Tuliosoma nje ya nchi tunanyanyapaliwa sana

Uzoefu labda
Muda uko nje wenzio wamepata uzoefu

Usichukulie kusoma nje ndo kila kitu
Una conclude kirahisi tu. Una majibu kichwani.
Hii mada imewagusa pabaya. Maana mnaongea tu bila kujali upande wa pili.
 
Kuna miaka ukipata div. 4 uganda unaingia advance wakati huku unaonekana kilaza. Kuna jamaa yangu akipata div. 4 akapelekwa kuendelea na shule uganda alivyomaliza akawnde chuo Maresia sasa hivi analima matikitiki shamba la babake bagamoyo kila taasisi na serkalini akienda hola wanaishia kuchukua wabongo tu anaonekana kilaza.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
Hiko chuo Maresia kiko nchi gani?
 
Kuna miaka ukipata div. 4 uganda unaingia advance wakati huku unaonekana kilaza. Kuna jamaa yangu akipata div. 4 akapelekwa kuendelea na shule uganda alivyomaliza akawnde chuo Maresia sasa hivi analima matikitiki shamba la babake bagamoyo kila taasisi na serkalini akienda hola wanaishia kuchukua wabongo tu anaonekana kilaza.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
Analima shamba la matikiti la Baba ake
 
Umesoma chuo ada milioni 20 kwa mwaka ,unakuja bongo kwenye kazi ya laki 8 kwa mwezi ,huo ni ufala,bakini hukohuko

Yaani hapo ndipo naposhindwa kuelewa. Mtu anapataje nguvu ya kurudi kufanya kazi TZ ilhali hakuna kampuni yenye hadhi ya kumlipa kwa kitu alichokisomea huko ughaibuni.
 
Sasa mkuu kama mimi na CBG yangu na shahada yangu ya kilimo hapo morogoro, hilo neno hapo juu nimelikoleza rangi ni compulsory na siyo compursory kama ulivyoandika wewe.

Sina budi kusema kuwa uhakiki uendelee kwa sababu kuna mapungufu kwa baadhi yenu.

Vipi kozi yako inakubali kuomba kazi hapo ajira portal?
Thanks nilikosea, kozi yangu achana nayo kwa sasa, nikija nitakutafuta...lol
 
Sasa mkuu kama mimi na CBG yangu na shahada yangu ya kilimo hapo morogoro, hilo neno hapo juu nimelikoleza rangi ni compulsory na siyo compursory kama ulivyoandika wewe.

Sina budi kusema kuwa uhakiki uendelee kwa sababu kuna mapungufu kwa baadhi yenu.

Vipi kozi yako inakubali kuomba kazi hapo ajira portal?
Mkuu umepiga kwenye mshono ujue
 
Kuna wakuu wanaona ni sawa tu. Ukigusa utaratibu huo wa kulipia au ukilalamikia mlolongo wa TCU wabongo ni wakali kama pilipili. Usiguse TCU. Teseka nayo tu maana wanasema ni kiherehere gani kilikutuma kusoma nje. Kwenye andiko langu sikutaka kugusia huo utaratibu wa TCU kwa kuusema ni mbovu maana najua ningeshambuliwa kama nyuki.
Nje wewe ndo wa kwanza kusoma?wacha porojo!
 
Mliondoka mkiwa hamna qualification mkaenda kusoma vyuo vya uchochoroni ambavyo havitambuliki mkirudi mnataka muajiriwe serikalini, duuuu!
 
Yani kuna watu wengine ni hopeless sana ukipata nafasi ya kusoma nje hutakiwi kufanya kazi ya serikali unatakiwa hata ukapige kazi nchi za watu huko kama ni South Africa, USA au Europe ule mema ya dunia sasa umesoma huko kote unakuja kuhagaika na ajira portal haijalishi umelipiwa ada na mzazi au umekua sponsored
Mkuu unataka kusema elimu ni about knowledge not know-who au?
 
Yap yap (DASP) ,Hahahaha, mkuu saizi ni mpambano wa kukata na shoka, wasomi wengi nafasi chache...
Usijali, utapata tu, ukiona hupati jaribu kujisogeza may be hapo Kenya ama Uganda, ama nchi zile zisizohitaji visa...
 
