Maisha tunayoishi Watanzania na Waafrika ni aibu tupu

professional ethics

Senior Member
Dec 24, 2023
108
352
Maisha ambayo raia wa Africa na Tanzania kwa ujumla tunaishi ni aibu, huzuni na mateso matupu. Maji shida, umeme shida, ajira hakuna, huduma za afya mbovu Yani Kila kitu tatizo.

Waafrika na Tanzania kwa ujumla tunaishi katika umaskini wa kunuka ndani ya utajiri wa kutupwa. Hakika hii ni laaana!

Waafrica wanajua chuki, roho mbaya, uchawi na husuda, hakika hii ni laaana.

Laaana! Laaana! Laaana ! Hakika Africa Ina laana ya kudumu.

SWALI LA MSINGI KIPI KIFANYIKE KUONDOA LAANA HII

Binafsi, laana ya Tanzania na bara la Afrika itaondolewa na walimu tu, walimu pekee na sio wachungaji Wala ma-sheik, ni wakati sasa serikali za Africa na Tanzania kwa ujumla kulitazama kundi Hili la walimu kwa jicho la tatu

NINI MSINGI WA KUSEMA HAYA

Laana ya Tanzania na Africa inasababishwa na philosophy problem, matatizo ya kimaaadili yaani ethics issues, na ukosefu wa uzalendo. Walimu pekee ndio Wana jukumu la kushape tabia za wanafunzi ambao badae ndio watawala na raia wa kesho.

Falsafa ya mwalimu ni falsafa ya wanafunzi, na falsafa ya wanafunzi ni falsafa ya taifa.

Serikali ya Tanzania, wizi huu, huduma mbovu za jamii kama maji, umeme na afya, tiba yake ni moja tu kutengeneza mazingira Bora ya walimu na motisha ili walimu wa impart falsafa chanya kwa wanafunzi na hatimae laaana hii itutoke.


Wenu mtiifu, Wana Duce mwaka wa tatu bachelor of science with education.
 
Yan wew ndio kama kawaida umeendelea na mchezo uliotufikisha Africa hapa, Blaming game 😂😂 kwamba leo jukumu apewe Mwalimu, na sio jukumu la raia wote kuanzia wazazi, kaka, dada, wajomba wote kuhakikisha tunatengeneza watoto wenye maadili na kulipenda taifa, ilq unakimbilia kusema kazi iachwe kwa walimu, 😂😂
Mchezo wa kutaka tufanyiwe na wengine ndio umetufikisha hapa
 
Watanzania tunapenda kujadili mambo mepesi mepesi kama vile unga umepanda au sukari ni mara chache sana kuona watu wakijadili kuhusu ubovu wa elimu tunayoendelea kuwapa vijana wetu huko chuoni na mwisho wanarudi mtaani kuwa bodaboda au machinga tunashindwa kuendelea sababu tuna elimu inayo toa ujinga na sio kitupa maarifa
 
Back
Top Bottom