Tunaisambaratisha Tanzania!!

Hapa akitokea rafiki yangu Topical na Sweke34 basi thread hii itasomeka CLOSED.
Na akitokea Kiranga (mwanasayansi wa JF) basi thread hii itawakimbiza watu kwa hoja.
Acha niwasubiri.

Asante kwa kunikumbuka inaonekana we have something in common!

Wewe unaipenda chadema kwasababu gani?

Wewe unaichukia CUF kwasababu gani?

Vyama vyote hivi vinaipinga CCM lakini kwanini umechagua Chadema?...

Udini upo solution yake si kukimbia ni kuongea na kuwekena sawa..na wakristo waache kuchota fedha za umma..no easy ride..tutapambana hadi kieleweke..time is not a problem to us
 
Mkuu Kigarama,
Unachokisema ni kweli tupu. Lakini mimi najikita zaidi katika kutafuta ufumbuzi. Umeelezea vizuri sana jinsi kuta zilizokwisha bomoka katika jumuiya yetu. Je, tumechelewa sana kwamba nyumba nzima itaporomoka, au kuna hatua tunaweza kuchukua kunusuru hili jengo na kulirudisha katika mwelekeo sahihi?

Haki Sawa Kwa wote..

87 vs 13 be reviewed..
 
Udini ulikuwepo tokea enzi za ukoloni na hivi sasa unakuja kwa dizaini yake yani ya kileo zaidi.Chakushangaza zaidi ni kwamba tunatunga sheria halafu sisi wenyewe tunakiuka.Kwasababu katiba ya nchi imesema nchi haina dini ila imani zitabaki kwetu sisi wananchi.Na ukiangalia zaidi hapa michuano ni kati ya dini mbili uisilamu na ukristo.Na ukweli ni kwamba sio suala la kuaminiana kivipi ila ni kutaka kuongoza nchi kwa kupendelea watu fulani hilo ndio kubwa zaidi.Na vilevile kumekuwa na malalamiko mingi kutoka kwa waisilamu kwamba hawapewi nafasi ya kujiunga na OIC ili na wao wawe na balozi wao ili wapate misaada kutoka ktk jumuia za kiisilamu.Na sioni kwanini wakristo wanakataa hilo na limepingwa bungeni na wabunge wengi wakiwemo mawaziri ambao wote ni wakristo.Kwasababu kama nchi haina dini halafu ikaonyesha upande mmoja umezidi kupita mwenzake basi hapo malalamiko lazima iwepo.Kwakuwa wakristo wamepewa nafasi kubwa ambayo nauhakika inawasaidia kwa kiasi kikubwa kujiunga na VATICAN na kuwa na balozi wao basi inabidi na waisilamu wapewe haki zao.Haya ndio mambo yanatakiwa ktk nchi kuweka usawa ili kusiwe na malalmiko.Hii nchi ina idadi kubwa ya waisilamu na wakristo na idadi zinakaribiana kwa hivo lazima haki itendeke na kama hakutakuwa na suluhisho basi kunaweza kuchafuka zaidi ya hivi mnavoona.Na ukiangalia miaka iliopita viongozi wote wakristo waliweka wakiristo wengi ktk madaraka kuanzia ngazi za juu mpaka chini naweza kusema asilimia 70 walikuwa ni wakiristo na hiyo 30 iliyobakia imefika kwasababu ya Zanzibar.Na JK alirekebisha na kujaribu kuweka usawa ili kusiwe na manung'uniko kutoka kwa waisilamu lakini haimaanishi kwamba ni mdini.Anajua kama waisilamu wanalalamika kuhusu idadi ya waisilamu ktk uongozi.Na kingine ambalo pia ni moja ya tatizo ni kuhusu bajeti kwa wakristo ambayo makanisa yanapokea kila mwaka tokea kusainiwa kwa "memorundum of understanding"mwaka 1992.Hili nalo ni neno kwasababu litakuja kuzua jambo kwasababu waisilamu hawataki tena kuonewa yaani misikiti haina hesabu ktk nchi isipokuwa makanisa tu.Na ukiangalia bajeti hiyo inatoka kwa kila mwananchi anaelipa kodi yaani muisilamu na mkristo pamoja na wengine.Sasa hilo ni moja ya tatizo.Kusema ukweli wakristo mnatakiwa kuangalia hili jambo ili muone kiundani zaidi kwanini waisilamu wanalalamika au je hayo yaliyopo au yanayozungumziwa ni kweli?Na kama yapo je kwanini serikali haliweki usawa kwasababu uimara wa nchi ni muungano wa wananchi.Hata kama kutakuwa na tofauti za kidini itabidi tuziache makanisani na misikitini na yanayohusu nchi tuyaangalie kwa wakati wake.Hatutaki yale ya Nigeria na Sudan yakafika huku.Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
 
Mkuu Kigarama, Unachokisema ni kweli tupu. Lakini mimi najikita zaidi katika kutafuta ufumbuzi. Umeelezea vizuri sana jinsi kuta zilizokwisha bomoka katika jumuiya yetu. Je, tumechelewa sana kwamba nyumba nzima itaporomoka, au kuna hatua tunaweza kuchukua kunusuru hili jengo na kulirudisha katika mwelekeo sahihi?
...Nimeipenda hii. Ni ukweli usiopingika kwamba, kwa nyakati tofauti, viongozi mbali mbali, hasa wa kisiasa, kwa maslahi binafsi au kwa kutekeleza na kuendeleza malengo yao, wamekuwa wakiwagawa Watanzania. Nasikitika kusema kuwa, hii ilianza toka enzi ya Mwalimu JKN. Waingereza wana ka msemo kazuri..."wagawe, uwatawale".

...Nini kifanyike?. Mi nadhani ni vyema Watanzania wakatafakari na kutambua kama kuna faida ambayo wameipata, wanaipata au wataipata kwa kuendeleza ugonjwa huu. Je, tunajenga nchi yenye maendeleo, kama hatuna mshikamano kama Watanzania na si watu wa dini, kanda, rangi, au kabila gani?

...Tujiulize, tatizo la maendeleo katika jamii fulani ya Kitanzania, linatokana na nini? Je, ni ubaguzi, kutengwa, kutojiendeleza, kunyimwa haki za msingi za kiraia, au ni nini?. Kwanini Wahindi -ambao wako nasi siku nyingi, lakini wametengwa na hata wakati mwingine kubaliwa- wana maendeleo yanayoonekana wazi, katika nchi yenye kila aina ya vikwazo vya maendeleo?

...Busara hushauri kwamba, unapopatwa na ajali kitu cha kwanza ni kupata huduma stahiki, na si kuanza kumlalamikia aliyekugonga, kwamba ndiye aliyesababisha ajali. Kitu cha muhimu ni uhai na hali nzuri kwanza, si maneno mengi yasiyo tibu au kuleta nafuu, baada ya kupata ajali.

...Wanaoona wamekuwa marginalized lazima watafiti chanzo na kukifanyia kazi kwa vitendo, si kwa kulalamika. Maneno matupu hayavunji mfupa!.

...Dunia yote hii, hamna jamii iliyoendelea kwa ku seek entitlement, bila kutoka jasho kwanza na hivyo ku deserve hiyo. Maendeleo hayaletwi na mdomo, huletwa kwa kutumia kichwa kufikiri na kutenda kwa mikono.
 
watu bwana! Wanaona udini tu hapo wakati kuna suala zima la elimu na jinsi gani unaitumia kufanikisha maisha yako na ya jamii inayokuzunguka. Hivi mtu akishaanza kusoma Master degree, ana mpango wa kujiajiri tena? Sio bongo. Kujiajiri kwa watu hawa ni matokeo ya kukosa ajira. Elimu ni maarifa ya kukabiliana na changamoto za kimaisha.
 
Watu weusi (Waafrika) hawana ubongo wa kutosha ku-accomodate jinamizi liiitwalo dini. Wataigiza kuwa wanapendana, likija suala la dini ndipo utapoona ujuha wao. Ni wehu tu. Afrika bwana taabu kweli kweli!!! Mojawapo ya mambo ambayo hunikimbiza JamiiForums ni hizi bangi zinazoitwa dini.

Wanafiki wanaongea kuhusu dini lakini hatuoni cha maana wanachofanya juu ya hizo dini. Hawa ni watu weusi, hawa ni Waafrika. Wamelewa. Dini!! Maajabu. Nasepa.
 
Back
Top Bottom