The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Nimeanzisha mjadala huu baada ya tukio la jana huko Chato la msafara wa Mgombea Urais - CHADEMA ndugu Tundu Lissu kushambuliwa kwa mawe na wafuasi wa CCM mara baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi katika mkutano wake wa kampeni.
Kabla ya tukio hilo la Jana tulimwona yule ajiitaye "mwanaharakati huru" wa kumtetea Bw. John Pombe Magufuli, Cyprian Musiba akionya kuwa Lissu asiende Chato na kumtukana Rais Magufuli kwa sababu atakiona cha mtema kuni!
Baada ya tukio hilo baadhi ya posts ktk mitandao ya kijamii zikaunga mkono uhalifu huo eti ni kwa sababu anamtukana sana Rais Magufuli na kuidhalilisha serikali badala amwage Sera..!!
Honestly, hoja hii mimi huwa siielewi, hainingii kwenye akili yangu na naiona ni ya watu wasio na ufahamu wa kutosha wa maarifa.
KWANZA;
Inaeleweka kuwa, kwa mujibu ya sheria za Tanzania "MATUSI" ama "KUTOA LUGHA YA MATUSI" ni kosa la jinai kwa yeyote dhidi ya mtu aliyetukanwa..!
PILI;
Ni nani amewahi kumlalamikia Tundu Lissu kuwa amemtukana? John Pombe Magufuli amewahi kufanya hivyo? Jibu ni: HAPANA. Kwanini? Haijulikani...!
Kama hakuna ambaye amewahi kumshtaki Tundu Lissu kwa madai ya "kutukanwa" akiwemo Magufuli mwenyewe, haya madai ya kuwa Tundu Lissu anamtukana Rais Magufuli na kuidhalilisha serikali yanatoka wapi? Msingi wake ni nini?
Kwa mtazamo wangu nadhani hizi ni sababu wanazozitumia kuficha udhaifu na mapungufu ya bwana Mkubwa huyu anayedaiwa kutukanwa;
1. Tundu Lissu amevunja MWIKO (taboo) na MAZOEA/UTAMADUNI mbaya (bad tradition) uliokuwa uanajaribiwa kujengwa miongoni mwa wanajamii kudhani kuwa "ni mwiko kumkosoa mfalme - Rais". Hili limewashitua na kwao wanaona haya ni MATUSI makubwa sana kuusema wazi udhaifu na mapungufu ya kiutendaji ya mfalme - Rais...
Lakini hakuna sheria inayounga mkono dai lao. Kwa sababu, hakuna matusi ktk hotuba za Lissu..!
2. Kingine kinachowasumbua ni umahiri na style ya mgombea Urais wa CHADEMA ndg Tundu Lissu kuuelezea udhaifu na mapungufu ya mgombea Urais wa CCM ndg John Pombe Magufuli katika lugha yenye kueleweka kwa urahisi kwa wananchi.
Wakati mwingine Tundu Lissu hutumia lugha kali kidogo yenye msisitizo wa nguvu ktk jambo analotaka kulikazia ili watu waelewe. Hili pia huwa ni tatizo kwa wahafidhina hawa..!
Hili ni baya mno kwao wana CCM na wafuasi wao. Ni MATUSI makubwa mno kwao. Hii inafunua upande wa pili wa shilingi wa John Pombe Magufuli ambao wananchi hawa walikuwa hawajui. Na kwa kweli wanashangaa na kupigwa na butwaa kuliko kawaida hata kusema;
"... ala, kumbe huyu mtu ndivyo alivyo? Kumbe tumekuwa tukidanganywa miaka yote hii huku ukweli ukiwa tofauti ..?"
Hili ndilo tatizo lao kwa Tundu Lissu...!!
3. Haya MAZOEA na utamaduni mbaya ndiyo uliokuwa katika majaribio ya kujengwa katika miaka hii mitano ya Rais Magufuli.
Na kiuhalisia yeye binafsi na wafuasi wake baadhi wachache, walishaamini kabisa kuwa wamefanikiwa na wanaweza kukaa kwenye viti vyao vya enzi milele kwa raha mustarehe.!
Kujitokeza ghafla kwa mtu mmoja jasiri wa kuanza kubomoa MAZOEA na UTAMADUNI huu mbaya kabisa kumewashitua. Kunawafanya wahahe, wawe desperate kujiokoa. Chochote kilichopo mbele yao cha kujiokoa, watakitumia. Iwe uongo au hata kumwaga damu ya mtu/watu..!!
Namna pekee ya kujitetea na kujaribu kuulinda au kuu - restore ni kubuni njia ya kunzuia. Kifo ndiyo ilikuwa option ya mwisho. Bahati mbaya kwao option hiyo ika - fail spectacularly!!
4. Kufeli kwa options zote ikiwemo ya kifo, ikawaweka katika "desperation state" watu hawa ktk namna ambayo pengine hawakurajia kabisa,kabisa..
Sasa kinachofanyika ni kutengeneza propaganda, wanazihalalisha kisha wanazitumia kama sababu za kuamuru vyombo vya mabavu hususani polisi kutumia nguvu zenye kusababisha maafa na uharibifu na maumivu makubwa kwa wafuasi wa mgombea huyu wanaomfuata kumsikiliza..!
Karibu kwa maoni na mtazamo wako wewe. Na wana CCM mnakaribishwa zaidi ya wengine kushiriki mjadala huu...