Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Siku ya jana na Leo Bunge limekuwa la moto kweli, kila mbunge akiishambulia serikali na mawaziri wake. Kwa sisi wenye uelewa tunajua hizi ni mbio za sakafuni tu.
Sasa hivi wabunge wanajua Muda wa kukaa bungeni umeisha, kila mbunge anajinadi sasa na kuishtumu serikali juu ya ubadhirifu wa fedha na ufisadi wote uliofanywa na serikali. Kwa sababu wanajua wamebaki mwaka mmoja tu wa kuendelea kubaki madarakani na mwaka huu umeshaisha ndio kwamba tuko Novemba, na mwaka 2025 hasa hasa ni wa kampeni na uchaguzi, hivyo mwaka pekee uliobaki kuwashawishi wananchi tuone wanafanya kazi ni mwaka 2024.
Wanajua kabisa Wananchi hawakubali mtaani, kwanza walipitisha DP World, pili Ufisadi, tatu Upigaji umerudi, rushwa na kadharika. Wabunge walikuwa wanapiga makofi tu bungeni, na kupitisha mikataba bila kusoma.
Sasa mtaani wanajua kurudi bungeni ni mtiti, wanafanya juu chini sasa hivi kutukana serikali, kwani mwanzo kipindi wananchi tunalalamika mlikuwa wapi wakati nyinyi ndio sauti zetu bungeni. CCM mnatuletea unafiki, mmeshapiga hela sasa hivi mnatuektia.
Mimi kura yangu ya wabunge na madiwani naipeleka vyama Pinzani, Kwenye Urais bado nasikilizia upepo, akitokea rais wa maana nampatia kura yangu.