Tuition imeua vipaji vya wanafunzi

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
182
Jamani kama kuna shimo la kufukia vipaji, na uwezo wa kufikiri kwa wanafunzi wetu ni TUITION. Sijui wazo hili lilitoka kwa nani. Tution ilizaliwa miaka ya 1990s na mbaya zaidi baada ya mwaka 2000.
Tuition inafanya wanafunzi wasijiamini kabisa. Wanaona mwalimu wake darasani hawezi kumfundisha hadi aelewe na ndio maana anamtafuta mwalimu mwingine huku akijua msemo wa kiswahili usemao, wapishi wengi huharibu mchuzi.

Wanafunzi wa siku hizi hawapewi tena HOME WORK, badala yake akitoka shule akienda nyumbani anamkuta mwalimu mwingine akimngojea. Wanafunzi wetu hawajui kujisomea wenyewe au kutumia maktaba, hata kufungua vitabu na kutafuta mada anayokusudia hawajui, maana muda mwingi wanazunguka na vipeperushi vilivyochakachuliwa na waalimu wa Tuition. Vitabu vya literature ambavyo enzi za 1980s tulivisoma vizima kama vile MINE BOY, THINGS FALL APART, THE RIVER BETWEEN, nk siku hizi wanafunzi hawavijui hata sura yake kwani wanasoma vipeperushi tu. Uwezo wa watoto wetu umewekwa kapuni.
Enzi zangu nikitoka shule nikenda nyumbani nilikabidhiwa jembe kulima ili kuchangia ada. Siku hizi wanafunzi wetu hawana nafasi ya kazi za mikono maana wamezungukwa na waalimu pande zote. Wamezoea kulishwa tu, SPOON FEEDING. Tunakwenda wapi.
Zamani tulifundishwa na kuzoeshwa kuwa ili ufaulu 60% ni juhudi ya mwanafunzi mwenyewe na 40% ni msaada wa mwalimu. Siku hizi wanafunzi wetu wamegeuzwa, wanajitegemea 20% na 80% ni kutegemea mwalimu. Wanafunzi hata wenye uwezo hawajiamini kufaulu bila dudu hili TUITION.
Ninaomba serikali ifute mchezo huu mchafu wa TUITION kwani HUUWA VIPAJI NA UWEZO WA WANAFUNZI WETU KUFIKIRI. Serikali ilipe waalimu vizuri ili nao wafundishe vya kutosha na si ovyo ovyo kama ilivyo sasa na hatamae wanawaelekeza wanafunzi kuwa ukitaka kujua zaidi njoo jioni. Hii njoo jioni mabinti zetu hugeuzwa kuwa wake za waalimu. Mnafahamu hilo?

mwasemaje?
 
mkuu hapo red wanafunzi wanaotegemea walimu kwa asilimia zote hizo labda wa shule za private ila shule za kata ni vice versa.
 
Hawajiamini hao wanafunzi,lakini pia wamezidi kuwa na uwezo mdogo ukilinganisha na watoto wa zamani hivyo wanakwenda tuition wakidhani wataelewa zaidi badala ya kutumia muda huo kujisomea.Kwa hali hiyo wanafunzi hao kutwa nzima wanatumia muda wao kufundishwa hawapati muda wa kujisomea kama ilivyokuwa zamani.Wazazi wawasisitize watoto wao kujisomea kwa bidii
 
Kuna ukweli ndani yake ila nadhani responsiiliti kubwa ni wazazi. Mimi watoto wangu hawana mwalimu wa tuition na wanafanya homework zao wenyewe. Wakija nyumbani wana 1h ya homework, rest of the time tunapiga story tu na wanaendelea vizuri, always in the A+ equivalent to 95%+ (they are both in primary)
 
Back
Top Bottom