Tunakoelekea Walimu wataacha kuhangaika na mtoto wa mtu

Mapema kama zipi.. Mtoto kama huyo unakuta ameshawai kusimamishwa.. Ila habadiliki, walimu wanaweza kutaka afukuzwe ila bodi ikakataa
Well said,tena na hizi shule zetu zinavyoendeshwa kisiasa,jumba bovu linawadondokea walimu.
 
Kwa walio katika taaluma ya ualimu wanaweza kunielewa ila kama sio mwalimu basi hutanielewa. Mimi sio mwalimu ila nimepita huko.

Kizazi cha sasa, malezi ya watoto wa siku hizi na kubadilika kwa life style yetu ni mambo yanayofanya kazi ya ualimu kuwa ngumu sana na alierudisha viboko mashuleni aliona mbali ila tuendako walimu wanaweza kuacha kabisa kuadhibu wanafunzi japo viboko vimeruhusiwa.

Watoto wa siku hizi wanalelewa tofauti na sana na zamani na wakienda mashuleni wanakuwa hivyo hivyo na mwalimu usieweza ku-control hasira zako utaishia jela kama sio kufukuzwa.

Utatumia mbinu zote za ualimu ila bado unaweza tu usifanikiwe ku-handle watoto wa siku hizi kwa mafanikio na hii ni moja ya sababu ya kushuka kwa kiwango cha elimu.

Baada ya kupitia baadhi ya comments, nimegungua kuna watu hawajanielewa ila naomba niweke ufafanuzi ufuatao juu ya hili tukio kulingana na mtazamo wangu.

Kwanza nianze kwa kusema binafsi siungi mkono tukio hili ila najaribu kuwa objective kulingana na hulka ya sisi binadamu(mimi na wewe).

Ukiangali ile clip ni wazi wale walimu walipandwa na hasira kupita kiasi na bila shaka si hivi hivi tu bali kuna sababu ingawa hakuna sababu inayohalalisha walichokifanya ila kwa nature ya sisi binadamu bado tu tunaweza kujikuta unafanya kitendo kama hicho bila kutarajia kutokana na hasira tu.

Kwa mfano,mtu anaweza kumchoma mtu kisu katika ugomvi kutokana na hasira na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani lakini mwisho wa siku kwa mshangao wa wengi mtuhumiwa anaweza kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na wala si kuua kwa kukusudia kutokana na mazingira ya tukio lenyewe.

Unaweza usiwe na nia ya kuua lakini mtu akakutibua na kutokana na hasira ukachukua kitu kama nondo au jiwe na kumpiga nacho na bahati mtu huyo akapoteza maisha na mahakamani ukahukumiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia na sio kuua kwa kukusudia.

Kwa kesi hii ya walimu hawa,bado tunahitaji kusikia kutoka upande wa pili ni nini hasa kilitokea na kuwafanya kufikia hatua ile ya kushangaza.Si ajabu tukisikia nini kilitokea baadhi mnaweza kujikuta mnabaki katikati.

Ni kweli taaluma na maadili ya ualimu hayaruhusu kabisa walimu kufanya walichokifanya ila niwaulize jambo moja.

Hivi mtu unapomfumania mkeo au mumeo au ukahisi anaku-cheat,kuna sheria inayokuruhusu kumpiga mpaka kumjeruhi,kumpa kilema na wakati mwingine hata kumuua?

Hamjawahi sikia mtu anachinja mkewe kwasababh ya wivu tu?

Ukishakuwa na hasira na ukashindwa kuzi-control akili inakuwa sio yako tena na hutakumbuka kuna maadili ya ualimu wala sheria za nchi bali utafanya kile akili yako inachokutuma kufanya kwa wakati huo ila mwisho wa siku wengi huishia kujuta na wengine hata kujiua.

Hivi mnafikiri haya matukio yameanza leo?Haya matukio yapo tu siku zote ila hapa teknolojia ndio imetufumbua macho na bila teknolojia hii tukio pengine lingepita kama yanavyopita mengine.

Tuwe objective na tusisahau hasira ni hasara

mimi sio mwalimu ndugu, lakini nimekuelewa sanaa, tunakoelekea ni waalimu watakuwa hawajishughulishi na chochote, mwanfunzi afanye homework au asifanye sawa tu, au wanawatungia maswali rahisi ya 1-1=? . watu wanalaumu upande mmoja tu bila kujiuliza upande wa pili ilikuwaje? what was the trigger of the same? hilo darasa lina wanafunzi zaidi ya 10 naamini hivyo, lakini kwa nini mwanafunzi huyo tu apigwe?lazima kuna shida pia kwa upande wa mwanafunzi, aidha alitoa lugha chafu kwa waalimu...tunatakiwa kuwa objective sana..tatizo sasa hivi mambo yanaenda kisiasa siasa..ki oya oya..hiyo ndio shida...
 
Salary slip kaka sijawahi kukupinga hoja zako zote kwa hili la Mbeya nakupinga MTU unapiga kama unapiga nyoka! hapana kaka wangeweza hata kuua kabisa. Wawachape hata fimbo 4 siyo mbaya lakini siyo hiyo ya Mbeya.
Hizo fimbo 4 anaweza kukataa kuchwapwa wakat huo huo anamkunja mwalimu shati! Katika mazingira haya mwalimu anashikwa na hasira anajikuta kutoa adhabu isiyostahili.walimu wanapata wakati mgumu kwa vijana wa Leo huko mashuleni.
 
Aisee dogo kapinda.
Naamini Waalim wataadhibiwa kwa temper ya mawaziri tu.

Lakini wajiandae shule za Serikali kuanguka vibaya mno kwenye matokea ndani ya muda mfupi.
Maana waalim kama mleta mada anavyosema,hakuna mwalim atashughulika na mtoto wa mtu.

Dogo malezi kwao Zero kabisaaa,na Mwalim aliepost hili tukio alikuwa na njia ya kuipeleka hii kesi kwa mkurugenzi,matokeo yake ameiingiza kwenye kiki ambayo ni athari kwa taifa.

Mie mwanzo niliona kama dogo walikurupuka tu kumdunda,kumbe ana record tata mpaka ndani ya familia.Sasa utetezi huu utafanya madogo watukutu wengine waige kama yeye kwa kuona kwamba watatetewa.

Mihemko ya Mawaziri kwa issue hii wajue itawa cost hapo mbele,na hapo mbele wajitokeze tena baaada ya hali ya elim kuwa mbaya kwa wanafunzi kuwa ndio waalim.
Tufaham kwamba Miaka ya under 2000,waalim walikuwa watu wazima ila sasa walim ni wadogo sana ambapo wanafunzi wana challenge nao sana.Na ndio kitakachofuata.

Waalim wana madai yao kibaooo,halafu wanafunzi pia wawadhalilishe.
Nahisi mwalim alie rusha tukio angeanza kulipeleka kwa Afisa wa Elim na Mkurugenzi kwa hatua za awali badala ya kuwaponza waalim wote Nchini bila kujua kwamba athari yake ni kubwa zaidi.

Naamini waalim hao wangeadhibiwa tu kwa hatua hizo bila kukurupuka kwenye mitandao ambapo mihemko ya Mawaziri inaoshesha kwamba Taasisi za Elim mkoa wa Mbeya hazina kazi na hazijui majukum yake.
Waalim watawachia sasa wanafunzi wafanye wanavyotaka,na tusubiri Zero nyingine teleeee.
Na mbaya Zaidi waalim wengi huwa na tabia ya kuwa na Chuki na waalim wenzao wanaokwenda kwa Vitendo kwenye mashule yao.Sasa nahisi Mwalimhusika nae alierusha picha alikuwa na Lake
Hongera kwa kuwa na uwezo mpana wa kuchambua na kuyaelewa mambo yanahusu taaluma ya Ualimu.
 
