Tulifika Dar saa 9 usiku kutoka Zanzibar, kitu cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi

Candela

JF-Expert Member
Aug 12, 2021
622
1,643
Hivi karibuni nilikuwa Zanzibar, baada ya shughuli zangu nilikwenda bandari lakini nikawa nimechelewa boat.

Nikalazimika kupanda ile ya saa 3 usiku. Tulifika Dar saa 9 usiku ila cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi.

Hii iliniacha na maswali sana kama kuna kusafiri usiku kwa nini tusishuke maana kwa Dar saa 9 usiku ni kama kumekucha tu.

Kama issue ni bandari basi uwekwe utaratibu ila kwa sasa ni kusumbuana aisee.

Yaani haya mambo ni viashiria vya umasikini wa nchi.
 
Wanaweza kukuambia hatuna wafanyakazi wa kufanya check in/out mpaka saa 12 asubuhi, ni dalili ya umaskini wa akili hakuna zaidi, kwa wenzetu mfano Bank za kimarekani ukiwa ndani ya Bank unasubiri huduma na imetokea muda wa kufunga umefika, security watafunga milango yote ya kuingilia ndani wataacha wa kutoka tuu, mtahudumiwa mliokuwa ndani mpaka wamemaliza wote au wakiona foleni zinakuwa kubwa ujue mpaka meneja atatoka ofisini kuja kuhudumia wateja, ikishindikana kabisa wako wakulipe au wakupe huduma bure kesho yake, niliwahi kulipwa dollar 800 kwa sababu ndege ilikuwa imejaa wakauliza yeyote ambaye yuko tayari kuachia sit mpaka next flight tunakupa 300$ hawakupata mtu mpaka walipopandisha 800$ mchizi nikanyoosha mkono:D
 
Hivi karibuni nilikuwa Zanzibar, baada ya shughuli zangu nilikwenda bandari lakini nikawa nimechelewa boat. Nikalazimika kupanda ile ya saa 3 usiku. Tulifika Dar saa 9 usiku ila cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi. Hii iliniacha na maswali sana kama kuna kusafiri usiku kwa nini tusishuke maana kwa Dar saa 9 usiku ni kama kumekucha tu. Kama issue ni bandari basi uwekwe utaratibu ila kwa sasa ni kusumbuana aisee. Yaani haya mambo ni viashiria vya umasikini wa nchi.
Nadhani ulipanda meli maana boat karibia zote speed yake ni masaa mawili ama matatu uko Dar na kuna mpaka za dk 45

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sio speed, kwanini mtu asubiri masaa matatu kutoka bandarini, huoni kama ni tatizo?
Hilo ndio tatizo kubwa na la msingi, na halijaanza kupigiwa kelele leo.. Zamani zile za Flying horse bandari ya Zenji ilikuwa inafungwa saa nne usiku kwahiyo inabidi chombo kiondoke bandarini na kwenda kupaki huko katikati ya bahari mpaka saa tisa alfajiri ndio kianze safari ya Dar.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni nini mpaka kuwasubirisha watu masaa matatu? giza au kukosa wafanyakazi, unaonekana akili zako ndio za hao hao anaowaongelea
Kwanini alichelewa?
We unaondoka usiku huna haraka kaa usubiri pakuche, Sio kuita ndugu zetu maskini hapa.
Kwanza Sie wote Maskini tunapishana tu kiwango cha Umaskini.
Ila ni tusi baya sana kumwambia Maskini we MASIKINI.
 
Nadhani ulipanda meli maana boat karibia zote speed yake ni masaa mawili ama matata uko Dar na kuna mpaka za dk 45

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna boat ya kutoka Zanzibar saa tatu usiku inatembea mwendo mdogo sana inaingia Dar saa tisa usiku. Abiria hamruhusiwi kuteremka Hadi ifikapo saa kumi na mbili asubuhi.

Ni boat nzuri na ya kisasa, sema Kuna mende wengi kwenye ile boat sijapata kuona... Sijui wahusika hawajaliona hilo
 
Kuna boat ya kutoka Zanzibar saa tatu usiku inatembea mwendo mdogo sana inaingia Dar saa tisa usiku. Abiria hamruhusiwi kuteremka Hadi ifikapo saa kumi na mbili asubuhi.

