Tafakari juu ya nchi yetu Tanzania

komanyahenry

JF-Expert Member
Sep 15, 2017
903
1,352
Kwa mujibu wa Sheria namba 15 ya Bendera na Ngao ya Taifa ya mwaka 1971 imetoa maelezo ya namna bendela ya taifa inatakiwa kuwa pamoja na matumizi yake. Mpangilio wake ni kama ifuatavyo

Bendera itakuwa imegawanywa kwa pande 2 kutoka juu kushoto kwenda chini kulia nafasi ya juu itakuwa kijani na chini itakuwa blue zilizogawanywa kwa mistari midogo miwili ya rangi ya dhahabu ikiwa katikati kuna mstari mweusi mkubwa kidogo kuliko rangi ya dhahabu.

Sheria hii ikaendelea kuelezea juu ya maana ya rangi hizi, ikiwa rangi ya blue inawakilisha bahari, maziwa na mito, rangi ya kijani ni juu ya uoto wa asili uliopo nchini mwetu, rangi nyeusi ni Jamii ya watu waliopo Tanzania na rangi ya njano ni juu ya madini yanayipatikana Tanzania.

Tafakari yangu ni juu ya madini yanayopatikana ndani ya nchi yetu na kuwakilishwa na rangi ya njano kwenye bendera yetu. Wote tunajua kuwa madini huwa yanaisha, je ikitokea madini yanayopatikana ndani ya nchi yetu yakaisha, je kutakuwa na haja ya kubadilisha bendera yetu na kutoa mstari wa dhahabu? Na kama tutauacha kizazi kijacho hakutaona kuwa wazee wao tulikuwa wazembe kwa kuacha rasilimali zetu kuwanufaisha mabeberu?

tz.jpg
 
Back
Top Bottom