Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Mwenye email au simu ya itv nataka niwashauri wamepoteza mashabiki sana zamani walikuwa super kweli sikuhizi ikiisha tu habari basi zamani walikuwa na vipindi vizuri mno wao ndo walileta tamthilia za kikorea zilipata mashabiki sana hata katuni za watoto enzi hizo kina ed edd eddy dexter powerpuf girls ben ten etc
 
Vipindi hivyo vingine ni vya uchochezi kwa vijana wetu...hatuvitaki virudi.tuwekewe vipindi vya kilimo vya kufuga...vya PowerTilla zinavyolima na hotuba za rais.
hahahahaa, sasa si bora vipindi vya kipindi kile kuliko now uchi uchi, eti power tilla
 
Kipindi hicho siku za Jumamosi nilikuwa ninaweza kuangalia ITV kuanzia asubuhi mpaka usiku bila kubadili channel. Ilikuwa ni kipindi bomba kimoja baada ya kingine.
 
Rastruss na misanya binghi, hiki ndo kipindi kilichoniintroducia bob marley kumjua kwa mara ya kwanza, kupitia ule wimbo wake wa no woman no cry
 
ITV ilitisha sana vipindi kama tamthilia ya tausi kuna mtu anaitwa mponda jamaa alikua akivunja mbavu zangu kwa kucheka,pia UEFA tulikua hatulali tukisubiri game za usiku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom