radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,427
- 32,196
Imefikia hatua usipojikomba kwa viongozi wa nchi, unaonekana hufanyi kazi na sio mzalendo. Unaweza kupoteza Utaifa wako usipojikomba na kusifia.
Tumekua watu wa kuabudu mambo ambayo unaona kabisa hayapo sawa lakini tunaaminisha ngazi za juu mambo yapo sawa nani anateswa? Mtawala au tabaka tawaliwa? Anafurahishwa nani mwajiri au mwajiriwa?
Nini hatma ya Taifa na hii tabia inayoua taaluma za watu kwa kujikomba na kujipendekeza?
Imefika hatua kiongozi mkubwa toka taasisi nyeti anasema wizi hakuna serikalini ina maana ripoti za CAG zinadanganya? Kazi ya CAG haipo?
Tutafakari kama Taifa na hii aibu inayoangamiza Taifa ina hama kizazi hadi kizazi
Mwisho tunajenga Taifa la hovyo
Nini kifanyike Watanzania wenzangu na hii aibu?