Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Tangu wakati Mwalimu akiwepo kwenye madaraka au nje ya madaraka kulikuwa na changamoto kama taifa, na wale wanaotaka tuamini kwamba enzi za Mwalimu kulikuwa hakuna changamoto ni watu ambao hawataki kuukubali UKWELI. Lakini tofauti na viongozi wengine waliomfuata Mwalimu kwenye Urais, yeye alikuwa anazielezea changamoto zilizopo, anazichambua,anatafuta njia za kukabiliana nazo,anakabiliana nazo,anafanya tathimini kisha anatoa mwelekeo.
Enzi za Mwalimu kulikuwa na maandiko mengi sana yaliyoandikwa na yeye mwenyewe au yaliyotokana na maamuzi ya vikao kwa kufuata falsafa yake. Mwalimu aliandika vitabu, makala, vijarida na alitoa hotuba mbalimbali kuelezea mambo muhimu yahusuyo taifa. Kama mtu atachukua hatua ya kuyasoma au kusikiliza hotuba za mwalimu, basi bila shaka atagundua kwamba Mwalimu alijenga utaifa na kuusimamia utu wa watu wake.
Lakini tangu kuja kwa mfumo wa vyama vingi kumekuwa na kiwewe cha kushika madaraka na kuyang'ang'ania na kupoteza kabisa watu wanaojali nchi yetu inakwenda wapi. Kiuhalisia jamii nzima imetopea kwenye kiu kubwa sana ya "kupata" bila ya kujali huko kupata kunapatikanaje.
Sasa hivi hapa nchini kwetu kuna udini wa kutisha sana na kwa bahati mbaya Rais wetu Jakaya Kikwete aliishia kusema tu "...kampeni za uchaguzi mkuu zilitawaliwa na udini" bila ya kwenda kwa kina sana udini huo ulifanywa na nani dhidi ya nani. Matokeo yake kila mwananchi akatoka na Tafsiri yake.
Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba sasa hivi ni waislamu "moderate" peke yao ambao wanaweza kusimama hadharani na kusema wao ni CHADEMA damu damu. Na wakristo wengi hivi sasa hata waliomo ndani ya CCM wanaamini "waislamu" wana ajenda ya siri ya kuislimisha nchi na wanaitumia CCM kama chombo cha kufanikisha azima yao hiyo. Hali ya kutokuaminiana kati ya dini hizi mbili ni mbaya kiasi kwamba hata ukiona viongozi wa dini hizi wanachekeana hadharani unatia shaka kutokana ya yale yanayotokea na kupangwa sirini!!
Tanzania (siyo Tanganyika wala Zanzibar) ilijengwa wakati wa vuguvugu la umajumui wa kiafrika (Panafrikanisim). Tanzania hiyo ilikuwa Tanzania ya watu wote kwa maendeleo ya watu wote na kila mtanzania aliwaamini viongozi wake na wao waliamini katika dhana ya "serikali ni wananchi" na 'cheo ni dhamana" Kila jambo lilikuwa letu sote ingawa tofauti ilikuwepo.
Tanzania ya leo kama mwaka 1995 Mwalimu aliiona ina "nyufa" basi bila shaka hii ya sasa baadhi ya kuta zake zimeshaanguka na kila apitaye nje anaona kilichomo ndani. Hakuna tena anayeutaka Muungano (wapo wanaojidai kuutaka) na wala hakuna tena anayejali kama ukivunjika kitatokea nini.
Tanzania ya leo watu wanaamua kuwa wanachama (siyo wafuasi) wa chama fulani si kwa sababu za kupenda sera,Itikadi au falsafa ya chama husika, bali kwa sababu chama hicho kinamhakikishia uwezo wa kushinda uchaguzi ili apate "ulaji' au njia za kujinufaisha yeye mwenyewe.
Watu hawasomi tena kwa ajili ya kuongeza maarifa ili wakaitumikie jamii inayowahusu, bali siku hizi kusoma ni zana mojawapo inayomsaidia mtu kuongeza nafasi ya kupandishwa cheo au kuongezwa mshahara. Hali hiyo imesababisha watu kuvurugana na kukanyagana kwenye kughushi vyeti au hata kuhonga ili "wafaulu' mitihani kwa kiwango cha juu sana (GPA?) kwa lengo la kuonekana "wasomi" bila ya kujali kama wana elimu stahiki kwenye fani husika.
Maadili kwenye jamii yetu yameshapuuzwa siku nyingi sana. Mtu kuanzisha NGO ya kulelea watoto Yatima kwa lengo la kupata fedha za kuanzishia miradi yake binafsi si kosa la jinai tena. Ni sehemu ndogo sana (kama bado ipo) ambayo haijihusishi na ufisadi huu wa kimaadili. Wazazi, watoto na wanajamii wote tunaufurahia mmomonyoko huu wa maadili kwa sababu tu unatufaidisha kwa namna moja ama nyingine.
Mtazamo wangu kama jamii ya Tanzania tukiendelea namna hii basi bila shaka huko tuendako siku si nyingi taifa letu LITASAMBARATIKA!!