Roger Sterling
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 13,012
- 23,613
Frankly, hii naona kama ni story tu. 'HR' amekaa pembeni anaacha watu wanabishana issue ambazo angeweza kuzitolea ufafanuzi na conclussion ikapatikana kirahisi tu.
Barua ya kumsimamisha kazi (heading yake) inasemaje? Kwa sababu usije ukamdanganya Mr. wake akadai kopi au wanoko wameshampa kopi sasa anataka uthibitisho kutoka kwako maelezo yakapishana au mmewasimamisha bila maandishi? Eleza Mkuu
Hii inadhihirisha wake za watu hawako salama huko maofisini.
Pole kwa huu mtihani mgumu. Hilo la kumwambia ukweli mume liepuke hasa ukitilia maanani mke kishakupigia magoti umsitiri kwenye ndoa yake. Ila kama mume yumo humu ndio siri ya mkewe kuhusu kusimamishwa kazi imeshavuja.
Ndugu yangu, huyo mama hakufa kwamba sasa familia au mume apewe taarifa ni kitu gani kimesababisha kifo chake akiwa kazini. Yuko hai na anao wajibu wa kumueleza mumewe ni kwa nini amesimamishwa kazi, ofisi haina huo wajibu kwa mume. Period
Tiba
Wakuu nimefuatilia mawazo yenu kwa kina kwa kweli yana mchango mkubwa sana katika kuleta tija
Niseme tu kwamba kampuni yetu haiwajibiki kumjibu huyu mume Wa huyu mama ila pia haizuiliwi na taratibu zetu kufanya hivyo ni busara inayopaswa kutumika zaidi
Kama viongozi pia limetusumbua sana hadi kuhusisha mwanasheria Wa kampuni kutusaidia kulielewa hili, maana mume aliandika kwenye barua kwamba yeye ni mwakilishi Wa mkewe katika kesi hii ingawa hakutaka kusema yy ni mwanasheria au la
That's why nikampa tarehe ili tujadiliane ndani kupata mawazo zaidi maana anasema kuwa nanukuu. "" ninaiomba ofisi yako inipe Maelezo ya kina juu ya chanzo na sababu za kusimamishwa kazi mke wangu nikiwa kama mwakilishi wake na pia mumewe"" mwisho Wa kunukuu.
It is particularly on this phrase nikapata ugumu Wa kuilewa barua yake, kwamba mwakilishi maana yake nini hasa?
Katika sheria zetu yaani hr manual na company by laws inaeleza kuwa mfanyakazi anaweza kuwakilishwa katika kesi yake na mtu yeyote aliemteua anaeona anafaa
Na tumefanya hivi Mara nyingi hata kesi za fraud, hii ni kwa sababu wanawake wengi ikitokea ana matatizo huwa hawawezi kujieleza au kujisimamia hivyo wengi huwakilishwa na waume zao
Sasa ili mwanaume aweze kumwakilisha mkewe lazima ajue chanzo cha tatizo kwa kina unfortunately katika case hii chanzo ni uzinzi hivyo mkewe mwenyewe ameshaniambia hataki uwakilishi hataki mumewe ajiingize kwenye hili
Anasema hataki Ku fight hii case ni ya kuaibisha utu wake atakubali matokeo
Again hatuna wajibu Wa kumjibu mume lakini hatuzuiliwi kumjibu
Lakini naweza kuijibu barua yake kwa kumwambia hatuwezi kumjibu anachouliza Kutokana na sensitivity of the matter na hivyo kumshauri apate Maelezo kypitia mkewe, na kama ni mwakilishi wake kisheria ni lazima tuambiwe na mkewe
Yote kwa yote mke anaweza Ku fight hii case maana aliewashka ni mtu mmoja hana shahidi mwingine ila wazungu wenzie kwenye management wakamuamini moja kwa moja
Mbele ya safari wote wataitwa mbele ya disciplinary committee wakiwepo na fibuca chama cha wafanyakazi na wawakilishi wao kama wapo
Ingawa kwenye barua mwanamke alikiri kosa na kuomba msamaha mwanaume alikanusha hajashikwa amesingiziwa
Kikazi jambo hili linashughulikiwa kwa mujibu Wa taratibu nilichepuka pembeni kupata mawazo yenu ili kutenda haki
Mume sio sehemu ya ofisi ya mkewe na kwa maana hiyo hana haki ya kujua kwa nini mkewe kasimamishwa. Akitaka kujua sababu ya kusimamishwa amuulize mkewe na bwana caxton hana jukumu la kusitiri ndoa isiyomuhusu.
Kwa mke, kosa lake ni la kinidhamu zaidi, ingawa kwa mtazamo wangu sioni kama hilo ni kosa serious sana, kwani hawakusababisha aibu kwa ofisi (kosa halikufanyika sehemu ya public au mebele ya watumishi wengine) na wala halijaleta hasara kwa ofisi, isipokuwa tu ni curiosity ya huyu Canadian. Hivyo ofisi ndiyo yenye kuamua adhabu stahiki kulingana na uzito wa kosa.
Nadhani adhabu ya onyo kali inatosha zaidi hasa kwa vile tayari wanabeba aibu ya mambo yao kujulikana.
CC: caxton
ni mambo ya kiofisi hayamuhusu huyo mume wala ofisi hailazimiki kumjibu barua yake. sana unaweza kumwambie ni utovu wa nidhamu details amuulize mkewe.Call a spade a spade, fuata utaratibu wa ofisi.
Aisee hiki ni kisa na mkasa.Kusema ukweli wote tunahitaji kujifunza kutokana na tatizo hili maana kuna wakati waweza zidiwa na penzi ukajikuta unadai kumega ofisini na yakakukuta makubwa kama hawa wenzetu.Kama HR ni lazima uwe transparent.Sababu ya kufukuzwa huwa inaelezwa kwenye barua ya kusimamisha kazi au kufukuzwa kazi afterall,barua hiyo lazima ai sign boss wa kampuni yenu so the issue is straight forward endelea na taratibu za kiofisi mkuu.