na mwajili, angalau kile kiwango kinachozidi 720,000 kiwe kinakatwa 20% badala ya 30% ya sasa.

Au wabadilishe mfumo mzima kama makampuni yanavyofanya, yanakatwa 30% baada ya kutoa gharama zao zote za uendeshaji ni kinachobaki ndo hukatwa kodi, tuwe na mfumo kwa wafanyakazi pia, kipato chetu chote baada ya kutoa matumizi yetu kama kodi ya nyumba, gharama za shule kwa watoto wetu,gharama za chakula n.k,

kiasi kinachobaki ndo kikatwe kodi, maana kodi zote anatupiwa mlaji (final consumer) this is not fair, kweli tunaipenda nchi yetu na tunapenda kulipa kodi, kitu kinacho tukatisha tamaa ni haya matumizi mabovu ya kodi zetu, please Mh Mbunge peleka kilio hiki cha wafanyakazi maana kodi yetu ndo inayotumika kuwalipa kodi hata nyie wabunge wetu.

Tunaomba serikaliyetu ijikite kukusanya kodi kwenye makampuni, badala ya kila mara kuzidi kumdidimiza mwananchi wa hali ya chini.
 
Asante sana kunjia hii tunaweza kuingia na kuwa na mwazo mapana.Kwanza kabisa kero yangu ni kuwa hii blabla ya maoni ya katiba mpya naomba mweweka mkakati maalum.Maana inavyoonekani ni kama mchezo wa kuigiza ,part 1 mara weka PART 2,KWISHA PICHA.

kwanza mwekeni rais na speaker chini muwaeleze ,mweelekeo wa taifa letu ni wapi,mimi niko mjini na nina access zote za habai alkini sijuwi kinachoendelea nasikia tu marumbano siasa nyingi wakati swala hili ndo tunatakiwa kuwa wamoja ,kwasababu unatengeneza kitu cha miaka mingi huko mbeleni wakati wewe regina ,kikwete na mimi hatutakuwepo.swala amabalo tunatakiwa kuwa na maono makubwa mbele kwamba nchi yetu iwe vipi,

Mimi ninachokiona ni kama watu wanaangalia 2015 tu.kwamba katiba ndo solution ya 2015,tuache hayo mawazo mgando,naungana na Mnyika siku alikuwa anahonjia na ITV alisema ,hii katiba sio ya chama fulani,wala Rais ni yawatu wote.

wewe fikiri mtu ulikuwa unapinga chepuo kwenye chama fulani ili katiba ikufavour ,linatokea la kutekea unaaungushwa kwenye uchanguzi vipi hayo uliyokuwa unayapingia chepuo ndo yanakuumiza wewe ,kwahiyo mimi nasema tena KATIBA Jamani tusipoteze muda kulumbana bali tukumaliane wote na kupainga kura ya wengi halisi wapewe.

Sio kutumia kwamfano nichosikia Tume ya taifa ya uchanguzi ndo italatibu kura hizo ,kwani hiyo kura mpaka ulatibu wewe nenda sehemu ukauliza hata sasa huko kijijini kuhusu hiyo tume watakuambia inasumbua mno.

Mimi nipendekeza kuwepo na mjadala murefu hata kama tutachukua 10 years kushughulikia katiba let be so.

Sio kama inavyopelekwa tutasababisha mambo mengi mabaya juu ya nchi yetu.

Asante
 
Ninayo mengi sana ila nitaje hili moja kwa leo ambalo ni mama wa mengine:-

Nimeenda kujiandikisha kupiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu nikapewa kitambulisho cha mpiga kura. Siku ya kupiga kura nafika kituoni jina langu halionekani kwenye orodha ilhali kitambulisho ninacho mkononi.

Nawasiliana na msimamizi wa uchaguzi wa kituo ananijibu tu kirahisi "KAMA JINA LAKO HALIPO MIMI SINA MSAADA MWINGINE. SUBIRI HADI UCHAGUZI UJAO". Ukitaka kuhoji zaidi unakutana na vyombo vya usalama - UNATAKA KUFANYA FUJO.

Kimya huyooooooo najiondokea zangu, haki yangu ndio hivyo tena imepotea. Na nahisi kwa hali inavyoonekana upuuzi huu utaendelea kujirudia tena na tena; kama si kwangu basi kwa wengine na majibu yakuwa hayo hayo.

Je, kuna mpango gani wa kumaliza kabisa tatizo hili?
 
Kilimo
1. Ruzuku ya kilimo - Utaratibu uliopo wa kutoa ruzuku ya pembejeo ni mbovu kuliko kitu chochote. Hakuna records za Mkulima yupi, yuko wapi, analima nini, analima kiasi gani, eneo analolima kitaalamu linahitaji pembejeo gani, tatizo hasa la mkulima wa eneo x ni nini? baada ya kuvuna mkulima x anafaidije mavuno yake, ni vigezo gani vinatumika kumqualify mkulima kupata ruzuku. Kukosekana kwa utaratibu huu kumefanya ruzuku inagawiwa kwa wakazi wa mijini!, pembejeo zinaibwa na kwa kweli, ufanisi wa suala la ruzuku ni pungufu ya 10%

2. Mauzo ya mazao ya kilimo - ni aibu kuwa serikali imekuwa inahamasisha kilimo lakini inashindwa kusaidia wakulima kuuza mazao yao, badala yake imekuwa ikikwamisha mauzo ya mazao nje ya nchi.

3. Maeneo ya mipakani - Control inayofanyika kuzuia usafirishaji wa chakula na sukari nje ya nchi imesababisha mateso makubwa kwa wananchi wa humo. Kwa mfano kwa sasa wilayani Rombo sukari ni Tsh 3000 kwa kilo kutokana na ugumu uliowekwa wa wafanyabiahsara wilayani humo kupata na kuuza sukari. Mahindi bei ni zaidi wa mara mbili ya maeneo mengine kwa sababu hizo hizo!

4. Shule za msingi na sekondari - Serikali imeshindwa kuboresha ubora wa shule za serikali, hali inayofanya kuongezeka kila siku kwa mamia ya shule za private. Matokeo yake ni kugawanyika kwa jamii ambapo watoto wa walala hoi na wenye fedha wanasoma shule tofauti. madhara yake ni kuwa unakuta mtoto wa mwalimu mkuu wa shule ya serikali anasoma shule ya private, mtoto wa mwalimu anasoma private, mtoto wa diwani private, watoto wa mratibu elimu, afisa elimu, mkuu wa wilaya nk wote wapo private, then inakuwa ngumu sana wadau hawa wa maendeleo ya shule za serikali kuwa na moyo na kubaki kuongea tu kwa maneno lakini hawahamasiki kwani wanajua watoto wao hawasomi humo.
 
Foleni nyingi katika Barabara Zingepungua kama Manispaa husika zingetenga maeneo na kukopa katika bank za TIB na kujenga miundombinu ya masoko na kuwaelimisha wafanyabiashara ndogondogo waweze kuhamishia shughuli zao Huko!! Kama eneo la ubungo Yenu Panahitaji soko, Mwenge Junction, tegeta na maeneo mengine ya aina hiyo! Sasa Inabidi tuwashauri ili wajali umuhimu wa masoko!! Hakuna plan bila kuweka maeneo ya social services!!
 
Heshima kwako Regia,

Kero yangu kubwa ni kama ifuatavyo.

[1] Wabunge kujiongezea posho.Huu ni uhuni mkubwa hamkuomba ubunge hili mjiongezee maslahi mliomba hili mtutumikie ajabu mmegeuka kero kila siku kilio cha posho kwa kisingizio maisha magumu tangu lini maisha magumu yamekuwa ni kwa wabunge pekee yao.

[2] Viti maalumu na viti 10 vya Rais vifutwe mara moja.Utafutwe utaratibu mwingine ambao utahakikisha wabunge wanawake wanachaguliwa na wanawajibika kwa wapiga kura.

[3] Teuzi za Rais [Mabalozi,Mawaziri,Wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama,Wakuu wa mashirika ya Umma] wathibitishwe na bunge

[4] Ukubwa wa Serekali upunguzwe.Bajeti inaonyesha 3/4 inatumika kwaajili ya uendeshaji wa serekali 1/4 kwaajili ya shughuli za maendeleo.Hali ibadilike 3/4 maendeleo na 1/4 shughuli za uendeshaji.

