Tunakoelekea watumishi kujiendeleza kielimu(regular classes) itakuwa ni suala la kujitoa muhanga

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,564
3,472
Ile imani ya kusoma ili upande daraja la mshahara au cheo imeyeyuka kwa kasi ambayo kilichobaki ni historia yake .
Kinachonipa matumani ni kuwa mfumo huu unazidi kuipa thamani elimu licha ya kuonekana kama joto juu ya barafu
Nadhani kukubali kuwa elimu ni uwekezaji siyo suala la kufundishwa tena
 
Kinachompandisha mtu cheo sio elimu. Elimu ya nyongeza kama masters degree au PhD ni elimu ya ziada haina uhusiano na kazi unazozifanya unless iwe ni kazi za kinadharia kama ualimu au utafiti ila za practical hakuna uhalisia kabisa.

Hua nashangaa mtu anamaliza bachelor degree anaunganisha masters, nashangaa sana au mtu anasoma masters ili aongezewe cheo, huo ni ukosefu wa maarifa.

Huku bongo masters imekua kama fasheni, unakuta ofisini watu kibao wana masters huku kichwani hakuna kitu.
 
Kabisa!

Kuna wengine niliwasikia wakisema wanavyeti vya masters lakini hawajahi ingia darasani

Nilichoka kusikia nakwambia!

Nikawaambia kumbe ndo maana mko hivyo mlivyo!

Elimu ni zaidi ya kupata cheti!

Inatakiwa mwanafunzi ahudhurie darasani, amsikilize mkufunzi ili aweze kuwa transformed from low level to high level.

Sasa kama mtu huingii darasani utawezaje kuambukizwa kwa njia ya kusikia toka kwa mkufunzi?

Siyo siri na wengi ndo maana hawataki kwenda kusoma masters ya UDSM sababu wale wako very strict, kuanzia mwanzo wa udahili, madhurio ya vipindi darasani, n.k wanafuatilia hasa .
 
Hata ulaya ni hivo hivo.mfumo wa elimu dunia nzima ni mmoja.Hivi kuna chuo duniani kinafundisha wanafunzi kudizaini maroketi tena maabala? Kudizaini chip za electronics circuits.Ingekuwa hivyo tungekuwa na wataalamu na viwanda vya roketi dunia nzima maana kila taifa hupeleka watu wao kusoma ulaya.China wamefanikiwa kupata teknolojia wametumia mbinu nyingi sana sio kusoma havadi tu au MIT.Vyuo vyetu tunavyovidharau huzalisha wataalamu wanaotumika ulaya na America.Tujadili jinsi ya kuboresha si kuponda.Siku hizi elimu ipohata mtandaoni sasa mnaponda tu hamtoi mbadala.
 
Kinachompandisha mtu cheo sio elimu. Elimu ya nyongeza kama masters degree au PhD ni elimu ya ziada haina uhusiano na kazi unazozifanya unless iwe ni kazi za kinadharia kama ualimu au utafiti ila za practical hakuna uhalisia kabisa.

Hua nashangaa mtu anamaliza bachelor degree anaunganisha masters, nashangaa sana au mtu anasoma masters ili aongezewe cheo, huo ni ukosefu wa maarifa.

Huku bongo masters imekua kama fasheni, unakuta ofisini watu kibao wana masters huku kichwani hakuna kitu.
Kuna tafiti huwezi zishiriki bila kuwa na master au PhD. Degree unasoma vitu vingi master unaspecialize zaidi.
Hivi unaweza kushiriki tafiti za kuunda quantum computer bila kuwa na master au PhD au wanaodevelop 5G teknology unafikiri wanadegree tu.Google, Facebook nk team leader wao ktk tafiti ni PhD holder au very experienced peoples.
 
Elimu imuwezeshe mtu ku improves performance na siyo vinginevyo!

Modern rewarding zinazingatia performance ya mtu na siyo elimu pekee!

Maana kuna watu wanavyeti lakini kwenye kazi ni wadhaifu sana!
 
Kuna tafiti huwezi zishiriki bila kuwa na master au PhD. Degree unasoma vitu vingi master unaspecialize zaidi.
Hivi unaweza kushiriki tafiti za kuunda quantum computer bila kuwa na master au PhD au wanaodevelop 5G teknology unafikiri wanadegree tu.Google, Facebook nk team leader wao ktk tafiti ni PhD holder au very experienced peoples.
PhD au masters google ni preferred qualifications ila minimum qualifications zao hua ni bachelor degree.

Kama ulivyosema kuna vitu viwili, PhD au experience plus creativity skills, leadership skills na mambo kama hayo.
 
Kabisa!

Kuna wengine niliwasikia wakisema wanavyeti vya masters lakini hawajahi ingia darasani

Nilichoka kusikia nakwambia!

