Tunaenda AFCON na jezi ambazo si Tanzania na wala hatushtuki

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Ndugu zangu, heri ya mwaka mpya 2024.

Baada ya kimya cha muda mrefu, leo nimewiwa kuandika jambo moja. Samahani sana kwa wale ambao nitakuwa nimewakwaza kwa namna yoyote ile.

Nimetumia muda mrefu kuzitazama jezi za timu ya taifa, Taifa Stars. Kuna hoja inanijia kichwani.

Kwa maoni yangu ninadhani kwamba hizi ambazo wengi tunaamini ni jezi za timu ya Taifa huenda zikawa si za kwetu. Kwa nini? Hoja yangu inatokana na nini? Naomba usome.

Msingi wa hoja yangu unakuja katika misingi ya kwamba, rangi za jezi za timu ya taifa huwakilisha bendera ya nchi husika.

Kwa mantiki hiyo, rangi za jezi za timu ya taifa ni sharti ziendane na rangi halisi za bendera ya nchi husika, vivyo hivyo kwa muktadha wa Tanzania.

Je, bendera ya Taifa ya Tanzania imeelezwa vipi kwa mujibu wa sheria? Hili ndiyo swali la kujiuliza.

Kimsingi rangi za bendera ya taifa ya Tanzania zimebainishwa kwa Sheria Namba 15 ya Bendera na Nembo ya Taifa ya mwaka 1971, yaani 'The National Flag and Coat of Arms Act No. 15 of 1971.

Eneo la kwanza la Sheria hiyo (First Schedule) imeeleza kwa lugha ya Kingereza kama ifuatavyo:

“A rectangular flag divided into two equal portions diagonally from the righ-hand upper corner to the left-hand lower corner the upper portion of green colour and lower portion of blue colour; the dividing bands being golden,black and golden colours, the two golden bands of equal size and smaller than the central black band”

Kwa tafsiri yangu ni kwamba, kwa mujibu wa sheria hiyo Namba 15 ya mwaka 1971:

'Bendera ya taifa ni ya Mstatiri, iliyogawanywa katika pande mbili zilizo sawa kimshazari kutoka kona ya juu upande wa kulia kuja kona ya chini upande wa kushoto, kipande cha juu cha rangi ya kijani na kipande cha chini cha rangi ya buluu; mistari inayogawanga ikiwa ni ya rangi ya dhahabu, nyeusi na dhahabu; mistari ya dhahabu yenye ukubwa sawa na midogo kuliko rangi nyeusi ya kati.'

Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 22/04/1971, na kusainiwa na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere tarehe 06/05/1971, na kuanza kutumika tarehe 07/05/1971, ingawa kimsingi Bendera na Ngao zilianza kutumika rasmi tarehe 26/04/1964.

Je rangi hizo huweza kubainishwa vipi ili watumiaji waweze kuzitambua?

Kimsingi, ubainishaji wa rangi halisi za bendera hufanyika kwa kutumia msimbo wa rangi ama Colour Code. Katika muktadha huo, Tanzania ina msimbo wake wa rangi ambao haufanani na wa nchi nyingine yoyote duniani.

Kipekee, bendera ya Taifa ya Tanzania huongozwa na Msimbo wa Rangi (Colour Code) wa BS 2660:1955. Kirefu cha BS ni British Standard yaani Viwango vya Kingereza vinavyotumika katika rangi.

Msimbo BS 2660:1955 ndiyo unaotumika kuainisha usahihi wa rangi zote za Bendera ya Taifa ya Tanzania. Hivyo basi, ilitarajiwa kuwa hata jezi za timu ya taifa zitengenezwe kwa kuzingatia Msimbo wa Rangi wa BS 2660:1955. Sina hakika kama hilo lilifanyika.

Ninamini kuwa wataalamu wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali au Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali wanafahamu vema huo msimbo. Sina hakika kama watengenezaji wa jezi walipata ushauri wa kitaalamu kutoka huko.

Kutokana na hoja yangu hapo juu, ninapata shaka kwamba huenda msimbo wa rangi (Colour Code) uliotumika katika jezi za Timu ya Taifa unaweza ukawa hauakisi bendera ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mantiki hiyo, endapo msimbo uliotumika kuandaa jezi za timu ya Taifa utakuwa si BS 2660:1995, basi jezi hizo zinaweza kuwa si za Taifa Stars, huenda zinaweza kuwa kitu kingine ambacho hakiakisi rangi za bendera ya Taifa ya Tanzania.

1705070910886.jpg
 
Sio lazima ziendane na rangi ya bendera, ni uchaguzi tu wa rangi pendwa. Italy uwa wanavaa blue na hawana hio rangi kwenye bendera yao hata Holland rangi yao Orange na haipo kwa bendera yao.. Kwa kifupi bongo tuna bahati sana maana tunaweza vaa blue, kijani, njano, nyeusi na hata tukipendezwa nyeupe.
 
Manina hii nchi ina wajuaji sijawahi fikiria, hivi wew jamaa unajua mpira 🤔
Haya kama homework, katafute jersey za mataifa yafuatayo

South korea
Germany
Holland
Senegal
Ghana


Kisha njoo uone kama hio sheria yako ina apply ? Usijitie ujuaji sana
 
Huyo Samata wamemuweka hapo wa nini.

Mchango wake katika timu ya Taifa ni upi??
 
Msingi wa hoja yangu unakuja katika misingi ya kwamba, rangi za jezi za timu ya taifa huwakilisha bendera ya nchi husika.

Kwa mantiki hiyo, rangi za jezi za timu ya taifa ni sharti ziendane na rangi halisi za bendera ya nchi husika, vivyo hivyo kwa muktadha wa Tanzania.
Hili sharti ni la kweli ama labda ni jinsi unavyodhani wewe tu?
 
Back
Top Bottom