Tuichunguze tanesco

Mtumiabusara

JF-Expert Member
Nov 18, 2009
473
40
TANESCO, shirika la umma linafanya biashara isiyo na ushindani katika nchi hii. Wanakusanya bili prepaid (LUKU) lakini huduma bado ni utata. Tunafahamu wana wataalamu wa kila aina mfano wataalam wa umeme, uhasibu, masoko, sheria nk. Maswali tunayojiuliza:

  1. Mvua isiponyesha, umeme mgao, je hawajui kuwa mvua ina msimu?
  2. More than 20 yrs vyanzo vya umeme wa maji unaweza kukuta ni vilevile, kidatu, mtera nk. Je wanashindwaje kutafuta vyanzo vipya wakati kila siku wanapata wateja wapya, mapato yanaongezeka lakini wao wanatumia mtaji ule ule? hii ni aina gani ya biashara?
  3. Sina data za kutosha, lakini tetesi zilizopo ni kwamba ghalama za kukodi mitambo ya kuzalisha umeme kwa miaka isiyozidi 3, inazidi gharama ya kununua mitambo yako mwenyewe mipya. Kwa nini tunakodi?
Kwa maoni yangu hili shirika ni bora lingebinafsishwa ili lijitegemee kibiashara, kwa sababu haiingii akilini malipo yawe prepaid (LUKU) alafu umeme mgao. kama maji yamepungua mtera au bwawa limejaa tope hiyo haiwahusu wateja wao, ilitakiwa wao ndo watafute magenereta kuhakikisha sisi tunapata umeme kwa gharama ileile.
 
Back
Top Bottom