Saharavoice
JF-Expert Member
- Aug 30, 2007
- 3,882
- 2,374
Sorry Umutwale,
Nimeiona, kumbe ni Kagasheki.
Nimeiona, kumbe ni Kagasheki.
Umutwale
Mbona linatajwa jina moja tu Wilson? ina maana ndiyo huyuhuyu masarafu?
Nakubaliana nawe Idimi kuhusu Mwakyusa hakujiuzulu wakati ule. Lakini bado namuona ni mtu asiye na kashfa na siyo mpenda ubilionea among the rest tulionao. ni suala la yeye kubadilika sasa na kuwajibika ipasavyo.
Nashauri pia JK aache ule utaratibu aliotumia wakati ule wa kuchomoa mawaziri kutoka kila mkoa. utaratibu huu haukuwa na manufaa yoyote kwa taifa zaidi ya kuingiza Mafisadi wengi serikalini. hatuitaji political balance, tunataka maendeleo that's all
Mie naona Pombe bado anatufaa kuwepo katika Baraza.Suala la nyumba kwa kweli alivuruga lakini tusisahau alikuwa chini Rais mwizi BMK. Inawezekana maagizo yalitoka kwa BMK au alitekeleza yeye Mwenyewe. Hapo alikosea lakini tunajua wazi hakuchukua pesa au kujiridhisha yeye.Tumsamehe kafanya mengi mazuri kuliko mabaya.
Huu mtindo wa mbunge kuwa waziri unapunguza sana uwigo wa kupata Mawaziri wachapakazi na waaminifu.Wengi wanaokuwa wabunge ndani ya CCM ni watu walele na ndo wanaotuibia na kutumia pesa kwa ajili ya kuchaguliwa kuwa wabunge then wapate nafasi ya uwaziri.Ni vizuri Serikali ikaacha kiburi, na kuruhusu marekebisho ya katiba.Kama ambavyo JK ameona kuwa haifai kuwa mfanya biashara na ukawa kiongozi wa serikari ndo hivyo hivyo haifai kuwa mbunge na kuwa waziri.Huwezi kuserve masters wawili kwa wakati mmoja.
Ningependa wafuatao wabakishwe kwenye wizara zao wamalizie visions zao:
1. Magufuli
2. Kawambwa
3. Tyson
4. Makongoro (awe waziri kamili)
5. Mama Sitta
6. Membe
7. Mary Nagu
8. Mwakyusa
9. Mwinyi
10. Maghembe
Maana kubadilisha badilisha within a short time nayo ina madhara ya mtu kushindwa ku achieve long run goals alizojiwekea.
* Msolwa na Mwandosya wanatakiwa wabadilishane wizara.
Chochonde JK mikorokocho ifuatayo ikaa bench pamoja na
" mabangusilo":
!. Chenge
2. Mramba
3. Mungai
4. Mwapachu
Wafuatao wapewe wizara:
1. Mwakyembe---Ushirikiano wa Africa Mashariki
2. Jenista Mhagama...Wanawake na Watoto
3. Ole Sendeka...Usalama wa Raia
Panga panga na wengine wenye uwezo wasio na harufu ya ufisadi
Sura Mpya aingie
Zitto , Lunyungu ,Kitila , Mwanakijiji, Mzee Es, Mwafike Jike , utaendeleza
Sijui Katiba ya Tanzania inasemaje, maana sijawahi hata iona...Naomba Msaada raisi anaruhusiwa kuchagua wabunge wapinzani kuingia kwenye baraza la mawaziri ? ama ni lazima watoke chama anachotoka raisi? Nilikuwa natamani Slaa achukue uwaziri wa Usalama wa Raia apambane na mafisadi na Zito achukue nafasi ya mama Zakia...
Jaribuni kubalance kwani inaonekana mnaipeleka nchi kwenye udini,uwiano uwepo ili kuondoa migongano ya kidini ,ni bora kama Waziri Mkuu Mkiristo ,Naibu awe muislamu hivyo hivyo kama Waziri Muislamu naibu awe Mkiristo ,kiasi kuweka kitu kinachoonesha uwiano flani ,Wakiristu wapo na waislamu wapo wanaoweza kushika nyadhifa hizo.Pia ikiwezekana wachukuliwe wasomi ambao wanathamini kazi za usomi wao kwa kile walichosomea na wameridhika na hali ya maisha waliyonayo naweza kusema wameridhika na umasikini wa nchi yao na hivyo hawatatumia vyeo vyao kujitajirisha binafsi zaidi watakuwa wafanyakazi wenye kufanya kazi kwa ajili ya kujenga Taifa lao na kuinua hali ya kipato cha wananchi ambao wanajumlisha wafanyakazi wakulima na waviwanda.
Nionavyo kumrudisha yeyote yule hata mdudu ambae wizara yake imekumbwa skendo basi kutamrudsha Mh.Kikwete katika ukurasa ule ule kwani wengine wamewekwa hapo na fadhila za hao walioondoka hivyo ulipaji wa fadhila utaivamia serikali ya Kikwete kwa rangi nyengine na kuwapa kazi wapinzani kup[iga mayowe.
Mimi naona mwisho wa Tanzania yangu ni kama Kenya.. badala ya chanzo kuwa Makabila kuna hatari itakuwa dini maanake madai mengi ynayoyaona ni sawa na yale ya Wajaluo!
Ni balance tu maana nikiangalia hapo kwenye mapendekezo sioni mabaniani wala masingasinga inafaa awepo Waziri wa Jamii ambae atakuwa ni mhusika wa wale wasio na dini au wenye hoja za kidini na kikabila ili zipate uwakilishi bungeni na kujadiliwa na wanataaluma mbalimbali.Hupaswi kuwa na hofu, mambo yote yataenda vizuri tu. Naamini tutaaendelea kuelimishana kwa hoja hadi tufikie mwafaka.
Angalia uzalendo wa mtu siyo madigrii yake; Professor Malima alikuwa na Ph.D. bila uzalendo. Sokoine alikuwa na uzalendo bila Ph.D. Je, ni nani kato yao alitufaa zaidi?
Angalia uzalendo wa mtu siyo madigrii yake; Professor Malima alikuwa na Ph.D. bila uzalendo. Sokoine alikuwa na uzalendo bila Ph.D. Je, ni nani kato yao alitufaa zaidi?
Logically hii kitu ya Kusema dini sii muhimu tusahau- mimi siafikiani nayo!
Kwa nini JK Hakuchagua Mwislamu??? Haingewezeka Rais, Mwakamu, na PM kuwa Waislamu!
Hata akipanga baraza la Mawaziri- dini pia anaconsier- haiwezekani eti mawaziri wote wawe Wakristo kwa kuwa tuu mradi tuwe na mtu mchapa kazi!
Tuyaongelee tu -wala tusifumbe macho- all the time maraisi ktk kuunda Cabineti tangu 1961 wamekuwa wanabalace kwa misingi ya mikoa, dini, jinsia na kadhalika!
Mauaji ya Mwembechai yametokea lini?... Mbona Sheikh Kassim bin JUmaa na baraza lake la waislaam walikuwa wanted wakati wa Mwinyi?..Nyerere yuko wapi hapa ikiwa muda wote wa Utawala wake hatukuwa na matatizo pamoja na kwamba mijadala ilikuwa ruksa!.
Nakuuliza tena JK ni muislaam anawasaidia nini waislaam?...
Huyo Mkapa, Lowassa na Sumaye waliokuwa wakristu waliwasaidia nini wakristu hata baada ya kuiba mabillioni?..
Jamani tume na upeo zaidi ya vitu hivi kwani JF ni uwanja mpana zaidi ya kufikiria ndani ya sanduku la udini.