[5] Serekali kwa maana ya viongozi waache kutumia magari ya gharama kubwa eg Land Cruiser VDJ 200 na Nissan Y 61.Haya magari ni kwaajili ya wasanii matajiri wa ulaya na Marekani.Viongozi watumie Suzuki,Corolla,RAV4 au Land Cruiser HZJ 76.

[6] Serekali ipunguze utegemezi wa Budget toka nchi wahisani.

[7] Mikataba ya madini itazamwe upya.Kodi na tozo mbali mbali ziongozwe.Serekali imiliki hisa za migodi yote ya dhahabu.

[8] Wakuu wa Mikoa,Wilaya na manaibu waziri waondolewe mara moja.Zoezi hili litasaidia kupunguza matumizi ya serekali.

[9] Viongozi wa kuchaguliwa na wananchi wawajibike kwa wananchi waliowachagua na si chama.Kiongozi wa kuchaguliwa avuliwe uongozi na wananchi waliomchagua na si vyama hata kidogo.Ni vyema sheria ikapitishwa haraka hili kumlinda mwananchi.

[10] Muda wa kupisha budget upunguzwe.Utafutwe utaratibu wa kuwapatia mapema waheshimiwa wabunge mswaada.

[11] Kiwepo kipengele kinachomtaka mbunge walau awe na shahada ya kwanza.Wabunge ni watunga sheria na wasimamizi wa serekali kumpa mtu ubunge asiyekuwa na elimu ya kutosha ni hatari kubwa.Fikiria ukiomba kazi ya Pump attendant unaulizwa cheti iweje mbunge kigezo kiwe kusoma na kuandika tu !.

 
Pamoja na kero zote zilizo tajwa kero nyingine kubwa ni ninyi chadema kufungua ofisi vijijini kwa kasi ndogo mno,tena pengi tu hata kufika hamja fika akati kuna wadau wenu, fungueni matawi na mashina kule kwenye watanzania wengi mijini kwa asilimia kubwa mmeeleweka.fanyeni hayo mapema jamani!
Kila rakheri katita ujenzi wa Taifa!
 
Kwanza nianze kwa kukupa heri ya mwaka Mpya.
Kero ziko nyingi sana,
1.Tunahitaji katiba Mpya na siyo Viraka kwenye katiba iliyochakaa,Iko haja ya kuangalia nafasi ya Mgombea binafsi katika ngazi zoote ili kuondokana na ugaidi wa kisiasa, wale viongozi wanajifanya miungu watu ndani ya vyama wametuchosha.
2.Iko haja ya kuwa na chombo kingine zaidi ya TFDA, Ambachp kiangalia mwenendo mzima wa mzunguko wa Mazao toka sehemu moja kwenda nyingine ili kupunguza upandaji holela wa vyakula. Bei ya Mchele kila siku inapanda sababu hatuzijui

3.Bei ya umeme ipungue.

4.Mafisadi warudishe pesa zetu.
5.Mafisadi warudishe nyumba za serikali.
 
[11] Kiwepo kipengele kinachomtaka mbunge walau awe na shahada ya kwanza.Wabunge ni watunga sheria na wasimamizi wa serekali kumpa mtu ubunge asiyekuwa na elimu ya kutosha ni hatari kubwa.Fikiria ukiomba kazi ya Pump attendant unaulizwa cheti iweje mbunge kigezo kiwe kusoma na kuandika tu!.
Tena hawa wa kusoma na kuandika "Mheshimiwa spika naunga mkono hoja aslimia mia miaaaaa" kumbe hamna kitu kichwani anaona kama akipinga anaweza kuulizwa sababu za kutounga mkono hoja hivyo anajiwahi.
 
