Tumetoka mbali: Unawakumbuka watu hawa na mambo haya?

Bila kuwasahau Sambulumaa Band na Marquiz du Zaire(wana Sendema)...Mambo ya Marquiz eeeh,mwasemaje ,Sendema...twende mbele sendema,rudi nyuma sendema,kushoto kulia sendema,sendema,sendema ya moto,hawa Marquiz walikuwa wazuri sana wakuu,walikuwa wanaujua muziki hasa...Nawakumbuka wanamuziki wao mahiri kama Tshimanga Kalala Assosa 'Mutoto Muzuri'(huyu baadaye alijitoa akaenda kuanzisha bendi ya Legho Stars akiwa na akina Anania Ngoriga wakatoa kibao kitamu cha Francisca-jamani makubwaa yamenipataa,sijui nifanyeje Francisca,ukimuona huko aliko muelezeni kweli nampenda,nafasi yake bado iko rohoni mwangu,oooh ngulupamba Francisca)..,Mbuya Makonga 'Adios',Banza Mchafu,Fredito Butamu,Bobo Sukari,Vumbi Dekula Kahanga,Kassongo Mpinda Clayton bila kumsahau baba yao Chinyama Chiyaza
 
Kulikuwa na kina Power Mabula, Power Vuru Mroma, Power Chaka Zulu, Power Tarzan, usahau Muungano kibisa Troupe na majoka yao, DDC Kibisa na enzi hizo maprofesa wa mazingaombwe kibao wanakuja mashuleni
 
kulikuwa na timu ya nyota nyekundu(red star) kina steven chibichi, kibingwa, maohamed nyauba na kina ayubu mzee
 
Msada tutani.... kwani nini Ali.. au kama anavyojulikana TX mishi william alipachikwa jina hili la Tx moshi william.. anayejua msaada
 
Bila kuwasahau Sambulumaa Band na Marquiz du Zaire(wana Sendema)...Mambo ya Marquiz eeeh,mwasemaje ,Sendema...twende mbele sendema,rudi nyuma sendema,kushoto kulia sendema,sendema,sendema ya moto,hawa Marquiz walikuwa wazuri sana wakuu,walikuwa wanaujua muziki hasa...Nawakumbuka wanamuziki wao mahiri kama Tshimanga Kalala Assosa 'Mutoto Muzuri'(huyu baadaye alijitoa akaenda kuanzisha bendi ya Legho Stars akiwa na akina Anania Ngoriga wakatoa kibao kitamu cha Francisca-jamani makubwaa yamenipataa,sijui nifanyeje Francisca,ukimuona huko aliko muelezeni kweli nampenda,nafasi yake bado iko rohoni mwangu,oooh ngulupamba Francisca)..,Mbuya Makonga 'Adios',Banza Mchafu,Fredito Butamu,Bobo Sukari,Vumbi Dekula Kahanga,Kassongo Mpinda Clayton bila kumsahau baba yao Chinyama Chiyaza

Kamanda, nimekukubali! Wewe ni moto wakuotea mbali kwa kumbukumbu. Daah, ee bwanae!
 
Halafu magazeti yalikuwepo Uhuru,Daily News,Mzalendo&Sunday News(Jumapili) bila kuyasahau yale yaliyotoka mara moja kwa wiki kama Mfanyakazi na Kiongozi...Baadae likaja gazeti la Motomoto(sijui lilifia wapi hili,lilikuwa na habari motomoto kweli) na magazeti kama Heko na Rai...Kwenye majarida lilikuwepo Sani bwana chini ya mtaalamu wa kuchora hayati John Kaduma(huyu bwana alikuwa na kipaji hasa)..Pia kuna Riwaya moja ilikuwepo kwenye gazeti la Sani iliyoitwa MAJI MAZITO mtunzi akiwa ni hayati Said M. Bawji,hii Riwaya ilikuwa si mchezo wakuu(wahusika wa riwaya walikuwa ni Omari Kissila-Ommy Kiss,dada Vicky na mzee Dickson Zakwa Mkongwe),mnaikumbuka Riwaya hii????dah!!!!!!!!!

