Tuikumbuke 9.11.2001: Tarehe kama ya leo iliyobadilisha historia ya Dunia

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,212
Wengi wetu miaka 21 nyuma tarehe kama ya leo tunaikumbuka siku hiyo tukiwa na umri tofauti na majukumu tofauti. Wengi wengine walikuwa baddo hawajazaliwa au walikuwa wadogo sana kiasi hawajaelewa kilichotokea lakini leo hii hakiwaodoshei kutojuielewa siku hiyo.

Binfasi naikumbuka siku hiyo na nnakumbuka nilivyoganda kwenye kioo cha TV kutazama na kusikiliza kila details mara tu baada ya kupata habari:



Ni siku ambayo iliibadilisha historia ya dunia na siku ambayo ilimgusa kila mtu katika maisha yake.

Binafafsi siku hiyo ilinibadilishia sana maisha yangu, nnadiriki kusema ni siku iliyoniondowa ujanani na kuniingiza utu uzimani kifikra na kimaisha. Matokeo na matukio mengi baada ya siku hiyo yalibadilisha sana mtazamo wangu wa dunia, mwelekeo, malengo na hata maisha yangu ya kila siku yalibadilika ghafla siku hiyo.

Nashukuru AlhamduliLlah, mabadiliko hayo yalikuwa na matukio mengi ya kuhuzunusha na kusikitisha lakini kwa muda mrefu yalikuwa chanya "positive" kwa maisha niliyoishi kila siku baada ya tukio hilo.

Kama una picha, video, clip au chochote cha kuandika karibu sana kwenye kuikumbuka siku hii, muhimu kwa kila mwanadam.
 
Kumbe ni siku nyingi hvyo zimepita,huu uzi wako umenifanya nigundue kuwa kumbe wakati huo nilikuwa mdogo sana lakin ajabu ni kuwa nilijua kila kilicho endelea wakat wa tukio hilo.

Nimewaza nikafikiria watoto wasasa wenye miaka 10 hata vita vya ukraine wanavijua kweli.

Maana nakumbuka enzi hzo ziliibuka taarifa mbalimbali zingine zikisema Osama kalipiza baada ya kunyimwa ujira wake kwa kazi aliyoifanyia marekani.
 
Us, learnt the truth in harsh way. Next time, they will learn not to accommodate just anybody all in the name of liberalism, Muslims are everywhere in France especially refugees, give them an inch, they will take thousands of miles, what they cannot try in Arab countries, they want to do much more in woke countries, same Arab countries that couldn't lend a hand to them and accommodate them as refugees and immigrants, they always want to go to western countries.
 
Nilikuwa standard 05 nawasha Tv niangalie cartoon saa 04:30 pm ITV, wako busy kuonesha hayo majengo yanafuka moshi hata sikuelewa😄
 
Jengo linapigwa juu linaanguka huku chini. Usanii tu.
Hahahaha wale wahuni,fire fighter mmoja alisema 'its a controlled demolition..it's bang bang bang from flow to flow' nakumbuka waliokua chini wakati ndege ya pili ikienda kupiga wakisema 'thats not an American airline, it's like a cargo plane, it's no windows..' pale pentagon hapakua na matairi ya ndege Wala vitu,na kwa ujazo wa mafuta uliosemaa ilikua nayo ile ndege,moto ungewaka muda mrefu na vyumba vilivyobaki vingekua vyeusi kwa Moshi,lakini mpaka personal computer tuliziona na vyumba vilikua viasafi,jirani na pentagon palikua na sheli Ina CCTV camera,wakaenda kubeba tape na kamera....nilikua form six,nafungulia DW ndo nasikia habari
 
Was it an inside job or an act of terrorism?
Hilo Wana jua us wenyewe, maana Hata kuhusu nchi ya sadam Hussein kuvamiwa.
👉Yali ibuka mengi, kuwa ili kuwa propaganda tu. I'll wabebe mafuta.
👉Na Hata Kuna ma ex generals, wali wahi Kwenda kuingilia press conference za Raisi wa wakati huo.
👉Mkumbuke Gaddafi au tazama kwa umakini swala la hapo Congo.
 
Jengo linapigwa juu linaanguka huku chini. Usanii tu.
"Theories" ni nyingi sana, hili halina ubishi wala halina shaka, kwa yeyote aliyelipika basi lilipikika.

Yote yanajadilika, mwisho wa siku kila mmoja wetu anazaliwa ana akili, ni vipi atatazitumia kuchambuwa mambo na kuyafanya au hasi au chanya ndicho kinachotutofautisha.

Unakumbuka nini siku hiyo?
 
"Theories" ni nyingi sana, hili halina ubishi wala halina shaka, kwa yeyote aliyelipika basi lilipikika.

Yote yanajadilika, mwisho wa siku kila mmoja wetu anazaliwa ana akili, ni vipi atatazitumia kuchambuwa mambo na kuyafanya au hasi au chanya ndicho kinachotutofautisha.

Unakumbuka nini siku hiyo?
Nilikuwa shule ya msingi. ITV wakaweka breaking news majengo ya US yanawaka. Zaidi nakumbuka matokeo ya tukio lile. Kila jioni kwe DW na BBC kusikia mabomu Kandahar, Torabora, Falujjah nk.
 
Back
Top Bottom