Nikawaambia kumbe ndo maana mko hivyo mlivyo!

Elimu ni zaidi ya kupata cheti!

Inatakiwa mwanafunzi ahudhurie darasani, amsikilize mkufunzi ili aweze kuwa transformed from low level to high level.

Sasa kama mtu huingii darasani utawezaje kuambukizwa kwa njia ya kusikia toka kwa mkufunzi?

Siyo siri na wengi ndo maana hawataki kwenda kusoma masters ya UDSM sababu wale wako very strict, kuanzia mwanzo wa udahili, madhurio ya vipindi darasani, n.k wanafuatilia hasa .
Huwezi kupingana na mabadiliko ya Dunia, kupata cheti ina maana kwamba ulifanya mitihani ya masomo husika ukafaulu ndipo ukapata cheti. Kufaulu mtihani au kupata uelewa wa kitu chochote sio lazima ufundishwe na mtu bali hata kwa kujisomea wewe mwenye kutoka katika vyanzo mbalimbali. SO usilazimishe kila mtu afundishwe na mwalimu darasani ndipo tuamini kwamba amesoma. Mimi naweza nisiingie darasani hata siku moja hadi semester inaisha na wewe ukaingia vipindi vyote na mwisho wa siku tukifanya mtihani mimi napata A na wewe D hicho ndicho kipimo cha uelewa wetu.

Ndio maana dunia ya sasa inahamasisha masomo kwa njia ya masafa au Distance and Open Learning.
 
Unaweza ukauhadaa umma na discourse za matakawa ya Dunia.
Dunia ni nani?na inahamasisha Open and Distance learning kwa nini?tunaweza tukasema Dunia kumbe ni tabaka fulani linapalilia maslahi take "hegemony"
Haya masuala ya kuambiana Dunia inataka hivi au vile yanapaswa kuangaliwa kwa kina sana kuliko tunavyofikiri.
Leo ushawishi Mkubwa unafichwa kwenye matakwa ya Dunia lakini ukiulizwa Dunia ni akina nani unaweza ukakuta ni maslahi ya Nchi chache zilizoshika uchumi wa Dunia zinapalilia maslahi yao.
 
Umeshikilia kwenye kipengele cha dunia lakini hujaziona hoja zingine nilizoeleza? au kwingine kote umeelewa isipokuwa kipengele hicho? Mfano hoja yangu kwamba kufundishwa darasani sio kigezo pekee cha kuelewa na kufaulu, bali hata kwa namna nyingine ya kutafuta maarifa.
 
Kinachompandisha mtu cheo sio elimu. Elimu ya nyongeza kama masters degree au PhD ni elimu ya ziada haina uhusiano na kazi unazozifanya unless iwe ni kazi za kinadharia kama ualimu au utafiti ila za practical hakuna uhalisia kabisa.

Hua nashangaa mtu anamaliza bachelor degree anaunganisha masters, nashangaa sana au mtu anasoma masters ili aongezewe cheo, huo ni ukosefu wa maarifa.

Huku bongo masters imekua kama fasheni, unakuta ofisini watu kibao wana masters huku kichwani hakuna kitu.
Aiseee!
 
Ile imani ya kusoma ili upande daraja la mshahara au cheo imeyeyuka kwa kasi ambayo kilichobaki ni historia yake .
Kinachonipa matumani ni kuwa mfumo huu unazidi kuipa thamani elimu licha ya kuonekana kama joto juu ya barafu
Nadhani kukubali kuwa elimu ni uwekezaji
Soma kwa kuongeza wigo wa ufikiri na channel Zaid ukisoma kwa ajili ya kupanda daraja,cheo,au mshahara utaumia Sana usipopata

Ila ukisoma kwa kupata channel nyingne huwa unapata tu na Wala hujutii ukikosa
 
Well said
 
Umeshikilia kwenye kipengele cha dunia lakini hujaziona hoja zingine nilizoeleza? au kwingine kote umeelewa isipokuwa kipengele hicho? Mfano hoja yangu kwamba kufundishwa darasani sio kigezo pekee cha kuelewa na kufaulu, bali hata kwa namna nyingine ya kutafuta maarifa.

Sasa nikuulize mazingira ya Ulaya ambako siyo lazima mwanafunzi aingie darasani yanafanana ya hapa nchini Tanzania ?

Wale wenzetu walishaandaliwa tangu elimu za awali. Kuna mambo muhimu sana ambayo walishayapata hapo awali.

Kifupi mifumo ya elimu ya Ulaya na ya Tanzania ni tofauti na kwa hiyo hatupaswi kuwaiga kwa kutoingia darasani.

Mnajidanganya sana!

Na ndo maana value additions hazionekani makazini.

Yani mtu anakariri vitu weeee mpaka basi!
 
Back
Top Bottom