Kuna mambo manne tu ambayo watanzania ni lazima yafanyike ili kuikomboa nchi yenu katika kuondoa kero na kuleta hali nzuri kiuchumi kwa wananchi wenu.
1. Kupata Katiba iliyo bora.
a. Katiba yenye kulinda maslahi ya taifa lenu na kujali maslahi ya wananchi kwanza.
b. Katiba yenye kulinda rasilimali za Taifa lenu na kuzimilikisha kwa wananchi
c. Katiba itakayowafanya viongozi wote waliochaguliwa na wananchi waweze kuwajibika kwa wananchi na sio vyama vya siasa.
d. Katiba itakayoangalia uwezekano mkubwa wa kuinua hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja mpaka kwa taifa zima kwa kifupi katiba yenye utashi wa kujenga uchumi wenu na kuondoa utegemezi.

2. Wananchi kupenda kuwajibika katika kulijenga taifa lenu. Hapa panahitajika zaidi kujenga msukumo na tarbia yya wananchi kulipenda kwa dhati taifa lenu na kuwa na kiu ya maendeleo . Kuchukia rushwa na ubinafsi na kupenda kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yenu

3. Viongozi kuacha kutumia afisi za umma na madaraka katika kujilimbikizia mali binafsi. Hapa panatakiwa kuweka sheria kali kulidhibiti hili


4. Taifa kuwa na mtazamo wa kiuchumi zaidi na sio siasa. Kila kitu kinachohusi maslahi ya taifa ni lazima kitazamwe kimapana zaidi katika angle ya kiuchumi na si kisiasa

Mkifanikiwa kurejesha hayo juu basi pasi na shaka mtaanza kusonga mbele.

Kila la kheir

 
dada Regia,

Inasemekana 80% ya watanzania ni wakulima, na kwakuwa serikali imeshauza ardhi kubwa sana na bado inaendelea kutafuta wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi (korea, USA, india etc ) kwa kasi ya kibunga, hii 80% itashughulika na nini miaka 10 ijayo? maana hata rais 2010 alikumbana na malalamiko ya wananchi handeni (azam), kagera (mzungu) etc wananchi wanalia hawana chakula na watoto wao hawasomi kwakukosa ada kwakuwa ardhi waliyokuwa wanaitegemea kwa kilimo amepewa mwekezaji. Rais aliwaahidi atashugulikia tatizo hilo, amefikia wapi?
 
Tena hawa wa kusoma na kuandika "Mheshimiwa spika naunga mkono hoja aslimia mia miaaaaa" kumbe hamna kitu kichwani anaona kama akipinga anaweza kuulizwa sababu za kutounga mkono hoja hivyo anajiwahi.

Mimi nashauri viondolewe kabisaa hivi viti maalum. Kwani vinasababisha mengi sana ikiwemo upendeleo, rushwa na kubwa zaidi vinaleta fitna katika vyama.

Kila mtu agombee kwa wananchi.
Na vile vile kila mbunge akae katika jimbo lake kama ilivyo kwa madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa au vijiji ili aweze kuwajibika moja kwa moja kwa wapiga kura wake na si vinginevyo.

Vote of No confidence ni muhimu kwa yule asiyaweza kutimiza ahadi zake.
 
Kero kubwa ni Vivuko vya Magufuri pale Kigamboni kwetu. Hivi ninaandika wazazi walio wengi wamewaondoa watoto wao waliokuwa wanasoma mjini kwa sababu ya ukubwa wa gharama za vivuko. Usafiri wa mtoto mmoja ambae anaishi maeneo ya mjini na mitaa yake ni kama Tzs.175,000/= kwa term ambayo ni miezi mitatu lakini gharama ya mtoto mmoja anayevuka kwa usafiri wa magari ya wanafunzi kabla ya nauli mpya ni Tzs.300,000/=. Sasa baada ya kupanda kwa gharama za pale kivukoni ni Tshs.420,000/= kwa term.

Hii Kero kubwa na wazazi tumeshindwa kumudu hizo gharama. Pls mtusaidie kwa hili.
 
Regia naomba niongeze mambo mawili matatu:

1. Brela. Hii ofisi ni aibu tupu. Vurugu mwanzo mwisho, mafaili yako kila mahali. Sijawahi kuona ofisi iliyokaa hovyo kama hii. Kuna urasimu wa kutisha, na hadi sasa najiuliza hivi hii ndio ofisi inayotakiwa kushindana na nchi zingine ndani ya Afrika Mashariki? Wafanyakazi wanaongea vibaya sana. Jambo lilinitisha ni pale mteja anakuja na kuanza kutafuta faili lake (mteja anatafuta faili kwenye ofisi za Brela)! Utunzaji wa kumbukumbu za wateja uangaliwe upya.

Rwanda inachukua siku moja tu kusajili kampuni, tena bila kuzungushwa, hapa Brela utapiga hodi week tatu hata mwezi. Tena na maneno ya kejeli juu!

Nyalandu anaweza kujigamba kuwa wewe ni presidential marerial lakini kama ameshindwa kuondoa uozo kwenye idara moja tu kama hii Brela ataiwezaje nchi nzima?

2.TRA. Machine za VAT ni jambo zuri lakini zoezi zima limejaa utata. Nitaeleza. Hizi machine zinauzwa na 'specific' agent. Bei yake ni juu sana, na hapa nahisi kuna walakini. Kwa nini TRA wasitoe specific requirement na kuacha watu wanunue wanakotaka ili mradi machine ina vitu vyote vinavyohitajika TRA? Kwa nini tulazimishwe kununua kwa maduka maalum? Sasa hivi tuko kwenye dunia ya utandawazi, hivi kujua bei ya kitu fulani sio jambo la siri tena, machine za VAT ni ufisadi mtupu.

3. Ulipaji kodi. Waziri mkuu aeleze Taifa inakuwaje Airtel wenye wateja approx 5 walipe kodi kushinda Vodacom wenye wateja milion 10 (mara mbili ya Airtel)? Inakuwaje Resollute walipe kodi kubwa kuliko Barrick? Hivi inawezekana housegirl akalipa kodi kubwa kuliko bosi wake? Kwa wale wanaofuatilia mambo, bosi wa Income tax UK (TRA ya UK) anatuhumiwa kupokea 'ukarimu' toka baadhi ya makampuni makubwa ili aangalie kwa jicho la huruma kodi zao. Amekuwa ananunuliwa Lunch na mabosi wa haya makampuni na mojawapo ni Vodafone (Vodafone ndio majority shareholder wa Vodacom TZ). Sasa tupate maelezo, vodacome wamelipa kodi kiasi gani kwa miaka 5 iliyopita? Au madawati yanafidia kodi?

Pia, ni makampuni mangapi ya madini yameanza kulipa kodi mpya? Ni aibu kuendelea kuomba omba wakati serikali inashindwa kukusanya kodi. Wafanya biashara wadogo wadogo wanatembelea na Majembe auction Mart kila leo lakini haya makampuni ya kibepari wanaendelea kukwepa kodi.
 
Kuna mambo manne tu ambayo watanzania ni lazima yafanyike ili kuikomboa nchi yenu katika kuondoa kero na kuleta hali nzuri kiuchumi kwa wananchi wenu.
1. Kupata Katiba iliyo bora.
a. Katiba yenye kulinda maslahi ya taifa lenu na kujali maslahi ya wananchi kwanza.
b. Katiba yenye kulinda rasilimali za Taifa lenu na kuzimilikisha kwa wananchi
c. Katiba itakayowafanya viongozi wote waliochaguliwa na wananchi waweze kuwajibika kwa wananchi na sio vyama vya siasa.
d. Katiba itakayoangalia uwezekano mkubwa wa kuinua hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja mpaka kwa taifa zima kwa kifupi katiba yenye utashi wa kujenga uchumi wenu na kuondoa utegemezi.

2. Wananchi kupenda kuwajibika katika kulijenga taifa lenu. Hapa panahitajika zaidi kujenga msukumo na tarbia yya wananchi kulipenda kwa dhati taifa lenu na kuwa na kiu ya maendeleo . Kuchukia rushwa na ubinafsi na kupenda kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yenu

3. Viongozi kuacha kutumia afisi za umma na madaraka katika kujilimbikizia mali binafsi. Hapa panatakiwa kuweka sheria kali kulidhibiti hili


4. Taifa kuwa na mtazamo wa kiuchumi zaidi na sio siasa. Kila kitu kinachohusi maslahi ya taifa ni lazima kitazamwe kimapana zaidi katika angle ya kiuchumi na si kisiasa

Mkifanikiwa kurejesha hayo juu basi pasi na shaka mtaanza kusonga mbele.