Mkuu naongea hivi from experience.Kuna mwalimu mmoja wa kike alifanyiwa vituko darasani na wanafunzi ikabidi aje kuripoti staff kutafuta msaada na kilichofuta ni hasira za walimu.

Ndio maana nasema mwalimu asieweza ku-control hisia zake kwa nyakati hizi ataishia kubaya.
Wanted inawezekana na ww ulishawah fanya unyama kama huu sema tu hakuwepo wa kukurekod mpuuz mkubwa ww unatetea wanafunzi waumizwe imagine kafanyiwa mwanao mbn watanzania hatuna utu!! Kwa maelezo yako unasupport huo unyama na kama na ww ni mwalim lazma tukupeleleze unaish vp na watoto wawatu tawezekana na ww ni jipu!!

Sheria inasema iwapo mwanafunzi kakaid adhabu ya mwalimu arudishwe kwao akaite mzaz wake ikishndkana afukuzwe tena kwa uthibitisho wa bodi ya shule sio kumpga !!!! Na nina was was na ualim wako pamoja na matokeo yako kiujumla ya somo la saikolojia!!
 
Kwa walio katika taaluma ya ualimu wanaweza kunielewa ila kama sio mwalimu basi hutanielewa. Mimi sio mwalimu ila nimepita huko.

Kizazi cha sasa, malezi ya watoto wa siku hizi na kubadilika kwa life style yetu ni mambo yanayofanya kazi ya ualimu kuwa ngumu sana na alierudisha viboko mashuleni aliona mbali ila tuendako walimu wanaweza kuacha kabisa kuadhibu wanafunzi japo viboko vimeruhusiwa.

Watoto wa siku hizi wanalelewa tofauti na sana na zamani na wakienda mashuleni wanakuwa hivyo hivyo na mwalimu usieweza ku-control hasira zako utaishia jela kama sio kufukuzwa.

Utatumia mbinu zote za ualimu ila bado unaweza tu usifanikiwe ku-handle watoto wa siku hizi kwa mafanikio na hii ni moja ya sababu ya kushuka kwa kiwango cha elimu.

Baada ya kupitia baadhi ya comments, nimegungua kuna watu hawajanielewa ila naomba niweke ufafanuzi ufuatao juu ya hili tukio kulingana na mtazamo wangu.

Kwanza nianze kwa kusema binafsi siungi mkono tukio hili ila najaribu kuwa objective kulingana na hulka ya sisi binadamu(mimi na wewe).

Ukiangali ile clip ni wazi wale walimu walipandwa na hasira kupita kiasi na bila shaka si hivi hivi tu bali kuna sababu ingawa hakuna sababu inayohalalisha walichokifanya ila kwa nature ya sisi binadamu bado tu tunaweza kujikuta unafanya kitendo kama hicho bila kutarajia kutokana na hasira tu.

Kwa mfano,mtu anaweza kumchoma mtu kisu katika ugomvi kutokana na hasira na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani lakini mwisho wa siku kwa mshangao wa wengi mtuhumiwa anaweza kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na wala si kuua kwa kukusudia kutokana na mazingira ya tukio lenyewe.

Unaweza usiwe na nia ya kuua lakini mtu akakutibua na kutokana na hasira ukachukua kitu kama nondo au jiwe na kumpiga nacho na bahati mtu huyo akapoteza maisha na mahakamani ukahukumiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia na sio kuua kwa kukusudia.

Kwa kesi hii ya walimu hawa,bado tunahitaji kusikia kutoka upande wa pili ni nini hasa kilitokea na kuwafanya kufikia hatua ile ya kushangaza.Si ajabu tukisikia nini kilitokea baadhi mnaweza kujikuta mnabaki katikati.

Ni kweli taaluma na maadili ya ualimu hayaruhusu kabisa walimu kufanya walichokifanya ila niwaulize jambo moja.

