Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,845
- 10,070
Msaada wakuu, hii hali imeanza kuwa serious sana. Kwa sasa inanikuta kila mwezi tofauti na awali ilipokuwa inanitokea mara moja kwa mwaka
Inaanza uko maeneo fulani ukiwa na mtu fulani, wakati unamalizia mazungumzo, ndipo unakumbuka kuwa hayo maneno umewahi yatamka kabla. Hata eneo ulilopo ndilo lile lile, pia mtu unayezungumza naye ni yule yule au mtu anayeendana hobies na uliyozungumza naye mwanzoni
Au unapita mahali unakutana na tukio amabalo umewahi kukutana nalo kabla. Hata majibizano ya watu yanayoendelea ni yaleyale ya kipindi hicho. Unapojaribu kufungua mdomo kuzungumza, unajikuta unazungumza yale yale uliyowahi kuzungumza. Unabaki unashangaa tu
Hii hali husababishwa na nini wakuu?
Je, tukio la kwanza kabla, lilikuwa ni ndoto? Au liliwahi tokea kweli? Au ni mawenge tu? Au naumwa malaria? Maake sielewi hata limekuja vipi, yaani from nowhere
Nikijaribu kumuuliza huyo ninayezungumza naye kwamba haoni kama tunafanya marudio?, anaishia kusema nipunguze wenge au kucheka tu
Naombeni ufafanuzi wakuu
N.B: Situmii mihadarati