Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,939
- 46,690
Wizara ya nishati tangu naijua na kuisikia sijawahi kuona ikipewa waziri mtaalamu wa umeme, watu wa electrical engineering au power systems engineering.
Tofauti na Profesa Muhongo ambaye angalau alikuwa mwanasayansi wa miamba(na alijikita zaidi katika madini) sijawahi kuona kabla au baada yake wizara hii ikiongozwa na Waziri mwanasayansi achilia mbali mtaalamu wa masuala ya umeme.
Wizara wamekuwa wanapewa zaidi wanasheria na wengine waliosoma sanaa ambao sayansi ya umeme kwao huenda wanaona nyotanyota tu. Japo pia imekuwa inaongozwa na wanasheria kwa muda mrefu bado ni mojawapo ya wizara ambazo tumepigwa sana katika mikataba ya ajabu.
Sasa labda ni wakati wa kuwapa wataalamu manguli wenye sekta yao katika nafasi zote za waziri na naibu wake tuwajaribu nao, huenda kuna mambo wanaweza kuyaona kwa jicho la tatu ambao sio rahisi mtu maamuma wa umeme kuyafahamu.