Kwa kweli Mkuu unakumbuka sana tena kwenye kulikuwa na vijarida vingi vingine vya hadithi ingawa watunzi wake siwakumbuki kama panga la shapa alivyokuwa anawatapeli wanawake waliokuwa wanakwenda kutafuta dawa ya mapenzi, vingine kama pinokyopia kuna vijitabu vidogovidogo vya hadithi ambayo nakumbuka wakati niko shule ya msingi niliwahi kuvisoma vyenye hadhithi kama hanahela, mpiga filimbi wa mahelin(mzee wa mapnya)achilia mbali za akina juma na roza, adili na nduguze hadithi za bahari nyeusi, waridi, nyoka mwenye vichwa kumi na mbili, tuanze lini, usiku wa balaa, unyoya wa kipanga azizi, alfulela ulea, n.k wa kadhalika, kweli tumetoka mbali si rahisi enzi hizo kurudi kwa sababu kizazi cha sasa ni cha tv na compyuta. sio cha kucheza parade shuleni, kukimbia mchakamchaka asubuhi, kutembea kwa miguu kwenda shule asubuhi, sidhani kama wanacheza mdako, rede, uki, kuruka kamba, combolea nk. zamani ukikaa na bibi anakusimulia hadithi za akina akilikufundishwa nk. lakini siku hizi watoto hawakai na bibi zao hakuna wa kuwasimlia hadithi hivyo wato kupenda udadisi wa kusoma vitabu inakuwa kidogo sana anachowaza akitoka shule ni kuchegame kwenye tv, computa, kuangalia movie basi na kulala.
 
enzi za mwalimu kulikuwa na wababe. kulikuwa kunajulikana kabsaa mtemi wa mtaa ni nani, ukienda shule utasikia flani anapiga darasa zima kuna wa pili hapo, watatu na kuendelea, haya kuna mbabe wa shule nzima, huyo mpaka walimu walikuwa wanamuogopa. mwingine utasikia anapiga mkoa mzima tehe kwenye madisco haguswi huyo. miaka ya mwisho ya themanini na mwanzo mwanzo wa miaka ya tisini kuna jamaa pale iringa alikuwa anaitwa cool nine ndo alikuwa anaaminika pale iringa town yote alikuwa mbabe

halafu mchezo wa shule ya msingi wa kuwekeana wanted ukimchokoza mwenzio anakuwekea wanted siku ya kufunga shule anakuvizia akupige. au saa ya kutoka darasana mnakwenda mbali na shule kupimana nguvu mstari unachorwa katikati halafu mmoja anachukua mchanga wale wanaopigana kila mmoja anapiga ule mchanga kuonyesha kuwa huogopi then mnaanza kukunjana. jamani!!!
 
Hii nayo inanikuna sana mwenzenu jamani, Mzee mzima Gurumo huyu

Celina - Mlimani Park Orchestra
Najua najua una mawazo
Lakini tutafanyaje ikiwa wazazi wako wameamua hivyo
Nia yangu na madhumuni yangu ......
Ilikuwa tufunge ndoa na tuishi sote kama mke na mume Celina
Nimejitahidi kadili ya uwezo wangu
Wazazi wako wameniwekea vikwazo vingi.....
Nimejitahidi kadili ya uwezo wangu
Wazazi wako wameniwekea vikwazo vingi.....
Gurumo
Celina aaaa.......

Oo Celina piga konde moyo oo Celina......
Oo Celina utafanikiwa oo Celina......
Gurumo; na kwa sababu imekuwa hivyo Celina aa
Sioni haja ya kutaka UJIUE kwa ajili yangu ...
Oo Celina piga konde moyo oo Celina......
Oo Celina utafanikiwa oo Celina......

Gurumo; Na kwa sababu imekuwa hivyo Celina aa
Sioni haja ya kutaka UJICHINJE kwa ajili yangu ...http://www.angelfire.com/linux/tizedboy/mlimani.htm#[Mwanzo]

Aisee!..Asante sana kaka,umenikumbusha mbali sana yaani...dah!!!!
 
Mkuu Balantanda nimekukubali wewe una kumbukumbu, umenikumbusha mbali sana wengine hawa pia walikuwepo Niko Zengekala, Kawelee Mutimwana, mafumu Billal "Bombenga" Zahir Ally"Zohro", Amani Ngenzi, Kibambe Ramadhani, Vumbi Dekula Kahamba,
Dingituka Molay na wengineo wengi.Safi sana Mkuu.
 
Christina Bundala - Mlimani

Max Bushoke naye kazi zake naona mwanaye tena kaurudia kwenye bongo fleva lakini hausikiliziki utamua wake upo kwenye ile original wazee

Ama kweli penzi jamani halikadiriki
Hata ulipime na mzani gani
Benno Villa; Nililichezea kamari pendo lake Christina
Na kujisahau kama lingenifaa na kudumu maishani mwangu

wote; Nililichezea kamari pendo lake na kuuza utu wangu
Kwa wasio thamini penzi wala kujua maana ya kupendwa

Gurumo; Kwa kweli Mpenzi Christina leo naomba unisamehe
Nitunze uniongoze kwenye penzi lako la haki

Gurumo; Nilihadaishwa na anasa za dunia
Kwa kweli Binadamu hujifunza kutokana na makosa
 
Gama hiyo...................

Afadhali pia ungenieleza makosa niliyokutenda yoo we Gama
Kabla hujaamua kuniachaaaaa
Ulilazwa hospitali miezi mitatu, miezi sita masomoni yote nimevumilia eee

Unataka upendwe vipi yooo we kaka?
Unataka upendwe vipi yooo we GAMA

(Chorus)
[Wote]Naomba unisamehe we kaka
[Mmoja] Nani atawaelea
[Wote]Naomba unihurumie we kaka
 
Hata Mwezi Bado - Chidumule huyu na sasa ni mwimbaji wa nyimbo za injili tu duh enzi hizo jamani na redio moja tu RTD

Hata mwezi bado oooo, tangu tuoane ee
Kelele kila siku ndani ya nyumba yetu mama
Benno VILLA; Ninaporudi kazini majirani huzima redio
Ili wasikize tunavyogombana
Wametupachika majina wewe Pwagu na mimi Pwaguzi
Kwa vile imekua ni mazoea
Ingawa nimekuoa kwa pesa na pendo langu ee
Tabia zako zimenishinda ooo nasikitika
 
MAMA FELLY HIYO NAYO WAZEE TUIKUMBUKE

Nina langu jambo linalonikera moyoni
Kidogo, kidogo...................

Nimevumilia lakini roho inauma aa
Umeanza kwa ndugu zako
Kuyafikisha malalamiko yako
Eti nina mpango wa kuoa mke mwingine
Wazo hilo sina mama

Lakini leo naona kama una lako jambo........

Tumetoka mbali eeee Mama Felly ooo
Yatupasa tukumbuke kulea watoto
Ili nao wajidai mbele ya wenzao
Baba yetu na Mama wapo kama sisi tunavyosema......
Chidumule; Kumbuka furaha ya watoto ni fahari kwa wazazi ee
Kumbuka furaha ya Doto na Kulwa fahari kwetu mama
Tukitengana ....tutawapa ukiwa bure
Tukitengana nawe tutawapa mateso watoto wetu
 
Mzuzu unatisha mkuu,kweli unadhihirisha kwamba wewe ulikuwa ni Nginde damu,safi sana kaka
 
Mkuu Balantanda nimekukubali wewe una kumbukumbu, umenikumbusha mbali sana wengine hawa pia walikuwepo Niko Zengekala, Kawelee Mutimwana, mafumu Billal "Bombenga" Zahir Ally"Zohro", Amani Ngenzi, Kibambe Ramadhani, Vumbi Dekula Kahamba,
Dingituka Molay na wengineo wengi.Safi sana Mkuu.

Kaka umemtaja Nico Zengekala umenifanya nikumbuke nyimbo za Jacky na Solemba.Hebu cheki mashairi matamu haya ya wimbo Jacky:

Mtoto Jackiee,mtoto wa Nirobi
Ingawa ni mara ya kwanza mimi nawe Jackiee
Tulipokutana palee Kampala kwenda Nairobi
Tulifurahiana sana kama tuliishi mwaka
Tabia yako njema kweli sitoisahau.