Ni boat nzuri na ya kisasa ,sema Kuna mende wengi kwenye ile boat sijapata kuona...sijui wahusika hawajaliona hilo
Sema Kuna mende wengi kwenye ile boat sijapata kuona...sijui wahusika hawajaliona hilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi karibuni nilikuwa Zanzibar, baada ya shughuli zangu nilikwenda bandari lakini nikawa nimechelewa boat. Nikalazimika kupanda ile ya saa 3 usiku. Tulifika Dar saa 9 usiku ila cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi. Hii iliniacha na maswali sana kama kuna kusafiri usiku kwa nini tusishuke maana kwa Dar saa 9 usiku ni kama kumekucha tu. Kama issue ni bandari basi uwekwe utaratibu ila kwa sasa ni kusumbuana aisee. Yaani haya mambo ni viashiria vya umasikini wa nchi.
Ndiyo maana zamani hizo boat ilikuwa zinakaa sehemu usiku zinaelea hadi saa sita usiku ndiyo zinaanza safari ili zifike Dar alfajiri..

Halafu hata huyo nahodha wa boat ni mpuuzi kwanini asikadirie speed anayotembea ili afike asubuhi badala ya kuingiza watu usiku mkubwa?.
 
We mwenyewe maskini,
umechelewa, ukapanda boti la usiku.
Umeshindwa nini kulala Hotel uondoke kesho?
Ndege hazipo kwanza?
We ni Maskini kuliko hata hao unaita Maskini
Kama alikuwa anawahi jambo asubuhi sana na amepata hiyo fursa ya saa tatu aiache aende akalale?

Issue hapa shughuli nyingi haziendi kisa tunafanya kazi masaa 12, inabidi tubadilike tuwe kama maaskari au hospitali.

Ni zamu kwa zamu hakuna kulala.
 
Kuna boat ya kutoka Zanzibar saa tatu usiku inatembea mwendo mdogo sana inaingia Dar saa tisa usiku. Abiria hamruhusiwi kuteremka Hadi ifikapo saa kumi na mbili asubuhi.

Ni boat nzuri na ya kisasa ,sema Kuna mende wengi kwenye ile boat sijapata kuona...sijui wahusika hawajaliona hilo
Tutumie common sense, boti ya kukaa masaa matano badala ya one hour baharini la kazi gani?

Sifanyi biashara hii.
 
Hivi karibuni nilikuwa Zanzibar, baada ya shughuli zangu nilikwenda bandari lakini nikawa nimechelewa boat. Nikalazimika kupanda ile ya saa 3 usiku. Tulifika Dar saa 9 usiku ila cha ajabu tukaambiwa kushuka ni saa 12 asubuhi. Hii iliniacha na maswali sana kama kuna kusafiri usiku kwa nini tusishuke maana kwa Dar saa 9 usiku ni kama kumekucha tu. Kama issue ni bandari basi uwekwe utaratibu ila kwa sasa ni kusumbuana aisee. Yaani haya mambo ni viashiria vya umasikini wa nchi.
Hiyo uliyopanda ni meli ya mizigo siyo boat. Azam sealink siyo boat. Siku nyingine uwe unafahamu umepanda nini na utaratibu ukoje.
 
Kuna siku ilinipata hiyo kadhia nikitoka Dar kwenda Zanzibar, tulipanda zile Azam Sea Link ( sio speed boat) ni ya mizigo, magari na abiria wengi zaidi ila Mara nyingi inasafiri usiku.

Tulifika Unguja saa tisa usiku na tuliruhusiwa kushuka Kwa vile kulikua na magari ya BoT ya kusafirishia pesa kwenye hiyo meli.

Turudi kwenye hoja ya mleta Uzi.

Zile meli Mara nyingi zinapakia abiria na kushusha eneo la bandarini, sio huku kwenye speed boat. Hapo inabidi wahusike maofisa wa usalama, TRA, Bandari na wenye chombo wenyewe, ina maana ikiwa mojawapo ya maofisa kati ya hao hapo juu hawatakuwepo, ni nadra sana mizigo na abiria kuruhusiwa kushuka usiku.

Flying Horse siku hizi safari zake ni Unguja - Pemba.

Hitimisho, kama una haraka na hauwezi kuchukua mwewe, Bora usubirie boat ya saa moja inayofika saa tatu kasorobo. Vinginevyo ukubali kubaki kwenye chombo hadi papambazuke.
 
Back
Top Bottom