Tume kuhamia Zanzibar kukusanya maoni

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
314.jpg




Tume inayoratibu mabadiliko ya katiba inatarajia kukutana na wajumbe kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili kupokea maoni yao kuhusiana na katiba mpya.

Tume hiyo katika taarifa yake imedaiwa mwishioni mwa wiki hii
itakutana na wawakilishi hao

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume hiyo, Assaa Rashid, ilisema wajumbe hao wote kwa pamoja watakutana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mjini Zanzibar.

Baadae tume hizo zitakwenda kukutana na vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia ikiwemo na makundi mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kupata maoni yao na kuyajumlisha.

Tayari tume hiyo imeshatembelea mikoa ipatayo 16 na kukutana na wananchi wa makundi mbalimbali kukusanya mabadiliko hayo.
 
Back
Top Bottom