Hivi mtu unapomfumania mkeo au mumeo au ukahisi anaku-cheat,kuna sheria inayokuruhusu kumpiga mpaka kumjeruhi,kumpa kilema na wakati mwingine hata kumuua?

Hamjawahi sikia mtu anachinja mkewe kwasababh ya wivu tu?

Ukishakuwa na hasira na ukashindwa kuzi-control akili inakuwa sio yako tena na hutakumbuka kuna maadili ya ualimu wala sheria za nchi bali utafanya kile akili yako inachokutuma kufanya kwa wakati huo ila mwisho wa siku wengi huishia kujuta na wengine hata kujiua.

Hivi mnafikiri haya matukio yameanza leo?Haya matukio yapo tu siku zote ila hapa teknolojia ndio imetufumbua macho na bila teknolojia hii tukio pengine lingepita kama yanavyopita mengine.

Tuwe objective na tusisahau hasira ni hasara

Iwe iwavyo walimu wale ni kizazi cha nyoka, tofautisha adhabu kwa maana ya kurekebisha na SHAMBULIO ambayo ni jinai, kutoa adhabu kwa kosa la kutokufanya homework hakukuhitaji kundi la walimu watano kumuadhibu kijana, ilikuwa jukumu la mwalimu wake wa somo husika tu! Anyway, wamevuna walichopanda, kazi kwao!
 
Kasaidia kufahamika kwa haya, pia alisikika akiwatahadharisha walimu wenzie
Logic na mwalimu huyu alierekodi huu unyama anafaa kuwa kiongozi maana hatetei unyama na unyamkera wala unyonyaji na km kuna mtu ana no yake ani pm nitamzawadia maana yy ni mlezi mwema
 
Kweli kabisa. Wizara haina mamlaka ya kuwasikiliza wahalifu, shambulio ni jinai mahakama ndo yenye mamlaka ya kuwasikiliza.
Wangekuwa waungwana wangejisalimisha wenyewe, wangejua hawana hatia wasingetoroka.

Hivi kwa tamko na tishio kama lile la waziri wa mambo ya ndani wewe ungeenda.? Ukizingatia tayari wameshakuwa biased na wana hukumu yao mkononi pasipo kufuata sheria.?

I Bet hili swala utawala wa JK lisingekuwa hivi. Lingetatuliwa kistaarabu na kihekima zaidi.

Ila hofu watendaji aliyowajengea raisi ya kutaka kuonekana wanafanya kazi, matokeo yake ndo haya. Kufanya mambo kwa kukurupuka ambapo in long run itakuja kuangamiza elimu ya yaifa kwa ujumla wake.
 
Logic na mwalimu huyu alierekodi huu unyama anafaa kuwa kiongozi maana hatetei unyama na unyamkera wala unyonyaji na km kuna mtu ana no yake ani pm nitamzawadia maana yy ni mlezi mwema

Jina lako linaadifu unachokitetea. Nonsense kabisa.
 
Jana TBC kuna wanafunzi walihojiwa, walikua wanasema huyo denti alikua hahudhurii vipindi na mara nyingi alikua anaonekana kwenye madarasa mengine akipiga stori, wakati wenzake wako wanakula lecture.
 
Nimepitia majibu ya wengi humu, nimegundua hawajafahamu kuwa kuwashambulia mwalimu ni sawa Na kutega Bomu kwenye shule za magu. Ngoja tuone wakianza kufeli watarudi humu kwa 120kph
Ningekuwa ni mimi nipo kazini ningeacha kabisa kufuatilia wanafunzi,ningeandaa kila kitu na darasani naingia kama ushahidi tu.
 
Niliwahi kufundisha part time home kwetu kwa kujitolea.manafunzi wapuuzi yakawa yanataka kupimana ubavu.nikamwambia Head master mimi nina hasira,utakuta dent wako amezima kwa mkongoto.naomba kuacha kazi
 
Back
Top Bottom