Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,755
- Thread starter
- #81
Bila kuwasahau Sambulumaa Band na Marquiz du Zaire(wana Sendema)...Mambo ya Marquiz eeeh,mwasemaje ,Sendema...twende mbele sendema,rudi nyuma sendema,kushoto kulia sendema,sendema,sendema ya moto,hawa Marquiz walikuwa wazuri sana wakuu,walikuwa wanaujua muziki hasa...Nawakumbuka wanamuziki wao mahiri kama Tshimanga Kalala Assosa 'Mutoto Muzuri'(huyu baadaye alijitoa akaenda kuanzisha bendi ya Legho Stars akiwa na akina Anania Ngoriga wakatoa kibao kitamu cha Francisca-jamani makubwaa yamenipataa,sijui nifanyeje Francisca,ukimuona huko aliko muelezeni kweli nampenda,nafasi yake bado iko rohoni mwangu,oooh ngulupamba Francisca)..,Mbuya Makonga 'Adios',Banza Mchafu,Fredito Butamu,Bobo Sukari,Vumbi Dekula Kahanga,Kassongo Mpinda Clayton bila kumsahau baba yao Chinyama Chiyaza