Kila la kheir


Siku zote nilikuwa na wasiwasi na uraia wako ila leo ndo nimejua wewe Sio Mtanganyika wala Mzanzibari....wewe ni mzamiaji.......kweli we Barubaru....mawazo yako yanaweza kuwa mazuri lakini kwa nini urumie neno lenu......yenu........ikimaanisha wewe si mmoja wetu. Angalia maandishi ya wenye uchungu na nchii hii wanasema nchi yetu..taifa letu.... lakini wewe...haumo!!!!Tueleze wazi we wa wapi. Au we Rostam nini?
 
-Teuzi zisizothibitishwa na zisizo na kikomo zinazofanywa na Rais.
Kwa kuongezea, kwanini watu wachache na familia zao ndio wanafaidi keki ya taifa?

Inaleta maana kuwarundikia familia moja vyeo na fursa? mfano mume na mke kupata uwaziri, kuteuliwa kwenye nafasi zenye marupurupu kibao na hata wakati mwingine hawana sifa za ajabu za kutisha.

Kwanini nafasi za juu serikalini zisitangazwe na watu wagombee/wa apply na kusailiwa? Nafasi kama za wakurugenzi, makatibu wakuu etc.na ziwe za mikataba ili utendaji upimike na kuamua warudi tena ama la!


 
Sijui ni jinamiz gani limewakumba kiasi cha ninyi wabunge wa CDM kutoweza kutambua au kuuona ukweli. Najua wote mnatambua kuwa jukumu kubwa la mbunge ni kuismamia Serikali na sio kuwa tarishi kubeba manendeleo toka serikalini kupeleka bungeni kama CCM walivyowafanya wananchi kuamini.

Natambua kuwa wachache wenu wanaifanya vyema hii kazi ya kuismamia Serikali, lakini kwa kuwa wananchi hawana elimu ya uraia ya kutosha kutambua nini majukumu ya mbunge bado wataendelea kuwapima kwa mtazamo ule ule wa kiccm ambao kwa bahati mabaya nanyi mliutumia kuingia bungeni, yaani kuwadanganya wananchi kuwa mnao uwezo wa kutatua kero zao mbali mbali.

Ni kwanini msianzishe kampeni kubwa ya kuwazindua watanzania ili kwanza watambue majukumu ya wabunge kuwa ni kuismamia Serikali; na ili mbunge awez kutimiza jukumu hilo ni lazma awe mtafiti na msomaji mzuri wa machapisho, ripoti na taarifa mbali mbali za kiserikali, hivyo muda wa kutafuta maendeleo ya kimbo moja moja haupo.

Kama Mhe Benjamin Mkapa aliweza kuomba kura kwa kutumia ilanai ya uchaguzi ya CCM iliyoshehni ahadi kibao na akachaguliwa halafu ndani ya kipindi cha miezi 6 tu akawaambai ukweli watanzania kuwa ilani ile haitekelezeki, akalipa madeni ya Tanzania na kurejesha imani ya wafadhili na kufanikiwa kutawla mfumuko wa bei. Ninyi wabunge wa CDM na CDM kwa ujamal mnashindwa nini kutuambia ukweli kuwa mbunge sio tarishi wa kubeba maendeleo toka serikalini kuleta jimboni?
 
Ragia

Bado naendelea.

[11] Jaji mkuu achaguliwe na majaji wa mahakama ya rufaa.Apigiwe kura na majaji wenzake.Jaji kiongozi achaguliwe na majaji wa mahakama kuu na atoke miongoni mwa majaji wa mahakama kuu.Iwepo bodi ya kuajiri majaji na mahakimu.

[12] Wabunge wawe na ukomo wa vipindi viwili au vitatu mwisho.Hii itaondoa wanasiasa aina ya Dr Mzindakaya au Jackson Makwete.

[13] Itungwe sheria ya kumfukuza mbunge / diwani aliyeshindwa kutimiza wajibu wake.Wapiga kura wakiorozesha majina na saini kwa idadi itakayokubaliwa kisheria mbunge au diwani anaweza kutimuliwa mara moja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom