Tumenunua mitambo ya gesi ya kuzalisha umeme, wakati hatuna gesi ya kuendesha

sirghanam

JF-Expert Member
May 29, 2009
284
92
HAYA YAMESEMWA NA MGURUGENZI WA SONGAS KAMA ALIVYONUKULIWA NA GAZETI LA MWANANCHI

"Mahitaji ya gesi ni makubwa kutokana na kuongezeka kwa matumizi yake na kwa sababub hiyo hata hiyo mitambo ya megawati 100 ambayo serikali imeinunua haitapata gesi na hakuna njia ya haraka kuweza kutatua tatizo hili," alisema Mkurugenzi huyo.


MGURUGENZI HUYO ALIENDELEA KUISHAURI SERIKALI KWA KUSEMA

Ford alisema kwa msingi huo, serikali inapaswa kutafuta njia mbadala ya kuzalisha umeme na si kwa kutegemea gesi.Mkurugenzi huyo alisema mpango uliopo kwa sasa ni kujenga kituo kingine cha kusafisha gesi kitakachogharimu zaidi ya Dola 170 billioni za Marekani na kwamba kazi hiyo itachukuwa zaidi ya miezi 18 kukamilika.

SASA NITAKUWA NA KOSA GANI KUHOJI UWEZO WA WATAALAMU WETU NA VIONGOZI WETU WA SERIKALI.. Na nina kuhakikishia hakuna mtu atawajibika ama kuwajibishwa kwa uzembe huu.. NA ATATOKEA KIONGOZI MMOJA MKUBWA SERIKALI ATAMTETEA ALIYEISHAURI SERIKALI KUNUNUA MTAMBO HUU BILA KUFANYA UTAFITI WA KUTOSHA...
Hii ndio Tanzania yangu..
 
nini gesi kwangu transfoma limelipuka wiki sasa kila siku tunapewa story, tushasahau umeme unafananaje
 
kitu kinachoniudhi ndugu zangu,ni kwamba gesi tuliyojaliwa nayo,imewasaidia watu wachache.Kwa miaka takriban 17 hii gesi imekuwa ikiwanufaisha watu wa daraja fulani ambao ni wachache kulinganisha na watanzania wengi vijijini.What a shame!!....we don't need that sh!t take it back!
 
Yaani ni mchezo wa kuigiza tu, Kama Isidingo vile kila siku vimbwanga vipyaaa. kweli hatuna serikali
 
Back
Top Bottom