Serikali si inayonyanyapaa. Bali Watu waliopo pale na hasa ukute mkuu wa kitengo hakusoma nje wewe unaletwa pale na qualification za kutokea nje ya nchi. Atawaweka waliosoma Tanzania kwenye vitengo mbali mbali wewe utabaki peke yako na hujui wapi uko wrong.
Ni ukweli nimeamua kuusema. Kama hutaki basi sikulazimishi. Haikuumi labda kwa sababu haijakukumba kwa sababu umesoma Tanzania hivyo suluba ya kusoma nje ya nchi haikuhusu.
Sawa kama hauhusiki lakini kutokuhusuika kwako haina maana hakuna watu wanaoteseka.
Mada iko wazi ila mnaipindisha makusudi tu. Mnapoipindisha makusudi mnaithibitisha mada yangu. Niliyoyasema kumbe kweli yapo.
Na maofisini wanaipindisha hivi hivi kama mnavyofanya humu. Ukiuliza kwanini nakaa miaka kumi bila kupandishwa cheo wanatoa jibu huna sifa........
Simple like that!!
Nimependa hii topic mkuu, acha akushambulie, lakini kuna tatizo, na kulizunguka mbuyu sio kulitafutia ufumbuzi........i think only solution kutoa favour maofisini ni kuwa na performance criteria ambayo itakua measured against kila employee....na ukiona miaka kumi hupandishwi cheo, unashtaki, Mkuu wako anaenda for disciplinary actions...very unfair....umehighlight changamoto zinazowakumba waliosoma nje, utapingwa vikali..lakini at least umesaidia wanaosoma nje wajue changamoto watakazokumbana nazo wakirudi..so its very useful, wala usikatishwe tamaa na watu wasio na busara humu, kwanza kama hakupandishi cheo kisa umesoma nje , chances anakuona threat ama ana inferiority complex ambayo sifa yao kubwa wenye hio kitu ni kubwatuka na kushambulia...
 
Habari za asubuhi.

Somo tajwa hapo juu lahusika.

Sisi tuliosoma nje ya nchi tukirudi Tanzania kwenye taasisi za serikali tunanyanyapaliwa sana. Suluba inaanzia hapa:

Kwanza tunaambiwa tukavithibitishe vyeti vyetu TCU. Tukifika TCU usumbufu tunaopata pale ni mkubwa sana!

Unaambiwa upeleke ushahidi kwamba ni kweli ulikwenda nje ya nchi.

Wanataka visa yako ioneshe ni student visa wakati unaondoka. Pia uoneshe sehemu ya passport ulivoondoka na ulovyofika kule yaani uoneshe sehemu iliyogongwa muhuri.

Hayo si issue sana maana mwisho unatakiwa ulipie.

Kubwa ni lile unapofanya kazi wakubwa hawakupi kipaumbele wala kuthamini elimu yako. Wanakuona ni adui na unajifanya mjuaji.

Linapokuja suala la promotion utasugua benchi mpaka utajuta kwa nini ulikwenda kusoma nje ya nchi.

Waliosoma hapa nchini utawaona wanapeta tu na maisha yao yanaenda vizuri. Vyeo wanapewa mpaka unashangaa mtu kapataje maana uwezo wa kiuongozi au kiufundi unamzidi kwa kila kitu.

Kwa kweli hali hii inatuumiza sana.
Je, ni kosa kusoma nje ya nchi?
Hata mie nimesoma nje ya nchi ila hayo uyasemayo isipokuwa la verification, hayana uhalisia! Verification ni muhimu sana ingawa wanaweza kupunguza ukiritimba! Kuhusu 'treatment' unayopata kazini is purely comes from your own attitude! The fact that you are still referring to your foreign university badala ya kuonyesha ujuzi is bull shit! Na ukiendelea hivyo utapiga jalamba sana! Mwajiri Hana interest na chuo ulichosoma, anataka u'showcase' skill!
 
Back
Top Bottom