Tumezungukwa na majirani wanaotuangusha sana, yaani uchumi wa EAC yote ukijumuishwa haukaribii wa Nigeria

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,752
48,646
Sijui shida nini haswa, ilhali raslimali nyingi tu za kumwaga....

mmexport1651920532378-png.2215157
 
Kilichowapaisha Nigeria ni mafuta, ila hilo halifai kuwa kisingizio. Hapa EAC tunakwazwa na siasa duni na elimu duni pia. Wengi wa viongozi ambao tunawachagua hawataki kabisa kubadilika na nyakati. Miaka nenda miaka rudi wapo pale pale, wakifanya vitu vya kipumbavu.

Naona Kenya licha ya kukosa rasilimali nyingi, tofauti na wenzetu, bado tunachangia zaidi ya 1/3 ya uchumi wote wa jumuiya ya AM. Nchi moja tu kati ya saba! Kenya hoyeee! 🇰🇪🇰🇪🇰🇪
 
Naona baada ya muda mrefu wa zile tantarira zako za kiccm, za sijui kuongoza kwenye ukuaji wa uchumi barani Afrika. Mara sijui dona kantrii na maupuuzi mengine, sasa hivi umeishia tu kwenye memes. Kwa huu mziki wa Kenya kiuchumi, jombaa hauni budi isipokuwa tu kukata kiuno. Bado mpo mpo tu mnachezea kwenye GDP ya $70s Bil, licha ya kuimba mamia ya chorus za sifa na mapambio kwa miaka kadhaa.
 
Lakini Nigeria ina watu > 200 million, dumber!
Ndio maana per capita, income, yao(pato la mtu mmoja mmoja kwa mwaka) @ 2,335 inakaribia ya Kenya, @ 2,251, licha ya wao kutuzidia kwenye GDP. Wamezidiwa sana na Egypt, S.Africa pia kwa mbali, @ 4,162 na 6,978 mtawalia. Kisa zama zile wao pia walifata mawaidha ya 'Jiwe' lao, kwamba wazaane kabisa, kwa raha zao, bila breki.
 
Ndio maana per capita, income, yao(pato la mtu mmoja mmoja kwa mwaka) @ 2, 335 inakaribia ya Kenya, @ 2,251, licha ya wao kutuzidia kwenye GDP. Wamezidiwa sana na Egypt, S.Africa pia kwa mbali, @ 4162 na 6,978 mtawalia. Kisa zama zile wao pia walifata mawaidha ya 'Jiwe' lao, kwamba wazaane kabisa, kwa raha zao bila

Umemuelewa mleta mada lakini anachoongelea ?
 
Ndio jombaa, wewe hujamuelewa au? Usiishie tu kwenye kusoma kichwa cha mada yake na sentensi moja hiyo, aliyotangulia nayo. Usipende kutafuniwa, alafu eti ndio ungoje tu kumeza. Jichambulie mwenyewe hizo takwimu, ukianza hapo katikati ya nambari tatu na nne. Ok?
 
“Uchumi wa EAC yote ukijumuishwa haukaribii wa Nigeria”, haya nifafanulie alikiwa anamaanisha nini ?
 
Acha zako wewe, kama hukumuelewa na hizo takwimu pia hukuzielewa basi tusisumbuane. Maanake tutakuwa tunajadili vitu ambavyo havina tija kabisa.
 
Ndio maana per capita, income, yao(pato la mtu mmoja mmoja kwa mwaka) @ 2,335 inakaribia ya Kenya, @ 2,251, licha ya wao kutuzidia kwenye GDP. Wamezidiwa sana na Egypt, S.Africa pia kwa mbali, @ 4,162 na 6,978 mtawalia. Kisa zama zile wao pia walifata mawaidha ya 'Jiwe' lao, kwamba wazaane kabisa, kwa raha zao, bila breki.
Umepoteza mantiki baada ya kumuhusisha Jiwe, yuke alikuwa laana ya Taifa
 
Acha zako wewe, kama hukumuelewa na hizo takwimu pia hukuzielewa basi tusisumbuane. Maanake tutakuwa tunajadili vitu ambavyo havina tija kabisa.

Kila kitu kinakinzana, kama ameongelea per capital siyo kweli kwamba per capital ya Nigeria ni kubwa kuliko EAC yote kwa ujumla, sasa alimaanisha nini ? Uchumi gani wa Nigeria aliomaanisha ambao ni zaidi ya EAC?
 
Funny thins is Nigeria has a GDP of $500b closer to Turkey with $700b
But comparing Nigeria with Turkey is like hell and heaven. GDP ya Mchongo, kama ya Kenya
 
Vipi kuhusu GDP, mbona unajitia hamnazo kuhusu hilo? Au hujui kwamba hiyo per capita income inapatikana kutoka kwa GDP Nominal/Idadi ya watu? 😆 'Denialism' ni sawa tu na ugonjwa sugu. Badala ya kujikita kwenye kujadili maswala kama yalivyo, wewe unatumia nguvu nyingi sana kutafuta pa kupenyezea visingizio.
 
Unafananisha uchumi wa Nigeria na Turkey, wakati umesema mwenyewe hapo kwamba tofauti kati ya GDP zao ni karibia $200B? Hivi nyie mmefikia hata nusu tu ya hiyo $200B ndio uipuuze?
 
Sijui shida nini haswa, ilhali raslimali nyingi tu za kumwaga....

mmexport1651920532378-png.2215157
Bro kwani Nigeria imesaidiwa na majirani? Unataka uwe uchumi wa Nigeria vs East Africa? Kwanini isiwe Kenya vs Nigeria kama mnavyofanya Twitter? Mnajibinua midomo kupambana na Nigeria huko Twitter, kumbe hamna kitu. Pambana na hali yako.
 
Vipi kuhusu GDP, mbona unajitia hamnazo kuhusu hilo? Au hujui kwamba hiyo per capita income inapatikana kutoka kwa GDP Nominal/Idadi ya watu? 😆 'Denialism' ni sawa tu na ugonjwa sugu. Badala ya kujikita kwenye kujadili maswala kama yalivyo, wewe unatumia nguvu nyingi sana kutafuta pa kupenyezea visingizio.

Ndo maana ukisoma andiko langu la kwanza nimeandika “lakini Nigeria ina watu zaidi ya milioni 200”
ambayo ni namba kubwa kuliko EAC tena kwa mbali sana, sasa cha ajabu nini nchi yenye Watu zaidi milioni 200 kuwa na gdp kubwa klk EAC yenye watu wachache? Kama angesema Afrika Kusini kuwa na uchumi mkubwa kuliko EAC yote hiyo ni sawa ingejadilika kwa maana AK ina watu kama milioni 60 tu, …
 
GDP ambayo ndio huwa inazungumziwa, tunaposema uchumi wa nchi fulani, ni pato la taifa jombaa. Pato la taifa ni thamani ya sokoni ya bidhaa na huduma zote za nchi fulani katika mwaka. Haijumuishi hayo unayoyazungumzia, kuhusu idadi ya watu. Idadi iwe ndogo au kubwa sio ishu na idadi ya watu ikiwa ya juu, haimaanishi kwamba GDP itakuwa hivyo hivyo.

Ulipotaja kuhusu idadi ya watu sikubisha, ndio maana nilikutajia per capita income nilipokunukuu. Nadhani sasa tumeelewana.
 
Back
Top Bottom