Wakuu habari! Nimatumaini yangu kuwa tunaendelea vizuri na majukumu yetu ya kila Siku.
Nimeamua kuanzisha Uzi huu kwa lengo la kukuza ya kero,maoni,ushauri na chochote toka kwenu ili tuweze kuyasimamia ndani na nje ya Bunge.Kwa kutambua kuwa wanaJF wamesambaa kila mahali,maofisini,mashuleni,mitaani,majumbani na huko kote kuna kero mbalimbali zinazohitaji attention ya Serikali lakini mambo hayaendi na ungpenda kuona suala hilo linafanyiwa Kazi na hivyo unapendekeza Kambi ya Upinzani izibebe na kuzisimamia. Basi tafadhali toa kero,maoni,ushauri au hata mapendekezo yako hapa.
Tafadhali kero ziwe za kijamii na sio za mtu binafsi.
Natanguliza Shukrani zangu za dhati kwa Ushirikiano wenu.
Wenu katika Ujenzi wa Taifa
Regia Mtema
Heshima kwako Regia,
Kero yangu kubwa ni kama ifuatavyo.
[1] Wabunge kujiongezea posho.Huu ni uhuni mkubwa hamkuomba ubunge hili mjiongezee maslahi mliomba hili mtutumikie ajabu mmegeuka kero kila siku kilio cha posho kwa kisingizio maisha magumu tangu lini maisha magumu yamekuwa ni kwa wabunge pekee yao.
[2] Viti maalumu na viti 10 vya Rais vifutwe mara moja.Utafutwe utaratibu mwingine ambao utahakikisha wabunge wanawake wanachaguliwa na wanawajibika kwa wapiga kura.
[3] Teuzi za Rais [Mabalozi,Mawaziri,Wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama,Wakuu wa mashirika ya Umma] wathibitishwe na bunge
[4] Ukubwa wa Serekali upunguzwe.Bajeti inaonyesha 3/4 inatumika kwaajili ya uendeshaji wa serekali 1/4 kwaajili ya shughuli za maendeleo.Hali ibadilike 3/4 maendeleo na 1/4 shughuli za uendeshaji.
[5] Serekali kwa maana ya viongozi waache kutumia magari ya gharama kubwa eg Land Cruiser VDJ 200 na Nissan Y 61.Haya magari ni kwaajili ya wasanii matajiri wa ulaya na Marekani.Viongozi watumie Suzuki,Corolla,RAV4 au Land Cruiser HZJ 76.
[6] Serekali ipunguze utegemezi wa Budget toka nchi wahisani.
[7] Mikataba ya madini itazamwe upya.Kodi na tozo mbali mbali ziongozwe.Serekali imiliki hisa za migodi yote ya dhahabu.
[8] Wakuu wa Mikoa,Wilaya na manaibu waziri waondolewe mara moja.Zoezi hili litasaidia kupunguza matumizi ya serekali.
[9] Viongozi wa kuchaguliwa na wananchi wawajibike kwa wananchi waliowachagua na si chama.Kiongozi wa kuchaguliwa avuliwe uongozi na wananchi waliomchagua na si vyama hata kidogo.Ni vyema sheria ikapitishwa haraka hili kumlinda mwananchi.
[10] Muda wa kupisha budget upunguzwe.Utafutwe utaratibu wa kuwapatia mapema waheshimiwa wabunge mswaada.
[11] Kiwepo kipengele kinachomtaka mbunge walau awe na shahada ya kwanza.Wabunge ni watunga sheria na wasimamizi wa serekali kumpa mtu ubunge asiyekuwa na elimu ya kutosha ni hatari kubwa.Fikiria ukiomba kazi ya Pump attendant unaulizwa cheti iweje mbunge kigezo kiwe kusoma na kuandika tu !.
Kuna mambo manne tu ambayo watanzania ni lazima yafanyike ili kuikomboa nchi yenu katika kuondoa kero na kuleta hali nzuri kiuchumi kwa wananchi wenu.
1. Kupata Katiba iliyo bora.
a. Katiba yenye kulinda maslahi ya taifa lenu na kujali maslahi ya wananchi kwanza.
b. Katiba yenye kulinda rasilimali za Taifa lenu na kuzimilikisha kwa wananchi
c. Katiba itakayowafanya viongozi wote waliochaguliwa na wananchi waweze kuwajibika kwa wananchi na sio vyama vya siasa.
d. Katiba itakayoangalia uwezekano mkubwa wa kuinua hali ya uchumi wa mtu mmoja mmoja mpaka kwa taifa zima kwa kifupi katiba yenye utashi wa kujenga uchumi wenu na kuondoa utegemezi.
2. Wananchi kupenda kuwajibika katika kulijenga taifa lenu. Hapa panahitajika zaidi kujenga msukumo na tarbia yya wananchi kulipenda kwa dhati taifa lenu na kuwa na kiu ya maendeleo . Kuchukia rushwa na ubinafsi na kupenda kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yenu
3. Viongozi kuacha kutumia afisi za umma na madaraka katika kujilimbikizia mali binafsi. Hapa panatakiwa kuweka sheria kali kulidhibiti hili
4. Taifa kuwa na mtazamo wa kiuchumi zaidi na sio siasa. Kila kitu kinachohusi maslahi ya taifa ni lazima kitazamwe kimapana zaidi katika angle ya kiuchumi na si kisiasa
Mkifanikiwa kurejesha hayo juu basi pasi na shaka mtaanza kusonga mbele.
Kila la kheir
Watumishi wa umma kupandishiwa mishahara lakini bado wanalipwa kwa rates za zamani (hawajarekebishiwa mishahara yao)
Watueleze pesa za sherehe ya miaka 50 ya uhuru zemetoka wap? Wkt kwenye bajet hazpo?
Wakuu habari! Nimatumaini yangu kuwa tunaendelea vizuri na majukumu yetu ya kila Siku.
Nimeamua kuanzisha Uzi huu kwa lengo la kukuza ya kero,maoni,ushauri na chochote toka kwenu ili tuweze kuyasimamia ndani na nje ya Bunge.Kwa kutambua kuwa wanaJF wamesambaa kila mahali,maofisini,mashuleni,mitaani,majumbani na huko kote kuna kero mbalimbali zinazohitaji attention ya Serikali lakini mambo hayaendi na ungpenda kuona suala hilo linafanyiwa Kazi na hivyo unapendekeza Kambi ya Upinzani izibebe na kuzisimamia. Basi tafadhali toa kero,maoni,ushauri au hata mapendekezo yako hapa.
Tafadhali kero ziwe za kijamii na sio za mtu binafsi.
Natanguliza Shukrani zangu za dhati kwa Ushirikiano wenu.
Wenu katika Ujenzi wa Taifa
Regia Mtema
Madiwani wasilipwe!....Mh.Regia,
Hoja nyengine ya muhimu ambayo inahitaji kufanyiwa maamuzi haraka ni kuhusu maslahi ya madiwani.
Madiwani ni watumishi wa umma ambao wako karibu sana na wananchi na ndio msaada mkubwa sana kwenu wabunge.
Tunataka muishinikize serikali ianze kuwalipa madiwani mishahara kama inavyowalipa watumishi wa umma wengine mkiwemo nanyi wabunge.
Kumlipa diwani kiasi cha sh.120,000 kwa mwezi ni kumdhalilisha na hii huchangia sana kushindwa kuwatumikia kikamilifu wananchi.
Vilevile malipo duni kwa madiwani kunafanya nafasi hizo kutowavutia wasomi na hivyo kujikuta madiwani wengi ni wazee ama watu wenye elimu za chini, kitu kinachotoa mwanya kwa wakurugenzi wengi kuwaburuza na wao kutokuwa na uwezo mkubwa wa kufuatilia bajeti na matumizi ya fedha katika miradi inayopangwa katika halmashauri zao.
Mh.Regia,

Kwanza, tunapinga posho kwa watumishi wote wa umma. Walipwe mishahara ambayo itakatwa kodi na kuchangia pato la taifa. As long as wanasiasa nao ni watumishi wa umma suala la kuwalipa halikwepeki. Labda kama unataka nafasi za kisiasa zifutwe, kitu ambacho hakiwezekani.Madiwani wasilipwe!....
Wabunge walipwe mil. 3 kwa mwezi... bila posho yoyote, posho zote zifutwe. Kuna mambo mengi ya kushughulikiwa na wanasisa wanalipwa fedha nyingi wasizostahili.
source of money??
Naona maswali mengi ni ya kuongeza matumizi; semeni na namna ya kupata fedha msiwe kama "wafanyakazi wao ni kudai mishahara tu bila kusema pesa itoke wapi??"
Kweli kabisa na inaonekana hakuna ugumu maana tuna mifano ya matukio kadhaa ambayo tumeona serikali baada ya kuingia mikataba na wawekezaji inatamka na kuzirejesha mali hizo kutoka wawekezaji. Mfano mzuri wa hili ni Serikali kupitia Waziri Mkuu Pinda kumnyang'anya mwekezaji ANBEN aka Mkapa, Mkewe pamoja na Yona Mgodi wa Kiwira. Mfano mwingine ni kunyang'anywa kwa UDA kutoka kampuni ya SGL na mifano mingi mingine, Hii inaonyesha hakuna ugumu wowote kwa Serikali kunyang'anya watu waliouziwa nyumba za serikali katika mazingira tatanishi ni suala la dhamira tu.Anza na hili la Nyumba za Umma waliojiuzia bei rahisi Vigogo wa serikali na wafanyabiashara wakubwa tena kwa bei rahisi,chonde chonde anza na hilo kwani lina-effect uchumi wa nchi na tumeona viongozi wa serikali wanakaa hotelin na kua na ofisi hoteli coz nyumba za kukaa hawana kwa sababu mafisadi wamejiuzia,hili mliwekee priority ya kwanza tunahitaji nyumba zote zirudishwe serikalini na sio kua za watu binasfi
Ragia
Bado naendelea ........
[20] Shirikisho la EAC likataliwe kwa nguvu zote.Nchi za Uganda,Kenya Rwanda na Burundi zote zimeungana dhidi ya Tanzania.Waziri wa Afrika Mashariki ni vyema akaambiwa wazi masuala yafuatayo kamwe yasikubaliwe.
[A] Masuala ya Ulinzi na Usalama yabaki jukumu la kila nchi.
Masuala ya Ardhi yasiingizwe katika EAC.
[C] Soko moja la Utalii Tanzania ikatae kwa nguvu zote.Sote tunajua jinsi Kenya ilivyodanganya ulimwengu kwamba mlima Kilimanjaro na mbuga ya wanyama ya Serengeti ziko kwao.Tanzania ikikubali upumbavu wa soko moja la utalii.
[D] Pasport itumike kuingia na kutoka kwa wageni wote wa EAC.