Mtotoo Jackie,mtoto wa mama Jackie wa mapendo
Japokuwa tuliachana stendi ukielekea Nairobi nyumbani eeh
Lakini tutakutana,nitakuja kutembelea,nawe karibu nyumbani eeh
Ooh Jackie yeyeeeh

Mtoto wa mama Jackie wa mapendo
Japokuwa tuliachana stendi,ukielekea Nairobi nyumbani eeh
LAkini tutakutana,nitakuja kutembelea,nawe karibu nyumbani eeh
Ooh Jackie yeyeeeh

Kiitikio:

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau lakini nashindwa
Hasa ni ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Nimejaribu kukusahau lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua eeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Sauti yako nyororo inaniua sana na mwendo wako wa maringo unanikondesha mamaaah,ayoleli mwanamama nakuwinda sana Jackie yeyeyeeeh mwanamamaah aeaeeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Mvumilivu hula mbivu,Jacki yeyeeeh,mvumilivu hula mbivu Jackie yeyeeeh
Jaribu kuvumilia yeeh tutaonana mamaah kama sio Kampala ni Tanzania mamaa
Jackie yeyeyeeh mwanamama aeaeeh

Mtoto Jackie eeh,mpenzi wangu najaribu kukusahau,lakini nashindwa,hasa ni kwa ile ndoto inayonisumbua naota unaniletea kifuko cha DHAMBARAU

Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Nitakuja Nairobi eeh nikuone mamaah
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Tutafurahi pamoja mi na wewe mama yeeh
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
Jackie yeyeyeeh Maneno sema na yeye
Jackie yeyeyeeh nitakuja Nairobi
 
Msada tutani.... kwani nini Ali.. au kama anavyojulikana TX mishi william alipachikwa jina hili la Tx moshi william.. anayejua msaada

Aulizwe mzee Kassim Mapili,yeye alikuwa na TX Polisi Jazz ambako ndiko jina la TX Moshi William lilianzia.Ila mimi nadhani alipewa hilo TX kutokana na utaalamu wake wa kutunga na kuimba(Sijui hilo la Moshi William lilitoka wapi sasa) si unakumbuka kipindi kile kuna magari yalikuwa na vibao vya namba vilivyoanza na TX(Tanzania Experts???).........
 
Bila kuwasahau Sambulumaa Band na Marquiz du Zaire(wana Sendema)...Mambo ya Marquiz eeeh,mwasemaje ,Sendema...twende mbele sendema,rudi nyuma sendema,kushoto kulia sendema,sendema,sendema ya moto,hawa Marquiz walikuwa wazuri sana wakuu,walikuwa wanaujua muziki hasa...Nawakumbuka wanamuziki wao mahiri kama Tshimanga Kalala Assosa 'Mutoto Muzuri'(huyu baadaye alijitoa akaenda kuanzisha bendi ya Legho Stars akiwa na akina Anania Ngoriga wakatoa kibao kitamu cha Francisca-jamani makubwaa yamenipataa,sijui nifanyeje Francisca,ukimuona huko aliko muelezeni kweli nampenda,nafasi yake bado iko rohoni mwangu,oooh ngulupamba Francisca)..,Mbuya Makonga 'Adios',Banza Mchafu,Fredito Butamu,Bobo Sukari,Vumbi Dekula Kahanga,Kassongo Mpinda Clayton bila kumsahau baba yao Chinyama Chiyaza

Hapo umenikumbusha na kumbi za muziki za enzi hizo, Lang'ata Kinondoni,DDC Kariakoo/Magomeni Kondoa,Amana Ilala, Ruaha Mpaka Maputo-Ukonga Majumba sita,White House Kimara,Safari Resort,Imasco temeke,Msasani Beach,Rungwe Oceanic,Africana,Bahari Beach,Club 92- Ubungo,New Africa ghorofa ya Saba-Ngoma za Maghorofani-MK group,etc.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom