Tujikumbushe aliyosema nyerere- viongoz tunaotaka

Dr wa ukweli

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
900
264
TUNAKWENDA WAPI? - VIONGOZI TUNAOWATAKA
>
> Naeleza baadhi ya matatizo ambayo viongozi tutakaowachagua tuwe na hakika
> iwapo wanayaona hivi kama sisi tunavyoyaona. Yanawauma kama sisi
> yanavyotuuma na kwamba, watakapofika hapo wanapopataka watusaidie kuyatatua.
> Wanayaona, yanawakera na hata watakapofika hapo, hicho ndicho
> kitakachowasukuma kutaka kuwa marais wetu na wabunge wetu. Marekani walikuwa
> na rais wao kijana mmoja mdogo anaitwa John Kennedy. Walimpiga risasi.
> Marekani nao ni watu wa ajabu sana! Vijana walilaani tukio hilo kwa kuwa
> walikuwa wanadhani wamemchagua rais wa umri wa kama miaka arobaini na mitatu
> au minne hivi. Sasa huyo ni kijana, hata kwa hapa Tanzania leo ni kijana.
> Alipochaguliwa na Marekani akawa Rais wao. Katika hotuba yake ya kwanza
> kabisa aliwambia wananchi wenzake, hasa vijana "Usiulize Marekani
> itakufanyia nini, jiulize wewe utaifanyia nini Marekani?".
>
>
> Kila anayetaka kuwa mgombea wa urais/ubunge ajiulize ataifanyia nini nchi
> yake
>
> Tunataka mtu anayetaka kuwa rais wetu ajiulize anataka kuifanyia nini nchi
> yetu na sio nchi yetu itamfanyia nini. Na tunataka swali hilo ajiulize kila
> mtu anayetaka kuwa mgombea wa chama cho chote kuwa mbunge/rais: "Kwa nini,
> kwa dhati kabisa, anaumwa na umasikini wetu na umasikini huo ndio
> unaomsukuma ashughulike na mambo haya ya siasa katika ngazi hiyo ama ya
> ubunge ama ya urais". Kama sivyo, hatufai!
>
> Mtu hapakimbilii Ikulu: Hakuna Biashara Ikulu
>
> Mtu anayetaka kwenda Ikulu kutaka faida ye yote Ikulu pale hatufai hata
> kidogo. Wananchi, mimi nimekaa pale Ikulu kwa muda mrefu zaidi kuliko
> mwingine ye yote, wala sidhani kuna mtu mwingine anaweza kuzidi muda huo.
> Tayari hapa tumeweka sheria. Kwa mujibu wa sheria, mtu hawezi tena kukaa
> Ikulu zaidi ya miaka kumi, kipindi ambacho hata hakijafikia nusu ya kipindi
> nilichokaa. Mimi nimekaa miaka ishirini na tatu!
>
> Najua, kwa mtu halisi kabisa, Ikulu ni mzigo! Hupakimbilii! Si mahali pa
> kupakimbilia hata kidogo; huwezi kupakimbilia Ikulu. Unapakimbilia kwenda
> kutafuta nini? Ni mgogoro; ni mzigo mkubwa kabisa! Ukipita barabarani,
> unakuta watu wana njaa, unaona ni mzigo wako huo. Pazito pale! Huwezi
> kupakimbilia na watu safi hawapakimbilii. Ukiona mtu anapakimbilia, na hasa
> anapotumia tumia vipesa kwenda Ikulu, huyo ni mtu wa kuogopa kama ukoma!
>
> Mtu ye yote anayeonekana anapenda sana kwenda Ikulu na hata yupo tayari
> kununua kura ili kumwezesha kufika Ikulu ni wa kumkwepa kama ukoma. Kwanza,
> hizo fedha kapata wapi. Mtanzania wa leo hawezi kununua watu bila kwanza
> yeye kununuliwa. Na kama kanunuliwa, atataka kuzilipaje? Kazipata wapi?
> Watanzania wote ni masikini tu. Mtanzania anaomba urais wetu kwa hela!
> Amezipata wapi?
>
> Pili, kama hajanunuliwa, kazipata wapi? Kama kakopa, atarudishaje? Ikulu
> pana biashara gani mtu akope mamilioni halafu aende ayalipe kwa biashara ya
> Ikulu? Ikulu mimi nimekaa kwa muda wa miaka ishrini na mitatu. Ikulu ni
> mahali pazito. Kuna biashara gani Ikulu?
>
> Rushwa na Matumizi ya Fedha Bila Utaratiba Wakati wa Chaguzi
>
> Sisi Waafrika ni watu wa ajabu sana. Unajua ni wadogo, lakini nasema, ni
> udogo wa mawazo. Umaskini wa mawazo ni umasikini mbaya kupita wote. Unaweza
> ukawa na almasi mfukoni, akaja tapeli na kijiwe kimetengenezwa kama almasi
> akakuambia "ebu tuone almasi yako. Bwana aa! Hii ya kwako sio almasi ni
> chupa tu, almasi ni hii. Kwanza nipe bwana." Mkabadilishana. Yeye akachukua
> almasi yako na akakuachia kichupa na ukatoka hapo unashangilia kama zuzu!
>
> Sisi hapa Tanzania tulikuwa tumeanza utaratibu ambao ukitumia fedha nje ya
> fedha za chama na serikali na ukatumia fedha zako mwenywe katika uchaguzi,
> tunakutoa. Hufai! Huo ndio ulikuwa utaratibu wetu. Tulikuwa tunakuuliza:
> "hii nchi ya masikini, wewe mwenzetu una mali umeipata wapi?"
>
> Mali, kwa wakati huo, kwetu sisi ilikuwa ni sifa ya kukunyang'anya uwezo wa
> kugombea uongozi Tanzania. Tulijua kwamba, kama una mali, utaficha. Leo watu
> wanasema waziwazi: "Mwalimu uchaguzi wa mwaka huu utapitishwaje?"
>
> Marekani wanatumia fedha nyingi sana katika uchaguzi. Nyingi sana! Kama
> Marekani sasa hivi wanazungumza watunge sheria inayofanana na ile mliyoitupa
> ninyi mnadhani kwa sababu ni mawazo ya masikini, haina maana. Wakubwa
> wanayafikiria mawazo hayo sasa hivi. Marekani wanafikiria uwezekano sasa wa
> kutunga sheria itakayoweka utaratibu wa fedha za ugombeaji kutokana na mfuko
> mmoja baada ya kugundua kwamba inapokuwa holela na kila mtu akiachiwa lwake,
> inavuruga. Inaleta rushwa kubwa kabisa. Unanunuliwa urais na unaweza
> kununuliwa na fedha za wauza bangi na wauza baa. Wauza bangi wanaiona hatari
> hiyo, ninyi haa!
>
> Hapa tulikuwa na utaratibu mzuri kabisa tuliouanzisha mlioutupa, mnafikiri,
> sisi mwaka huu fedha tu! Uchaguzi wa fedha, mtazipata wapi? Mimi nimetoka
> juzi tu, mara mmetajirika kiasi hiki! Waswahili hee! Kumbe mnaweza
> kutajirika zaidi kwa haraka hivyo? Sasa kama mnao uwezo wa kutajirika,
> nawambienj 'Fanya wote tutajirike. Hivi mtajirike peke yenu, tutajirike
> wote". Wapi! Ni rahisi sana watu wachache kutajirika.
>
> Tunataka Serikali inayotoza kodi
>
> Kwa hiyo, naserna sasa hivi mimi sijali kabisa na wala msifikiri tena
> napinga watu wanaotaka uhuru wa kujipatia mali. Tunataka serikali
> itakayotoza kodi. Tulikuwa na viserikali vya rafiki zetu za Skandinavia
> vinavyoongozwa na watu wanaojali maslahi ya umma. Vinatoza kodi matajiri,
> halafu mapato hayo yanasambazwa kwa faida ya wote. Hata hapa fanyeni hivyo.
> Lakini isiwe ni kukusanya kodi na halafu, kilicho chetu mnataka kukiuza.
> Hata hicho muuziane, halafu mpate pesa na hizo pesa zenu wala rnsilipe kodi!
> Hii ndio kazi tuliyowapeleka Ikulu?
>
> Sifa za ziada za viongozi
>
> Nilipokuwa Dar es Salaam, nilieleza mahala fulani kwamba watu wanaotaka
> kutuongoza wawe angalau na sifa hizi na hizi. Sasa nasema hata wakiwa nazo
> bado tutawauliza: "sifa mnazo, lakini mnakwenda kufanya nini?" Hata nikiwa
> na watano wenye sifa nzuri bado nitasema: "Ninyi watano mna sifa nzuri
> kabisa, mimi sioni kama mna kasoro lakini bado nitawauliza hasa mnakwenda
> kutafuta nini Ikulu. Uniambie kwa dhati ya moyo wako kinakuuma nini kwamba
> unaweza kweli ukaumwa kabisa". Halafu ukasema: "Mwalimu, Ikulu sipapendi.
> Ikulu siyo tatizo. Kama mambo yanakwenda ovyo ovyo utaacha tu?
>
> Zile sifa nilizozitamka hazitoshi: kwamba lazima uwe Mtanzania na unaheshimu
> Tanzania. Maana tunatafuta rais wa Tanzania na wala hatutafuti wasifu wa
> Rais wa Tanzania. Tuna miezi saba uwe umezipata zile tano na kuendelea. Hata
> hivyo, bado tutawauliza mambo ya uchumi, viwanda na shule unavyoyaelewa.
> Mambo ya afya, ninyi mnayajua yote. Hospitali zetu, hali yake ya sasa hivi
> mnaielewa inaendaje endaje na kama mnaelewa ninyi unaionaje? Unaona raha tu?
> Maana sisi ni watu wa sera ya kuchangia. Sawa. Lakini wewe umechangia mara
> ngapi? Hebu nenda katika hospitali moja uone watu wanavyochangia.
>
> Tunataka kufikiria kwa msingi kwamba kitu kimoja tunachotaka kuelewa ni
> hali ya matatizo yetu yalivyo sasa. Hii ni kwa sababu awamu ya kwanza, awamu
> yangu mimi, imefanya mema na imefanya ya kijinga. Yale ya kijinga,
> mnayaacha. Lazima yanaachwa. Ubaya wenu ni kwamba mnayaacha mema na
> mnachukua ya kijinga.
>
> Miaka ishirini na tatu, bwana, lazima tumefanya makosa. Pale, bwana,
> hatukuwa na wasomi wengi, ujuzi wala cho chote. Tulikuwa tunahangaika tu.
> Kama watu hamjui kuogelea, mnatupwa kwenye maji, mnahangaika kuogelea,
> lazima mtafanya makosa. Tusifanye makosa kwani sisi ni malaika? Awamu ya
> kwanza ina mambo fulani fulani na hasa ya msingi na mengine ya utekelezaji
> mazuri, mnaendelea nayo. Mengine ya utekelezaji ya ovyo ovyo, mnayachilia
> mbali mnaanzia hapo tena.
>
> Ila la ajabu ni kwamba hata ya msingi mnayawekea alama ya kuuliza. Mimi
> sikudhani kama ya msingi yalikuwa na matatizo, Nilidhani mambo yetu ya
> utekelezaji yana matatizo mengi hivi ya kusikilizana, hata ya msingi. Sasa
> watu wataanza kugombana katika misingi ya ukabila, udini na mambo mengine ya
> kijinga kabisa.
>
Kwa hiyo, nasema, awamu ya pili mnaanza na mengine mnaongeza hapo. Awamu ya
pili nayo inafanya makosa yake, itafanya mema yake. Yale mema, ndiyo
mnayoendelea nayo; mnaendelea na yale mema yake. Yale mabaya mnayaacha kama
yalikuwapo ya msingi yamesahauliwa mnayarudia. Kutoyarudia yale ya msingi,
mtapotea tu. Mnafanya hivyo halafu mnaendelea.

Mimi nataka kujua kama viongozi wetu wa sasa hivi wanaotaka kuingia katika
awamu ya tatu ya uongozi wanayaelewa hivyo na tutaelewana hivyo au
> wanafikiri uongozi ni biashara tu! Je wanaotaka kutuongoza wanaweza, kwanza,
> kuelezea tulikuwa wapi, tuko wapi, tunataka kwenda wapi? Pili, je wanao
> uwezo wa kutupeleka kule tunakotaka kwenda? Tatu, watatushirikishaje kule
> ili na sisi tusaidiane kwenda huko? Hiyo ndiyo kazi iliyobaki. Pimeni Sana!
>
 
Back
Top Bottom