Tukumbushane miiko ya mila zetu

Kitty Galore

JF-Expert Member
May 24, 2011
345
100
Wadau najua kila mmoja ana mila za kwao. Hebu tukumbushane kidogo miiko yetu ili hata ambao hawazijui waweze kufahamu kwamba zilikuwepo. Hapa haijalishi ni kwa kabila, koo n.k
Mfano:
1. Mwanamke akiwa anasonga ugali mwiko ukivunjikia sufuriani ni mbaya (sijui ubaya wake ni nini)
2. Mtoto akianza kuota meno ya juu, akija kuoa/kuolewa mwenza wake atakufa,
3.
4.
Tuendelee
 
1. Mtoto wa kike akikaa katikati ya mlango hatoolewa. 2. Mtu akikuruka hutorefuka. 3. Ukijiangalia kwenye kioo usiku sikumbuki utafanya nini ila inatisha.
 
Ukikojoa kichakani tema tema mate ili mama asivmbe matiti,
mtoto wa kiume aruhusiwi kukaa jikoni! Firigis ni ya baba na maini! Ila mjin kilamtu anakula ni pesa yako lol!
 
kuku akichinjwa na nyama yake kupikwa FIRIGISI ni ya baba hahaaa. huruhusiwi kupiga mluzi nyumbani ni baba peke yake anaruhusiwa. ukipiga mluzi usiku unaita nyoka.
 
  1. usikalie kinu mwanamke hutajaaliwa kuzaa
  2. usitupe nguo yako ama kitambaa chochote chenye hedhi for mbaya wako akitupia jicho huzai...
  3. Ukiona zeru zeru temea mate kwenye blouse ili nawewe usizae zeruzeru (THIS IS DELICATE I KNOW) Natoa ili tuweze ona ni jinsi gani imani nyingine zilikua za kijinga kabisaa!!
  4. Mwanaume asilie kwenye sufuria la sivyo siku ya ndoa yake mvua nzito itanyesha...
 
ni mwiko kwa mwanamke kumwambia mumewe ana hamu ya kukazwa! Ni mwanaume tu ndo mwenye ruhusa ya kuanzisha game usiku.
 
Jamani...naomba tu tuseme hii miiko tulifundishiwa wapi maana zote zinakaa za uchagani uchagani...ama ndo miiko meingi ya kitanzania inaendana!??
 
1. singles wakila chakula wamekaa kitandani hawataoa katu

2. wavulana wakikojia mtoni siku ya kupashwa tohara watavuja damu itiririke hadi pale mtoni walipokojoa
 
Ashadii dadaa, mbona unaniangusha, yaani uoni hikma yake kwenye hizo taboo?

Kabla sijadadaua, inakupasa utambue kwanini waliweka hiyo miko, kwenye jamii. Kwanza ili kutunza kuheshimiana, kutodharauliana na dhana nzima ya usafi wa mwanamke na vitendea kazi.

1. usikalie kinu mwanamke hutajaaliwa kuzaa
Kila mtu anaelewa kazi ya kinu, ni kutwanga/kukoboa nafaka, iki ni kifaa muhimu sana na kinatakiwa kupewa hishma yake ili kibakie kwenye hali ya usafi, na ndio maana miko mingi ipo kwenye dhana ya kutishana ili watu waifuate. Ebu mwenyewe fikiria umkute mtu kakalia kitu upande ule wa kutwangia, kisha akipumulie, na kesho atwangie humo humo.
Mf: Ukitaka kuwatisha wanaume wasinywe/kula kinywaji/chakula fulani basi waambie kuwa kula/kunywa kutawapunguzia nguvu za kiume. Ni rahisi sana kuacha kuliko wangeambiwa kutawapelekea kupata saratani (cancer) japo ndio ukweli.

2. usitupe nguo yako ama kitambaa chochote chenye hedhi for mbaya wako akitupia jicho huzai...
Sasa hapa ujui kuwa wanawake wanatakiwa kuwa wasafi, wao na mazingira yao, hivi kila mwanamke kijijini au mjini au uko mitaani akitupa hizo Space Shuttle za kuendea mwezini, ujui kuwa ni kueneza maradhi kwenye jamii inayo wazunguka.

3. Ukiona zeru zeru temea mate kwenye blouse ili nawewe usizae zeruzeru (THIS IS DELICATE I KNOW) Natoa ili tuweze ona ni jinsi gani imani nyingine zilikua za kijinga kabisaa!!
Hapa tuaelekezwa kuonyesha kuheshimiana, kama wewe unamuona zeruzeru ni mchafu au anakuchefua kwa arufu yake basi temea mate kwenye brouse yako (kama unaweza).

4. Mwanaume asilie kwenye sufuria la sivyo siku ya ndoa yake mvua nzito itanyesha...
Mwanaume kulia kwenye sufuria ni dalili ya ulafi, kinachokufanya mpaka ule kwenye sufuria ni nini? Ndio wakatishwa kwa kuambiwa hayo waliyo ambiwa.

Kuna lingine dadangu!?
 
Ashadii dadaa, mbona unaniangusha, yaani uoni hikma yake kwenye hizo taboo?

Kabla sijadadaua, inakupasa utambue kwanini waliweka hiyo miko, kwenye jamii. Kwanza ili kutunza kuheshimiana, kutodharauliana na dhana nzima ya usafi wa mwanamke na vitendea kazi.

Kila mtu anaelewa kazi ya kinu, ni kutwanga/kukoboa nafaka, iki ni kifaa muhimu sana na kinatakiwa kupewa hishma yake ili kibakie kwenye hali ya usafi, na ndio maana miko mingi ipo kwenye dhana ya kutishana ili watu waifuate. Ebu mwenyewe fikiria umkute mtu kakalia kitu upande ule wa kutwangia, kisha akipumulie, na kesho atwangie humo humo.
Mf: Ukitaka kuwatisha wanaume wasinywe/kula kinywaji/chakula fulani basi waambie kuwa kula/kunywa kutawapunguzia nguvu za kiume. Ni rahisi sana kuacha kuliko wangeambiwa kutawapelekea kupata saratani (cancer) japo ndio ukweli.

Sasa hapa ujui kuwa wanawake wanatakiwa kuwa wasafi, wao na mazingira yao, hivi kila mwanamke kijijini au mjini au uko mitaani akitupa hizo Space Shuttle za kuendea mwezini, ujui kuwa ni kueneza maradhi kwenye jamii inayo wazunguka.

Hapa tuaelekezwa kuonyesha kuheshimiana, kama wewe unamuona zeruzeru ni mchafu au anakuchefua kwa arufu yake basi temea mate kwenye brouse yako (kama unaweza).

Mwanaume kulia kwenye sufuria ni dalili ya ulafi, kinachokufanya mpaka ule kwenye sufuria ni nini? Ndio wakatishwa kwa kuambiwa hayo waliyo ambiwa.

Kuna lingine dadangu!?

Bora nimekukuta hapa for now i remember deni... Aalafu XP
nakubali hio misemo ila tu huo wa zeru zeru ndio niliosema haufai....
Ndio maana nikasema mila zingine (note sio yooote...)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom